Dhana ya mwanamke kuzeeka mapema na 'age difference' katika ndoa

Dhana ya mwanamke kuzeeka mapema na 'age difference' katika ndoa

none of the above.

Nazani hapa tunahitaji majibu yakisayansi kutoka kwa wanasayansi.

Tusubiri.
 
ni kweli mwanamke anachoka mwili mapema kutokana na majukumu yake
 
  • Wanaume wanawahi kufa kwasababu wengi hawajatulia viruka njia,asilimia kubwa ya wanaume wana wanawake wengi na hii tangia enzi za babaangu tofauti na sasa wanaume na wanawake wapo level moja hasa kwenye suala la michepuko.

Hivi michepuko huleta kifo haraka?
 
Tafsiri ya kujipenda eti ni kuvaa nguo tena kwa fashion,kupaka poda,kuonekana sana burger point,mawigi ya brazil na kutupia tupicha instagram na whatsaap ukila pizza

Ukimwambia mdada kujipenda ni kuzingatia ulaji unaofaa kiafya,lifestyle,kuepuka cosmetics zenye kemikali hatarishi.utasonywa.nyooo

hahahaha!!! chezeiya manyama choumer. ila acheni masihara, ukiwa na hela itachukua muda mrefu sana hadi uzeeke.
 
dalili kuu ya kumhusisha mtu na Uzee ni ngozi ya mwili kusinyaa.
Kiukweli ngozi za wanawake zinaweza kuwa zinaharibiwa na madawa mengi wanayopaka mpaka ngozi inachoka yenyewe. ukichanganya miili yao hawataki itoke jasho na ina lundo la mafuta na sometimes manyama uzembe yameachiwa yakalepeta mpaka basi.
Na kama ni wale wanawake wanaofanya kazi za -sedentary(kukaa ofisini nakula kiyoyozi bila kutumia nguvu na nyumbani kuna hausigeli).inamzuia kupata hata zoezi kidogo. Hivyo kinachowatokea sana sana sio Uzee bali kukata ringi mapema.

Mazoezi ni njia bora ya kuonekana mrembo zaidi. na waache ama wapunguze pombe kwani sukari ya pombe( polysaccharide) inafanya ngozi kusinyaa. Hapa nawagusia wale wasio na stress na misongo ya mawazo, lakini wanajikuta wanachoka mapema kupitia life style.

pia kuna tabia ya wanawake kuzaa sana kama kuku na vifaranga, ni wazi atachoka tu.

Vilevile wakati fulani women are not that much happy and wanaishi kwa hofu sana na mawazo kuliko wanaume.Mtu wa hivi hata ukijidanganya umepeleke mazoezi ni wazi hataweza ku-concentrate.wanapaswa kuishi positive life. japo sio kazi rahisi ku-manipulate mind
 
Back
Top Bottom