Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,635
- 729,545
Kaburi linachukuliwa kama nyumba ya milele kwa wafu lakini uhai wa mwili mfu kaburini si zaidi ya miaka 20, labda ile kumetumika njia maalum za kuhifadhi mwili husika
Sehemu nyingi leo hii zilizokuwa makaburi zimebadilishwa matumizi na kufanyiwa uwekezaji mwingine japo huwa na matukio mbalimbali
Maana yake iko hivi, roho nyumba yake ni huu mwili uharibikao na baada ya roho kutengana na mwili, mwili husika huzikwa (kwa ile miili inayobahatika kuzikwa)...kiroho na katika dunia isiyoonekana pale kaburini ndio huwa pia makazi ya roho husika kwenye ule mwili unaoendelea kuoza na kuharibika kabisa
Kama palichaguliwa hapo kama makazi ya milele kuja kuparudia bila utaratibu ni kuingilia makazi ya wenyewe bila ruhusa....ndio maana sehemu kama hizo huwa na matukio mengi hasa vifo na ajali
Kilichowekwa pale ni mwili mfu lakini kuna roho isiyokufa ipo pale na ukitaka kupaingilia kuna taratibu maalum za ibada, kafara na matambiko hufanyika ili kuomba ruhusa ya roho husika zihame ili kuepusha madhara mbeleni....mkikosea kwenye hilo tarajieni mengi
Mwananyamala hospital imejengwa juu ya makaburi bila kufuata utaratibu