Dhana ya kulipa kisasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana ya kulipa kisasi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Shy, Oct 24, 2008.

 1. Shy

  Shy JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,238
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  ni mara ngapi hujawatendea wenzako haki? Mara ngapi umedanganya? Mara ngapi umekosea? Je, na wewe ulipiziwe kisasi? Wakati unajibu hili inakuwa rahisi kwako kuamua kulipiza kisasi au lah.

  Inakuwaje pale unapogundua kwamba mpenzi wako alikusaliti? Uumie ndani kwa ndani, umweleze kuwa unajua alikutenda na kisha umuonye au umlipizie? Kwa kupitia kwa makini vipengele vifuatavyo itakuwa rahisi kwako kujua kitu cha kufanya.

  Ni kweli inauma...
  Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya baada ya kuhisi mpenzi wako anakusaliti ni kufanya uchunguzi. Mchunguze kwa makini, lakini kitu cha kuzingatia ni kwamba unapomchunguza asijue kabisa.

  Ni kweli kwamba baada ya kugundua kama mpenzi wako anakusaliti inauma sana, lakini unatakiwa kutulia na kufikiria kwa makini kitu cha kufanya kuliko kuwaza jinsi gani na wewe utakavyoweza kumlipiza kisasi. Kimsingi suala la kulipa kisasi siyo zuri kwako wewe uliye katika uhusiano na mpenzi uliyegundua kwamba anakusaliti. Kwa ufafanuzi zaidi, pitia kipengele kinachofuata.

  UNAJIONGEZEA MAUMIVU...
  Ukweli ni kwamba utakapowaza juu ya kulipa kisasi ni mwanzo wa kuitesa akili yako pamoja na kujiongezea maumivu moyoni mwako. Kuna mambo mengi sana ya kufanya kuliko kuwaza kisasi. Utakapokuwa na nia ya kulipa kisasi ni wazi kwamba utakuwa tayari kufanya mapenzi na mwanamke/mwanaume yeyote atakayetokea mbele yako jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha yako.

  Usiuumize moyo wako, tulia kwanza, weka mipango yako achana na kuwaza mambo ya visasi, sana sana utakuwa unapoteza muda wako bure.
  ZUNGUMZA NAYE...

  Hii inaweza kuwa dawa bora zaidi kuliko zote! Baada ya kuchunguza na kugundua ni kweli mpenzi wako alikusaliti, huna sababu ya kujiumiza zaidi, zungumza naye. Katika mazungumzo yako na wewe, tayari utakuwa umeshapanga kitu cha kufanya akilini mwako.

  Wakati mwingine inawezekana umeshagundua kwamba hakufai tena au pengine kwa sababu unampenda na unaamini alifanya kwa bahati mbaya, mazungumzo yenu yaelemee kwenye kumuonesha kwamba kitendo alichofanya siyo kizuri na kwamba unamtaka abadilike haraka kama ni kweli anataka uhai wa penzi lenu.

  “Unajua dear nakupenda sana, sijui kwanini umeamua kunisaliti mpenzi wangu au kuna kitu ulichotaka nikashindwa kukupa? Niambie mpenzi wangu!” Kauli hii ni muafaka kwa mpenzi aliyekusaliti lakini bado una nia ya kuendelea naye.
  Kwa upande wa mpenzi ambaye umegundua ni tabia yake na alikusaliti zaidi ya mara moja, huku nia yako ikiwa ni kuachana, unaweza kumwambia; “Sioni sababu ya kuendelea kuwa na mpenzi msaliti kama wewe. Siwezi kuendelea na wewe tena, ingawa ni kweli moyo wangu unaniuma sana.”

  Unaweza kukosa yote!
  Wataalamu wa Mambo ya Mapenzi wanashauri kwamba, ni vyema kutatua tatizo kuliko kulikuza zaidi. Kitendo cha kuamua kulipiza kisasi kwa kutoka nje ya penzi lako ni makosa makubwa sana. Mambo mawili yanaweza kutokea kutokana na kulipiza kwako kisasi.

  Mpenzi wako anaweza kukuacha lakini huyo mpya uliyeanzisha uhusiano kwa nia ya kulipa kisasi utashindwa kuwa naye katika mapenzi maana humpendi lakini pia yawezekana ukawapoteza wote ukabaki unahangaika. Chagua moja kuliko kulipiza kisasi, ukweli ni kwamba kisasi hakijengi bali kinabomoa.

  J SHULUWA
   
Loading...