Dhana ya kujifukuzisha kazi(absconding) iko vipi?

Ndo maana mi nataka niwe mjasiriamali
 
acha upumbavu eti hakuna sheria inayosema mtumishi aombe ruhusa.wewe umeajiriwa idara gani kwanza tuanzie hapo
Tatizo mnakariri....!! Lete sheria inayosema lazima mtumishi kuomba ruhusa! Hizi ni taratibu na kanuni ndogondogo za sehemu za kazi. Angalia standing order then unipe kifungu au sheria yoyote inayosema mtumishi lazima uombe ruhusa! Mi nachojua ni kwamba cha muhimu ni kutoa taarifa.....!!!
 
nimepeleka malalamiko cma nimepangiwa tarehe22 march kwa usuluhishi nimejaribu kuongea na mwajiri ili anipatie barua ya kusitisha ajira ili nifatilie mafao yangu nssf amekataa anasema tusubiri maamuzi ya cma ila mimi ndiye mpataji wa shida maana kazi sina familia inazidi kupata shida na mimi kama baba sina ajira
Nashindwa kumuelewa mwajiri nimejaribu kumuomba tuyamalize mimi sikupenda yatokee anipatie barua ya kusitisha ajira hataki
 
Umeishaenda CMA ....stop informal negotiations- not healthy for you case.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na mwajiri tena, hapo yeye ndo ataomba msiende mbali zaidi
Nimeona wengi wamelipwa na hawakua na mkataba,
We una mkataba kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo umejifukuzisha kazi mwenyewe(gross misconduct) tafuta namna nyingine ya kupata kipato, hii inatukumbusha kujiandaa kwa akiba hapo baadae unapopata tatizo

Sababu hata izo Pesa za Nssf unazozitaka hutazipata sasa ivi au mwaka huu,maana kilio chako kikubwa kimeegemea kwenye kukosa pesa ya kulisha familia na sasa hauna so unategemea io ya Nssf

Kampuni za wahindi nyingi zinakuwa na makosa mengi ambapo ukimpata mwanasheria mzuri anaweza kutumia izo loophole Kutengeneza madai juu yao, nafikiri suala lako umelipeleka sehemu sahihi hapo tume ya usuruhishi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…