Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,299
- 3,055
Salaam wanajukwaa!
Bila kupoteza muda wenu au kuwachosha, nilete mbele yenu kwa mjadala dhana hiyo hapo juu.
Uko msemo wa zamani wa Kiingereza unaosema "Give the dog a bad name and hang him"
Ambao kwa tafsiri rahisi ya Kiswahili ni "Mpe (muite) mbwa jina baya kisha mnyonge/muue".
Nimelazimika kutafakari, kupambanua, kuchambua na kulinganisha mambo ya zama zetu za sasa na kule tunakoelekea kama jamii na Taifa, nikaona huo msemo una nafasi yake.
Moja ya neno linaloendelea kupata nguvu na lisipokemewa litakuja kuwa majuto kwa Taifa letu siku za usoni....ni hii tabia ya ku-attach kila kitu na dili. Kila kitu sasa hivi kinahusishwa na dili na watu wanachinjiwa baharini on the spot! Haki hakuna tena. Ukweli hauna nafasi kabisa. Imekuwa kama ni mwonekano mpya wa "mob justice". Safari hii ikifanywa waziwazi na kuonekana kushangiliwa na hadhira bila kujiuliza wala kuhoji sababu hasa ya hamasa na nderemo zao!
Na mbaya zaidi kuna watu (sio wachache) wanaojidanganya kuwa mwisho wa siku mambo yatakuwa sawa na nchi itanyooka na kuwa ya neema!
Niseme tu, ni rahisi sana kuota ndoto mchana, tena ukiwa unakimbia kuliko, kufikia mema kwa njia za uonevu na dhuluma. Uongozi ni lazima uoneshe njia, utende haki, ulinde na kuhifadhi utu na heshima ya raia zake bila kujali jinsia, umri, itikadi au kitu chochote. Hili ni suala mtambuka Kikatiba na Kisheria, sio hisani au mbeleko. Uongozi bora na thabiti utajikita siku zote katika kutoa huduma na kutengeneza fursa katika nyanja za elimu, ulinzi, maendeleo na afya za raia wake.
Kwa bahati mbaya sana inaonekana wananchi wengi hawajipi muda na wajibu wa kuhoji na/au kuchunguza badala yake wanashangalia tu (wanameza). Nawaasa washangiliaji wsisahau kuwa siku moja nao watapewa jina baya na kunyongwa.