Dhana Ya Mpe Mbwa Jina Baya Kisha Mnyonge/Muuwe

Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,837
Likes
1,559
Points
280
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,837 1,559 280
Salaam wanajukwaa!

Bila kupoteza muda wenu au kuwachosha, nilete mbele yenu kwa mjadala dhana hiyo hapo juu.

Uko msemo wa zamani wa Kiingereza unaosema "Give the dog a bad name and hang him"
Ambao kwa tafsiri rahisi ya Kiswahili ni "Mpe (muite) mbwa jina baya kisha mnyonge/muue".

Nimelazimika kutafakari, kupambanua, kuchambua na kulinganisha mambo ya zama zetu za sasa na kule tunakoelekea kama jamii na Taifa, nikaona huo msemo una nafasi yake.
Moja ya neno linaloendelea kupata nguvu na lisipokemewa litakuja kuwa majuto kwa Taifa letu siku za usoni....ni hii tabia ya ku-attach kila kitu na dili. Kila kitu sasa hivi kinahusishwa na dili na watu wanachinjiwa baharini on the spot! Haki hakuna tena. Ukweli hauna nafasi kabisa. Imekuwa kama ni mwonekano mpya wa "mob justice". Safari hii ikifanywa waziwazi na kuonekana kushangiliwa na hadhira bila kujiuliza wala kuhoji sababu hasa ya hamasa na nderemo zao!

Na mbaya zaidi kuna watu (sio wachache) wanaojidanganya kuwa mwisho wa siku mambo yatakuwa sawa na nchi itanyooka na kuwa ya neema!

Niseme tu, ni rahisi sana kuota ndoto mchana, tena ukiwa unakimbia kuliko, kufikia mema kwa njia za uonevu na dhuluma. Uongozi ni lazima uoneshe njia, utende haki, ulinde na kuhifadhi utu na heshima ya raia zake bila kujali jinsia, umri, itikadi au kitu chochote. Hili ni suala mtambuka Kikatiba na Kisheria, sio hisani au mbeleko. Uongozi bora na thabiti utajikita siku zote katika kutoa huduma na kutengeneza fursa katika nyanja za elimu, ulinzi, maendeleo na afya za raia wake.

Kwa bahati mbaya sana inaonekana wananchi wengi hawajipi muda na wajibu wa kuhoji na/au kuchunguza badala yake wanashangalia tu (wanameza). Nawaasa washangiliaji wsisahau kuwa siku moja nao watapewa jina baya na kunyongwa.
 
iparamasa

iparamasa

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Messages
13,457
Likes
14,170
Points
280
iparamasa

iparamasa

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2013
13,457 14,170 280
kila mjasiliamali anayejituma akapata fedha zake anaitwa mpiga dili!

hata mfanyabiashara akisema mzunguko wa fedha hauridhishi,kitu ambacho hata kwenye uchumi kipo,anaitwa mpiga dili
 
Jidu La Mabambasi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Messages
4,868
Likes
4,050
Points
280
Jidu La Mabambasi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2014
4,868 4,050 280
Salaam wanajukwaa!

Bila kupoteza muda wenu au kuwachosha, nilete mbele yenu kwa mjadala dhana hiyo hapo juu.

Uko msemo wa zamani wa Kiingereza unaosema "Give the dog a bad name and hang him"
Ambao kwa tafsiri rahisi ya Kiswahili ni "Mpe (muite) mbwa jina baya kisha mnyonge/muue".

Nimelazimika kutafakari, kupambanua, kuchambua na kulinganisha mambo ya zama zetu za sasa na kule tunakoelekea kama jamii na Taifa, nikaona huo msemo una nafasi yake.
Moja ya neno linaloendelea kupata nguvu na lisipokemewa litakuja kuwa majuto kwa Taifa letu siku za usoni....ni hii tabia ya ku-attach kila kitu na dili. Kila kitu sasa hivi kinahusishwa na dili na watu wanachinjiwa baharini on the spot! Haki hakuna tena. Ukweli hauna nafasi kabisa. Imekuwa kama ni mwonekano mpya wa "mob justice". Safari hii ikifanywa waziwazi na kuonekana kushangiliwa na hadhira bila kujiuliza wala kuhoji sababu hasa ya hamasa na nderemo zao!

Na mbaya zaidi kuna watu (sio wachache) wanaojidanganya kuwa mwisho wa siku mambo yatakuwa sawa na nchi itanyooka na kuwa ya neema!

Niseme tu, ni rahisi sana kuota ndoto mchana, tena ukiwa unakimbia kuliko, kufikia mema kwa njia za uonevu na dhuluma. Uongozi ni lazima uoneshe njia, utende haki, ulinde na kuhifadhi utu na heshima ya raia zake bila kujali jinsia, umri, itikadi au kitu chochote. Hili ni suala mtambuka Kikatiba na Kisheria, sio hisani au mbeleko. Uongozi bora na thabiti utajikita siku zote katika kutoa huduma na kutengeneza fursa katika nyanja za elimu, ulinzi, maendeleo na afya za raia wake.

Kwa bahati mbaya sana inaonekana wananchi wengi hawajipi muda na wajibu wa kuhoji na/au kuchunguza badala yake wanashangalia tu (wanameza). Nawaasa washangiliaji wsisahau kuwa siku moja nao watapewa jina baya na kunyongwa.
Tuanze na maana halisi ya kupiga dili.
Kiuhalisia maana yake nini?
Isije changanywa na biashara halali?
 
B

babrau

Member
Joined
Nov 27, 2016
Messages
57
Likes
16
Points
15
Age
58
B

babrau

Member
Joined Nov 27, 2016
57 16 15
Bunge lilizimiwa vipaza sauti na kuoneshwa live ilikuwa mwanzo wa jibwa kupewa jina baya. Yanayoendelea usishangae tuombe salama 2020 uchaguzi ujao.
 
kivyako

kivyako

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Messages
13,390
Likes
9,543
Points
280
kivyako

kivyako

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2012
13,390 9,543 280
Eti na Dangote alikuwa mpiga dili tu
 
M

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Messages
2,904
Likes
2,151
Points
280
M

MIGNON

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2009
2,904 2,151 280
Salaam wanajukwaa!

Bila kupoteza muda wenu au kuwachosha, nilete mbele yenu kwa mjadala dhana hiyo hapo juu.

Uko msemo wa zamani wa Kiingereza unaosema "Give the dog a bad name and hang him"
Ambao kwa tafsiri rahisi ya Kiswahili ni "Mpe (muite) mbwa jina baya kisha mnyonge/muue".

Nimelazimika kutafakari, kupambanua, kuchambua na kulinganisha mambo ya zama zetu za sasa na kule tunakoelekea kama jamii na Taifa, nikaona huo msemo una nafasi yake.
Moja ya neno linaloendelea kupata nguvu na lisipokemewa litakuja kuwa majuto kwa Taifa letu siku za usoni....ni hii tabia ya ku-attach kila kitu na dili. Kila kitu sasa hivi kinahusishwa na dili na watu wanachinjiwa baharini on the spot! Haki hakuna tena. Ukweli hauna nafasi kabisa. Imekuwa kama ni mwonekano mpya wa "mob justice". Safari hii ikifanywa waziwazi na kuonekana kushangiliwa na hadhira bila kujiuliza wala kuhoji sababu hasa ya hamasa na nderemo zao!

Na mbaya zaidi kuna watu (sio wachache) wanaojidanganya kuwa mwisho wa siku mambo yatakuwa sawa na nchi itanyooka na kuwa ya neema!

Niseme tu, ni rahisi sana kuota ndoto mchana, tena ukiwa unakimbia kuliko, kufikia mema kwa njia za uonevu na dhuluma. Uongozi ni lazima uoneshe njia, utende haki, ulinde na kuhifadhi utu na heshima ya raia zake bila kujali jinsia, umri, itikadi au kitu chochote. Hili ni suala mtambuka Kikatiba na Kisheria, sio hisani au mbeleko. Uongozi bora na thabiti utajikita siku zote katika kutoa huduma na kutengeneza fursa katika nyanja za elimu, ulinzi, maendeleo na afya za raia wake.

Kwa bahati mbaya sana inaonekana wananchi wengi hawajipi muda na wajibu wa kuhoji na/au kuchunguza badala yake wanashangalia tu (wanameza). Nawaasa washangiliaji wsisahau kuwa siku moja nao watapewa jina baya na kunyongwa.
Nimeisikiliza clip ya Makonda akimwita afisa ardhi kichaa,tone aliyokuwa anatumia na maneno yake nahisi ya kuwa tunakoelekea siko.
Hivi hizi taratibu ziliwekwa za nini za nini ikiwa kero zote zitakuwa zinatatuliwa jukwaani bila kumpa mtuhumiwa nafasi na yeye kujitetea?
Cha kushangaza zaidi ni umati uliokuwa unashangilia.Hii iltokea daraja la kigamboni na Wilson Kabwe akatumbuliwa na naona watu hawajifunzi.
Nakumbuka maneno ya DR. Msabaha wakati wa sakata la RICHMOND na jinsi alivyoeleza kuhusu KIBR au KIBURI!!!KIBR si sifa ya mtu anayemwamini MUNGU.
 
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Messages
3,701
Likes
6,290
Points
280
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2013
3,701 6,290 280
Mimi nina kiosk changu mtaani, mwaka Jana biashara haikuwa nzuri sana ila kila Siku mauzo hayakupungua 70,000 hadi 90,000 ila tokea mwaka huu mwanzoni sijawahi kufikisha sabini, mwanzoni nilihisi dogo ananipiga ila with time nimegundua ndio hali halisi hata nikiongea na wenye magenge jiran wote wanalia mwingine muuza mbogamboga kila cku zinabaki anamwaga.
 
T

TRUVADA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2014
Messages
4,527
Likes
1,190
Points
280
T

TRUVADA

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2014
4,527 1,190 280
Salaam wanajukwaa!

Bila kupoteza muda wenu au kuwachosha, nilete mbele yenu kwa mjadala dhana hiyo hapo juu.

Uko msemo wa zamani wa Kiingereza unaosema "Give the dog a bad name and hang him"
Ambao kwa tafsiri rahisi ya Kiswahili ni "Mpe (muite) mbwa jina baya kisha mnyonge/muue".

Nimelazimika kutafakari, kupambanua, kuchambua na kulinganisha mambo ya zama zetu za sasa na kule tunakoelekea kama jamii na Taifa, nikaona huo msemo una nafasi yake.
Moja ya neno linaloendelea kupata nguvu na lisipokemewa litakuja kuwa majuto kwa Taifa letu siku za usoni....ni hii tabia ya ku-attach kila kitu na dili. Kila kitu sasa hivi kinahusishwa na dili na watu wanachinjiwa baharini on the spot! Haki hakuna tena. Ukweli hauna nafasi kabisa. Imekuwa kama ni mwonekano mpya wa "mob justice". Safari hii ikifanywa waziwazi na kuonekana kushangiliwa na hadhira bila kujiuliza wala kuhoji sababu hasa ya hamasa na nderemo zao!

Na mbaya zaidi kuna watu (sio wachache) wanaojidanganya kuwa mwisho wa siku mambo yatakuwa sawa na nchi itanyooka na kuwa ya neema!

Niseme tu, ni rahisi sana kuota ndoto mchana, tena ukiwa unakimbia kuliko, kufikia mema kwa njia za uonevu na dhuluma. Uongozi ni lazima uoneshe njia, utende haki, ulinde na kuhifadhi utu na heshima ya raia zake bila kujali jinsia, umri, itikadi au kitu chochote. Hili ni suala mtambuka Kikatiba na Kisheria, sio hisani au mbeleko. Uongozi bora na thabiti utajikita siku zote katika kutoa huduma na kutengeneza fursa katika nyanja za elimu, ulinzi, maendeleo na afya za raia wake.

Kwa bahati mbaya sana inaonekana wananchi wengi hawajipi muda na wajibu wa kuhoji na/au kuchunguza badala yake wanashangalia tu (wanameza). Nawaasa washangiliaji wsisahau kuwa siku moja nao watapewa jina baya na kunyongwa.
lakini tusema ukweli nchi ilikuwa imefika pabaya nakumbuka 2014, wakati ESTA bulaya akichangia alisema nchi kila mradi ni dili , kila kitu ni dili , bandari dili, TRA, dili NSSF madili, TBS WATUMISHI HEWA DILI dili , sasa mahela ya madili kwa kiasi fulani yaliwatukia manyoka kama sisi tukajiona na sis tuna neema , kwa hiyo dili zilikuwepo mkuu USIBISHE
 
M

mtogapelu

Member
Joined
Oct 21, 2016
Messages
38
Likes
13
Points
15
Age
49
M

mtogapelu

Member
Joined Oct 21, 2016
38 13 15
Waswahili wanasema mbwa ukimjua jina hakusumbui wenye akili wamewajua watanzania.Namnukuu Mzee Mengi hakuna ulemavu mbaya kama wa fikraha,mwisho wa kunukuu.God is able.
 
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,837
Likes
1,559
Points
280
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,837 1,559 280
lakini tusema ukweli nchi ilikuwa imefika pabaya nakumbuka 2014, wakati ESTA bulaya akichangia alisema nchi kila mradi ni dili , kila kitu ni dili , bandari dili, TRA, dili NSSF madili, TBS WATUMISHI HEWA DILI dili , sasa mahela ya madili kwa kiasi fulani yaliwatukia manyoka kama sisi tukajiona na sis tuna neema , kwa hiyo dili zilikuwepo mkuu USIBISHE
Hakuna anayekataa kuwa hii nchi kwa muda mrefu ilikuwa shamba la bibi. Hiyo sio hoja ya msingi kwa sababu wakati wapinzani na watu (wengine ndani ya Serikali na CCM) walipiga kelele kuwa nchi inaliwa na mchwa baadhi ya watu ambao leo wanaimba wimbo wa "....nchi ilifika pabaya..." walikataa na kukanusha kwa nguvu nyingi.

Na pia hoja ya kuwa nchi ilifika pabaya ni hoja dhaifu, na haihalalishi baadhi ya matendo na matamko ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Ziko njia zaidi ya mia moja za kushughulika na wale mchwa na wakati huohuo uchumi na utawala wa sheria kuendelea bila bugudha. Uwezo wa kuongoza na kufanikisha mambo muhimu unapimwa kwa vitu vingi, kwa bahati mbaya niseme sina matumaini wala imani kivile na hawa wa sasa pia.

Sioni ni kwanini mpaka sasa Serikali hii imejikita kutazama na kulazimisha milango iliyofungwa ifunguke ilihali kuna milango mingine mingi tu iko wazi.

Ukaguzi, uhakiki, tuhuma, kuteua, kutengua, kukanusha, kutoa matamko nk nk haviponyi ugonjwa wa rushwa na ufisadi. Hizo sio njia za kukabiliana na matatizo mtambuka ya Tanzania. Kwa mfano, kwa nini wasijaribu kufanya haya?:-

1) Rushwa ni zaidi ya vitisho na kutumbua. Rushwa ni jambo lenye kugusa hulka, tabia na weledi wa mtu husika. Rushwa ina hatua na viwango. yaani inaanza kidogo, inakua na mwisho inakomaa.Suala la kushughulikia rushwa (bahati nzuri ziko tafiti na ripoti nyingi makini) kwa sehemu kubwa halijawahi kupewa uzito unaostahili.

Kujenga uwezo wa kitaasisi na kisheria kwa upande mmoja na elimu/mafunzo ya kimaadili kwa upande wa pili ndio jawabu sahihi la kupambana na rushwa. Rushwa kupambana nayo inahitaji zaidi ya nguvu au utashi wa mtu au watu wachache. Inahitaji mada ya kivyake.

2) Utumishi - Ni siri iliyo wazi kuwa wafanyakazi wengi wa Serikali wa ngazi za juu mpaka chini hawana mafunzo, maadili, weledi na uwezo stahiki. Na kuongeza chumvi kwenye kidonda wengi hawana motisha/morali ya kazi. Watanzania kwa asili yetu hatuheshimu wala kuthamini kazi, tunachukulia kazi kama kijiweni au mahali tu pa kupoteza muda. Sasa huwezi kubadilisha utamaduni huo ghafla na kwa vitisho. Ni suala la kujenga watoto toka shule za msingi hadi vyuo na pia majumbani mwetu wapende kufanya kazi. Wakipenda kufanya kazi watajenga uwezo na mapenzi na taaluma zao, watakuwa na weledi na ubunifu katika kazi na maisha yao hivyo tija itakuwa bora.

Vyuo vya utumishi navyo sio vya kiwango. Marekebisho yanatakiwa kila nyanja na yaende kwa hatua na wakati sio matamko, vitisho nk

3) Kodi - kabla ya kuhangaika kukamua wananchi wa kawaida Serikali yetu ingetazama mambo mengi ambayo kwanza yamechangia watu kutopenda/kukwepa kulipa kodi. Mosi ni elimu ya kodi; pili viwango vya kodi (ni vikubwa); tatu umangimeza usio na tija; nne utitiri wa kodi, ada na tozo; tano mafunzo kwa maofisa wa kodi, sita yajengwe mahusiano kati ya mlipaji na mpokeaji.

TRA na Serikali hawatakaa wafanikiwe kwenye kodi (sahau mafanikio ya kwenye makaratasi) kwa njia wanazotumia sasa kwa sababu binadamu wote wamepewa uwezo wa akili, wakizitumia vibaya basi huo mtafutano hauna mshindi.

4) Uchumi - Uchumi una pande kuu mbili; macro na micro economies. Uchumi ili ukue na kustawi lazima kila mdau (Serikali na Sekta Binafsi) washirikiane na kuonekana kuwa wanashirikiana. Hakuna upande mmoja usiomhitaji mwingine. Ni dhana potofu tu kudhani kuwa unaweza kukiuka au kupuuza misingi na kanuni za uchumi halafu ukabaki salama.

Nitoe rai na maombi kwa Serikali yetu ya Awamu ya Tano, msipuuze kilio na maumivu mnayosikia wananchi wa kawaida wanayougulia. Kila siku moja inayopita uchumi na pato la mtu wa kawaida unazidi kudidimia. Chukueni hatua haraka kurekebisha kasoro zilizoko. Kumbukeni ni rahisi sana kubomoa lakini ni ngumu sana kujenga.
 
Forum statistics

Threads 1,274,136
Members 490,601
Posts 30,502,217