Dhana ya uhujumu uchumi na mrundikano wa mahabusu

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,000
Sasa hivi kila mtu ni mtakatishaji fedha na muhujumu uchumi na hakuna dhamana kwao. Ukijiuliza haya makosa yanatokea wapi unagundua DPP ndizo kesi anazofungua baada ya kujua akifika mahakamani anakwenda kukataa wahusika wasipewe dhamana.

Leo hii hata ukipewa maelekezo haramu ukayakataa kitakachofuata ni kufunguliwa uhujumu uchumi ukose dhamana na ndugu zako pamoja na familia wakae meza moja na wakubwa wajadiliane.

Uhujumu uchumi imekuwa ni kigezo Cha serikali kudai rushwa kwa wananchi na wakaazi wa Tanzania na kibaya zaidi wanaoomba fedha wamehalalisha mtindo kwa kusaidiwa na mahakama.

Ifike mahali mawakili wasomi wakaona ni namna gani wanazipitia sheria zinazowanyima watu ambao ni watuhumiwa dhamana kuepusha kazia hii.

Sheria hizi Leo zinaonekana ni tamu kwa watawala na baadhi ya watendaji mahakamani hawazioni kama ni tatizo hadi pale watakapokamatwa na kutundikiwa dripu ya uhujumu uchumi ndo watatambua madhara yake.

Ni vyema tukaandaa mazingira ya kisheria yaliyosafi Sasa kabla hatujaumizwa na sheria tunazoona leo si kandamizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
Ndo madhara ya kutokuwapo kwa utawala wa Sheria, uhujumu uchumi ni fimbo ya kupigia pesa, na kama njia ya kuwasulubu wengine, wengine wanawekwa ndani ili nje biashara zao zifilisike kwa kukosa usimamizi wao.hizi dhuluma dhidi ya wanadamu wenzetu ndizo uleta laana ktk nchi
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
Hizi Sheria za kikoloni tungejaribu kuzitupa ndizo ziletazo laana ktk nchi na kufanya kila tufanyalo linafail halina baraka sababu ya dhuluma dhidi ya wengine.Nchi nyingi kesi ya mauaji tu ndio haina dhamana zingine zote zinadhaminika.Unakuta MTU ni Mtz na ana Mali mara mia zaidi ya anachotuhumiwa nao laki moja kwa Milioni 10 kwann usizuie hizi Milioni 10 hadi MTU apambane na kesi zake.Hizi utasikia sijui DPP hana nia ya kuendelea nayo tafsiri yake jamii uona huyu alionewa kumbe.
 
ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,086
2,000
Muda wa kuondoa sheria hizi bado haujafika hadi zitakapompata Jaji Mkuu akafungwa na kunyimwa dhamana vinginevyo sijui.
Waliozishabikia asa wabunge vipofu wa sisiemu zishaanza kuwang'ata lakini bado wanawaza kwa mtumbo. Adhabu yao ni kansa, pressure, ukimwi na magonjwa yasiyopona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiraremapojoni

JF-Expert Member
Nov 30, 2018
389
500
hakuna masika yakosayo mbu kubwa ni subira kwani kula giza linapozidi kuwa kali sana ndio mapambazuko yanapokaribia. Ila nami nashangaa sana aina hii ya kesi mana katika tawala zilizopita hakujawahi kutokea kadhia hii na kama ilikuwepo basi sio kwa kasi ya ajabu kama awamu hii. Hakika kuna farajakubwa sana kwa watanzania itakayokuja baada ya dhuluma hii wanayotendewa wenzetu
 
Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
3,462
2,000
mawakili, wanasheria akina fatma karume wanashinda twitter kuandika mipasho . mambo kama haya ndio walitakiwa wayatee. lile TLS sijui lina kazi gani
 
PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,954
2,000
Mimi si laumu mahakama. maana mahakama sio watunga sharia, watunga sharia ni Bunge.

Mimi sikatai kutungwa sharia ya uhujumu uchumi. Ila sharia hii ingeweka mkazo kwa DPP Kuwa jibika kwa weledi. Maana si vizuri kumkamata mtu ukamtia ndani mwaka mzima kwa kisingizio cha bado uchunguzi unaendelea! Sasa ulimkamataje mtu kabla ujakamilisha uchunguzi?

Mimi kwa uelewa wangu mdogo. Najua mtu upelekwa mahakamani baada ya kukamisha uchunguzi na kuhuwasilisha mahakamani. Ili mahakama itafsiri na kutoa hukum. Lakini sikubaliani na kumkamata mtu kumweka ndani mwaka 1 eti uchunguzi haujakamilika, hii si sawa.
 
Wenzetu huwezi kukaa ndani kama uchunguzi ujakamilika,wao uchunguzi kwanza,sisi uoze ndani kwanza ili Furaha ya MTU itimie kwanza.
 
boaz mwalwayo

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
5,769
2,000
Ndo maana mpaka mda huu naamini kwamba Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenyewe haiwezekani sheria kandamizi kama hizi ziendelee kuepo nchini alafu awamu ya Tano kuhujumu Uchumi ndo kauli mbiu yao wakitaka ukose dhamana mahakamani
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
Sasa hivi kila mtu ni mtakatishaji fedha na muhujumu uchumi na hakuna dhamana kwao. Ukijiuliza haya makosa yanatokea wapi unagundua DPP ndizo kesi anazofungua baada ya kujua akifika mahakamani anakwenda kukataa wahusika wasipewe dhamana.

Leo hii hata ukipewa maelekezo haramu ukayakataa kitakachofuata ni kufunguliwa uhujumu uchumi ukose dhamana na ndugu zako pamoja na familia wakae meza moja na wakubwa wajadiliane.

Uhujumu uchumi imekuwa ni kigezo Cha serikali kudai rushwa kwa wananchi na wakaazi wa Tanzania na kibaya zaidi wanaoomba fedha wamehalalisha mtindo kwa kusaidiwa na mahakama.

Ifike mahali mawakili wasomi wakaona ni namna gani wanazipitia sheria zinazowanyima watu ambao ni watuhumiwa dhamana kuepusha kazia hii.

Sheria hizi Leo zinaonekana ni tamu kwa watawala na baadhi ya watendaji mahakamani hawazioni kama ni tatizo hadi pale watakapokamatwa na kutundikiwa dripu ya uhujumu uchumi ndo watatambua madhara yake.

Ni vyema tukaandaa mazingira ya kisheria yaliyosafi Sasa kabla hatujaumizwa na sheria tunazoona leo si kandamizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mdogo wake ROSTAM kesi ya uhujumu uchumi ikawa ya kama kukamatwa ugoni
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom