Dhana ya mwanamke kuzeeka mapema na 'age difference' katika ndoa

Dhana ya mwanamke kuzeeka mapema na 'age difference' katika ndoa

GKM

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2012
Posts
738
Reaction score
332
Wakuu habarini..

Kuna dhana imejengeka sana hasa huku afrika kwetu kwamba mwanamke huzeeka mapema! Je swala hili ni kweli? na kama ni kweli huwa inasababishwa na nini? Mbona data zinaonesha wanaume wanawahi kufa (hata kwa uzee) kuliko wanawake?

Kutokana na 'imani' hiyo, je, mwanamke anapokua mkubwa kiumri (tofauti ya 1-3 years) kuliko mwanaume katika ndoa kuna madhara gani?

Nawasilisha wakuu
 
Kwa nini haya mawazo yapo afrika zaidi?
 
mi hata sielewi juu ya hili,nasubiri shule wakuu
 
Sijui hizo takwimu zako ni za lini kwa kufikiria juu juu tu naweza mwanamke anazeeka haraka kwasababu
  • Anazaa kwa hio mwili unakongoroka!NB:hii inategemea na mwili wa mtu na jinsi anavyojiweka kama ni hodari wa kufanya mazoezi au mtu active katu hilo si tatizo.
  • Mawazo na stress za maisha zinazeesha pia.

  • Wanaume wanawahi kufa kwasababu wengi hawajatulia viruka njia,asilimia kubwa ya wanaume wana wanawake wengi na hii tangia enzi za babaangu tofauti na sasa wanaume na wanawake wapo level moja hasa kwenye suala la michepuko.
  • Wanaume wengi pia wanajilemaza wanamalizwa na lifestyle diseases kuona ujiko kuwa na kitambi,wanaongeza risk ya kupata atheroscleorosis (heart diseases) ,high blood presser na wengi wao wanavuta sigara wanaongeza risk ya kupata high cholesterol again heart disease na matatizo ya mapafu!
  • Wanaume wanakunywa kwa kiwango kikubwa kuliko wanawake....na kuchosha ini 🙂
 
Sijui hizo takwimu zako ni za lini kwa kufikiria juu juu tu naweza
mwanamke anazeeka haraka kwasababu
1.Anazaa kwa hio mwili unakongoroka!NB:hii inategemea na mwili wa mtu na jinsi anavyojiweka kama ni hodari wa kufanya mazoezi au mtu active katu hilo si tatizo.
2.Mawazo na stress za maisha zinazeesha pia.
Wanaume wanawahi kufa kwasababu wengi hawajatulia viruka njia,asilimia kubwa ya wanaume wana wanawake wengi na hii tangia enzi za babaangu tofauti na sasa wanaume na wanawake wapo level moja hasa kwenye suala la michepuko.
Wanaume wengi pia wanajilemaza wanamalizwa na lifestyle diseases kuona ujiko kuwa na kitambi,wanaongeza risk ya kupata atheroscleorosis (heart diseases) ,high blood presser na wengi wao wanavuta sigara wanaongeza risk ya kupata high cholesterol again heart disease na matatizo ya mapafu!

kwa hiyo mwanamke asipozaa hazeeki mapema relatively to mwanaume?
 
kuna program inaonyeshwa startimes,inaitwa taboo. Pamoja na mengine inaonyesha mahusiano ya men and women yasiyo ya kawaida. Jibu la hoja hii lilionyeshwa jana lakini bado wanaendelea kufafanua. Watch it!
 
kuna program inaonyeshwa startimes,inaitwa taboo. Pamoja na mengine inaonyesha mahusiano ya men and women yasiyo ya kawaida. Jibu la hoja hii lilionyeshwa jana lakini bado wanaendelea kufafanua. Watch it!

hiyo chanel ya 'startimes' kwetu haishiki mkuu, ungetuwekea tu vitu hapahapa
 
Okay,mimi ni mlengwa ktk topic hii,mchumba wangu kanizidi miezi mi3;Labda nikusaidie kutokana na kiwango kidogo cha uelewa wangu mkuu,wanawake wana CHANCE kubwa ya kuzeeka(au kuzeeshwa) mapema kwasababu wanapitia nyakati ngumu sana hasa ile ya Kujifungua..kama utampachika mimba mkeo kila baada ya mwaka unategemea nini?! alafu unakuta mnawatoto 6 au 7..lazma azeeke mapema! lakini pia ugumu wa maisha huchangia! mwanamke anaweza kuwa na mtoto 1 tu lakini kutokana na ugumu wa maisha,hasa wale wanaolea bila msaada toka kwa mumewe.Afrika,ktk jamii nyingi wanawake(hata wakiwa wadogo) wamekuwa wakichukuliwa kama Chombo cha kazi!!! kuanzia kijijini na hata mjini! in that case,majukumu mengi huwakomalisha na kuwadhohofisha mapema,hatimae kuonekana wame "kula chumvi nyingi"..
Mwanamke anahitaji kupendwa,kulindwa,kuheshimiwa n.k (lakini na yeye ajipende,ajitunze na kujiheshimu zaidi) ukimpa vitu kama hivyo,utanipa results.
mfano mzuri;Angelina jolie,Beyonce,my mother! utadhani hawazeeki...!
 
  • Thanks
Reactions: GKM
Hakuna madhara yoyote, ila kwa hali ilivyo wanawake wanachakaa mapema kuliko wanaume
 
Wanazeeka mapema kwa kuwa wanazaa watoto wengi, kazi nyingi, hakuna matunzo na lishe duni. Angalia wanawake wa mjini wa sasa wenye pesa zao na waliozaa watoto wachache akikuambia ana 50 yrs huwezi amini.
 
  • Thanks
Reactions: GKM
Wanazeeka mapema kwa kuwa wanazaa watoto wengi, kazi nyingi, hakuna matunzo na lishe duni. Angalia wanawake wa mjini wa sasa wenye pesa zao na waliozaa watoto wachache akikuambia ana 50 yrs huwezi amini.
Muangalie mdogo wangu OPRAH WINFREY unasemaje mkuu?
 
Wanazeeka mapema kwa kuwa wanazaa watoto wengi, kazi nyingi, hakuna matunzo na lishe duni. Angalia wanawake wa mjini wa sasa wenye pesa zao na waliozaa watoto wachache akikuambia ana 50 yrs huwezi amini.

Kuna wamjini.wale vibonge wanazeeka hao.huwa wanakuja kulia lia hapa JF eti hawaoleki.wanageuzwa nyumba ndogo
 
tatizo si mwanamke, tatizo ni matunzo mabovu anayopewa kiumbe huyu..

kazi nyingi ambazo kaumbiwa mwanaume utakuta anazifanya mwanamke, lazima wazeeke mapema tu!

hali zao nyingi za kiuchumi ni mbovu, wamelimbikiziwa zigo kubwa sana la kutunza familia kubwa ikiwemo na unwanted children from their children...!

mimi naamini kuwa wanawake wote ni sawa, J.LO ni sawa na Shilole... check the difference now, shilole yuko na kitumbo kama chungu! wakati mwenzie yuko healthy tu kutokana na kujua afanye nini na wakati gani.. ELIMU DUNI inahusika!
 
Mwanamke matunzo,, msosi fresh, pesa isiyo ya mawazo, no stress, apate upendo kutoka kwa mwanaume , ajitambue hasa afya ya mwili utamwona anapendeza na hazeeki
Ila kwa haya maisha ya wabongo wengi mtu ana 40 kazeeka kuchujika kama bibi ake utadhani ana 60 yrs
 
  • Thanks
Reactions: GKM
Wanakula ovyo na hawafanyi mazoezi

Tafsiri ya kujipenda eti ni kuvaa nguo tena kwa fashion,kupaka poda,kuonekana sana burger point,mawigi ya brazil na kutupia tupicha instagram na whatsaap ukila pizza

Ukimwambia mdada kujipenda ni kuzingatia ulaji unaofaa kiafya,lifestyle,kuepuka cosmetics zenye kemikali hatarishi.utasonywa.nyooo
 
Back
Top Bottom