Dhana ya kuombewa

Dhana ya kuombewa

Labda tumuombee afe mapema hakuna namna ,na asidhani yuko huru kutulazimisha tumuombee ahaaa sio kwa kiwango hicho
 
17554315_1302149159870920_2310389317293388067_n.jpg
 
Ni neno la kawaida la kiimani kwa wale waamini na waaminio. Lakini awamu hii ya tano linaelekea kupata umaarufu
Nimejikuta napitia makabrasha mbalimbali ya kidini kuona ni nani wanaopaswa kuombewa na kwanini
.wagonjwa
.yatima
.Wajane
.wenye shida za kiroho
.wenye shida za kimwili
Hawa ndio tmefundishwa kuwaombea kwa imani ya kikristo
Lakini vile vile tuna maombi na sala maalum za kuombea Taifa na viongozi wake wote ...tuna maombi na sala rasmi kila siku ikianza na kila siku ikiisha
Napatwa na ukakasi mkubwa kuendelea kuombwa nimuombee mtu mwenye kila aina ya ulinzi kuanzia wa mitambo mpaka wa majeshi na usalama
Napatwa na mshangao kuendelea kuombwa nimuombee mtu ambaye hajui bajeti yake ya mahitaji ya kila siku kuanzia chakula usafiri ada za watoto shule , mahitaji ya ndugu na jamaa nk nk..vyote hivi anavipata bure na ziada
Hii ni aina fulani ya uchoyo na ubinafsi uliopitiliza...! Hivi yule mgonjwa pale Hospitali ataombewa na nani? Je yule mjane aliyedhulumiwa nyumba na mirathi yake yeye ataombewa na nani?
Nchi imezungukwa na matatizo na shida kila mahali ni vilio na maumivu...maisha magumu hela hakuna kazi hakuna....hawa ndio waombe? Wamuombee asiye na dhiki wala changamoto za maisha yetu haya???jamani mbona mnatuonea na kututia majaribu ni tumkufuru Muumba wetu
Yani kweli kabisa nitoke Muhimbili kumuangalia mgonjwa wangu ninayetakiwa kutafuta pesa ili aweze kutibiwa huku nadaiwa kodi ya nyumba na ada za watoto na mengine mengi...na uchovu wote na changamoto zote hizi halafu niombwe kumuombea mtu ambaye hata nilitaka kuonana naye siwezi? Kweli dunia ina mengi
Uongozi wa nchi ni uongozi wa kisiasa...michezo ya kisiasa inajulikana pote duniani ni michafu tena huku Africa ndio kabisa...kumhusisha Mungu kwenye mambo ya kisiasa ni kumdhihaki
Mtu Hapaswi kuwa na wasiwasi...kama una imani kwa Mungu wako na utendalo ni sahihi hata Mungu anajua , hupaswi kuwa na wasiwasi kwakuwa yeye hachagui wala habagui...na ukitenda kwa haki mkono wake utakuepusha na mabaya yote na malaika mlinzi atakuwa nawe bila hata maombi ya mzinifu, muongo, mtenda dhambi zote....
Mtaji Kwa VIONGOZI wetu wa kisiasa karibu ulimwenguni kote.....( hasa wale wenye imani ya KATOLIKI) wengi wao hutumia kanisa kama jukwaa na waumini kama wapiga Kura.

Hi kauli ya NIOMBEENI ni kauli inayosimama kisiasa zaidi kuliko dhamira na nia ya kweli toka moyoni..
 
6a1674e2a83750210f3c3197ec746924.jpg

Mshana,,unachanganya kati ya natural and super natural life,,,,,lengo la sala ni kumuunganisha mtu na Mungu, lengo la sala sio kumbadili maskini awe tajiri!,japo inawezekana,,,,haimaanishi mwenye mahitaji yote ya kimwili automatically mbingu ni yake,ndiyo maana kuna maskini wa mwili na maskini wa roho,,,,,,mwenye yote hayo uliyotaja anaweza kuwa very poor kiroho hivyo kuhitaji Sala huenda kuliko hata maskini wa mali unayedhani ndiye wa kuombewa, labda ungeandika hivi,,,,,,,,,,,,,,pamoja na kumuombea kiongozi pia viongozi wa dini waendelee kumshauri,kwani mara kadhaa unaona kabisa hapa hakupaswa kufanya hivi
 
Tuyaombee makinia yasiwe mada badala yake tuombee almasi dhahabu nk vinavyobebwa direct daily toka machimbo

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ni neno la kawaida la kiimani kwa wale waamini na waaminio. Lakini awamu hii ya tano linaelekea kupata umaarufu
Nimejikuta napitia makabrasha mbalimbali ya kidini kuona ni nani wanaopaswa kuombewa na kwanini
.wagonjwa
.yatima
.Wajane
.wenye shida za kiroho
.wenye shida za kimwili
Hawa ndio tmefundishwa kuwaombea kwa imani ya kikristo
Lakini vile vile tuna maombi na sala maalum za kuombea Taifa na viongozi wake wote ...tuna maombi na sala rasmi kila siku ikianza na kila siku ikiisha
Napatwa na ukakasi mkubwa kuendelea kuombwa nimuombee mtu mwenye kila aina ya ulinzi kuanzia wa mitambo mpaka wa majeshi na usalama
Napatwa na mshangao kuendelea kuombwa nimuombee mtu ambaye hajui bajeti yake ya mahitaji ya kila siku kuanzia chakula usafiri ada za watoto shule , mahitaji ya ndugu na jamaa nk nk..vyote hivi anavipata bure na ziada
Hii ni aina fulani ya uchoyo na ubinafsi uliopitiliza...! Hivi yule mgonjwa pale Hospitali ataombewa na nani? Je yule mjane aliyedhulumiwa nyumba na mirathi yake yeye ataombewa na nani?
Nchi imezungukwa na matatizo na shida kila mahali ni vilio na maumivu...maisha magumu hela hakuna kazi hakuna....hawa ndio waombe? Wamuombee asiye na dhiki wala changamoto za maisha yetu haya???jamani mbona mnatuonea na kututia majaribu ni tumkufuru Muumba wetu
Yani kweli kabisa nitoke Muhimbili kumuangalia mgonjwa wangu ninayetakiwa kutafuta pesa ili aweze kutibiwa huku nadaiwa kodi ya nyumba na ada za watoto na mengine mengi...na uchovu wote na changamoto zote hizi halafu niombwe kumuombea mtu ambaye hata nilitaka kuonana naye siwezi? Kweli dunia ina mengi
Uongozi wa nchi ni uongozi wa kisiasa...michezo ya kisiasa inajulikana pote duniani ni michafu tena huku Africa ndio kabisa...kumhusisha Mungu kwenye mambo ya kisiasa ni kumdhihaki
Mtu Hapaswi kuwa na wasiwasi...kama una imani kwa Mungu wako na utendalo ni sahihi hata Mungu anajua , hupaswi kuwa na wasiwasi kwakuwa yeye hachagui wala habagui...na ukitenda kwa haki mkono wake utakuepusha na mabaya yote na malaika mlinzi atakuwa nawe bila hata maombi ya mzinifu, muongo, mtenda dhambi zote....

......Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. (mathayo 5: 43&44)
 
Mnaomba weeee...kesho tu wakati mnangojea majibu ya maombi yenu kwa Mungu juu ya aliyeomba kuombewa mara mliyekuwa mnamwombea anajitokeza hadharani anafoka..."mimi sijaribiwi", "...mtu yeyote asiyeungana nami katika vita hii ya kiuchumi lazima aondolewe", "... kamanda...kwa nini usiwapige hao wanaokukwamisha..."
Halafu anamalizia kwa kusema; "msema kweli ni mupenzi wa mungu"
 
Jamiiforum ina watuuuuu!! Raha sn
 
Ndiyo maana Ukristo ni dini tofauti. Ukristo unafundisha kumbariki anayekulani, kumpenda adui, kumwombea unayemwona anatenda dhambi. Ila maombi ya fisadi ni kutubu tu. Yaani aombe Mungu amsamehe na amwondoe kwenye ufisadi. Hspaswi kuudanganya moyo wake.
 
watanzania wenzangu, niwasihi na niwaombe mniombee sana..... Soma kwa rafudhi ya magufur
 
Mnaomba weeee...kesho tu wakati mnangojea majibu ya maombi yenu kwa Mungu juu ya aliyeomba kuombewa mara mliyekuwa mnamwombea anajitokeza hadharani anafoka..."mimi sijaribiwi", "...mtu yeyote asiyeungana nami katika vita hii ya kiuchumi lazima aondolewe", "... kamanda...kwa nini usiwapige hao wanaokukwamisha..."
Halafu anamalizia kwa kusema; "msema kweli ni mupenzi wa mungu"
Baada ya maneno hayo Tundu Lissu anapigwa risasi za kutosha. Kweli hamna uovu ambao hauchi alama za mhusika
 
Mtaji Kwa VIONGOZI wetu wa kisiasa karibu ulimwenguni kote.....( hasa wale wenye imani ya KATOLIKI) wengi wao hutumia kanisa kama jukwaa na waumini kama wapiga Kura.

Hi kauli ya NIOMBEENI ni kauli inayosimama kisiasa zaidi kuliko dhamira na nia ya kweli toka moyoni..
Hivi tukiwa tunamuombea atavua zile hirizi?
 
Back
Top Bottom