Na Yahya Msangi (PhD).
Lome - Togo
Nimepitia kurasa mbalimbali za vijana na wengi leo wamelalamikia mishahara kutoongezwa na raisi. Siwalaumu sana kwa kuwa ndivyo walivyoaminishwa na hakuna anayewaelimisha.
Wengi wananukuu au kuongozwa na historia; wananukuu "enzi ya Nyerere". Tatizo ni kutochambua mambo kwa kina.
Mshahara popote duniani huongezwa na mwajiri au mwenye hisa. Mfanyakazi kujiongezea mshahara ni hizaya. Ni uhuni. Uhuni uliopo kwenye mabunge ya nchi nyingi za kiafrika. Ni ndani ya mabunge yetu tumeacha tuliowaajiri kujipangia na kujipandishia mshahara na marupurupu watakavyo. Kipare tunaita THE AFRO CURSE OF PARLIAMENTARY SYSTEM. Nje ya mabunge ya kiafrika hakuna hizaya hiyo.
Enzi za Nyerere ilikuwa sawa kupandisha mishahara siku ya MEI mosi kwa kuwa chini ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kundi la wafanyakazi lilikuwa sehemu ya wenye Mali. Ndio maana kulikuwa na mabaraza ya wafanyakazi yaliyokuwa na mamlaka hadi ya kupanga mapato na matumizi.
Waliofuatia baada yake walianza kuacha huu utaratibu kidogo kidogo kwa kuwa umiliki Mali ulibadilika. Sekta binafsi ilianza kuchukua nafasi yake. Kwa hiyo ni kutofahamu au ujinga au upumbavu kudhani kila MEI Mosi mshahara utaongezwa. Wafanyakazi sio wenye Mali tena.
Na hata serikali imepunguza umiliki wake na kuichia sekta binafsi chini ya dhana ya PPP (Public Private Partnerships). Kwa Leo sitazungumzia mapungufu ya PPPs. PPPs ni hika ya sekta binafsi ikipigiwa upatu na WORLD BANK NA IMF! Ni mbinu mpya ya kuruhusu sekta binafsi ifadhiliwe kwa hela za umma!
Ukitaka kujua MEI MOSI so siku ya kupandisha mshahara tens nchini Tanzania jaribu kujiuliza: hivi so imeadhimishwa note duniani? Ni nchi IPI Ulaya Leo imeongeza mshahara? Je marekani Leo wameongeza dola ngapi kwenye mshahara?Je Japan wameongeza? Kwa nini udhani Tanzania imekosea kutoongeza leo?
Hebu achaneni na ndoto za alinacha. Dunia imebadilika. Hakuna cha nyongeza mshahara siku ya MEI MOSI labda mkubali kurudia SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA!
TUCTA zile hotuba za kudai nyongeza MEI MOSI achaneni nazo. Sasa zama nyingine. Msiimbe kaswida kilabuni! Msiimbe kwaya sokoni! Hailipi tena siku hizi.
Halafu kichekesho ni watu walewale wanaodai hawana ajira ndio wanaolalamika mshahara kutoongezwa!! Walau kwa sasa tuitumie MEI MOSI kudai ongezeko LA nafasi za ajira (employment creation), hifadhi ya jamii (social protection for all), ajira bora na zenye utu (decent work) na ajira zinazojali mazingira (green jobs).
Ujinga Wa kudai nyongeza MEI MOSI tuachane nao. Tukachape kazi makazini mwetu tuongeze tija halafu tutumie ILO Convention Number 98 kujadiliana na waajiri wetu (collective bargaining) nyongeza ya mshahara na marupurupu. Tuache uvivu, wizi, uzembe na kuingiza siasa sehemu za kazi.
Niwatakie MEI MOSI njema waajiriwa na familia zenu! Msio na ajira jitahidini kusoma, kuongeza skills na kukataa kupoteza muda kwenye shughuli zisizo na maana kama MAANDAMANO, MIKUTANO, VIJIWE, MAOMBI, DUA, TUNGURI, MITANDAONI, VILABUNI, SHISHI, n.k.