Dhana potofu: Nyongeza ya mshahara Mei mosi

KADA08

Member
Dec 2, 2017
44
152
Na Yahya Msangi (PhD).
Lome - Togo
Nimepitia kurasa mbalimbali za vijana na wengi leo wamelalamikia mishahara kutoongezwa na raisi. Siwalaumu sana kwa kuwa ndivyo walivyoaminishwa na hakuna anayewaelimisha.

Wengi wananukuu au kuongozwa na historia; wananukuu "enzi ya Nyerere". Tatizo ni kutochambua mambo kwa kina.

Mshahara popote duniani huongezwa na mwajiri au mwenye hisa. Mfanyakazi kujiongezea mshahara ni hizaya. Ni uhuni. Uhuni uliopo kwenye mabunge ya nchi nyingi za kiafrika. Ni ndani ya mabunge yetu tumeacha tuliowaajiri kujipangia na kujipandishia mshahara na marupurupu watakavyo. Kipare tunaita THE AFRO CURSE OF PARLIAMENTARY SYSTEM. Nje ya mabunge ya kiafrika hakuna hizaya hiyo.

Enzi za Nyerere ilikuwa sawa kupandisha mishahara siku ya MEI mosi kwa kuwa chini ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kundi la wafanyakazi lilikuwa sehemu ya wenye Mali. Ndio maana kulikuwa na mabaraza ya wafanyakazi yaliyokuwa na mamlaka hadi ya kupanga mapato na matumizi.

Waliofuatia baada yake walianza kuacha huu utaratibu kidogo kidogo kwa kuwa umiliki Mali ulibadilika. Sekta binafsi ilianza kuchukua nafasi yake. Kwa hiyo ni kutofahamu au ujinga au upumbavu kudhani kila MEI Mosi mshahara utaongezwa. Wafanyakazi sio wenye Mali tena.

Na hata serikali imepunguza umiliki wake na kuichia sekta binafsi chini ya dhana ya PPP (Public Private Partnerships). Kwa Leo sitazungumzia mapungufu ya PPPs. PPPs ni hika ya sekta binafsi ikipigiwa upatu na WORLD BANK NA IMF! Ni mbinu mpya ya kuruhusu sekta binafsi ifadhiliwe kwa hela za umma!

Ukitaka kujua MEI MOSI so siku ya kupandisha mshahara tens nchini Tanzania jaribu kujiuliza: hivi so imeadhimishwa note duniani? Ni nchi IPI Ulaya Leo imeongeza mshahara? Je marekani Leo wameongeza dola ngapi kwenye mshahara?Je Japan wameongeza? Kwa nini udhani Tanzania imekosea kutoongeza leo?

Hebu achaneni na ndoto za alinacha. Dunia imebadilika. Hakuna cha nyongeza mshahara siku ya MEI MOSI labda mkubali kurudia SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA!

TUCTA zile hotuba za kudai nyongeza MEI MOSI achaneni nazo. Sasa zama nyingine. Msiimbe kaswida kilabuni! Msiimbe kwaya sokoni! Hailipi tena siku hizi.

Halafu kichekesho ni watu walewale wanaodai hawana ajira ndio wanaolalamika mshahara kutoongezwa!! Walau kwa sasa tuitumie MEI MOSI kudai ongezeko LA nafasi za ajira (employment creation), hifadhi ya jamii (social protection for all), ajira bora na zenye utu (decent work) na ajira zinazojali mazingira (green jobs).

Ujinga Wa kudai nyongeza MEI MOSI tuachane nao. Tukachape kazi makazini mwetu tuongeze tija halafu tutumie ILO Convention Number 98 kujadiliana na waajiri wetu (collective bargaining) nyongeza ya mshahara na marupurupu. Tuache uvivu, wizi, uzembe na kuingiza siasa sehemu za kazi.

Niwatakie MEI MOSI njema waajiriwa na familia zenu! Msio na ajira jitahidini kusoma, kuongeza skills na kukataa kupoteza muda kwenye shughuli zisizo na maana kama MAANDAMANO, MIKUTANO, VIJIWE, MAOMBI, DUA, TUNGURI, MITANDAONI, VILABUNI, SHISHI, n.k.
 
Aiseeee!!!
Baada ya kujua kuwa Mkuu anapenda PhD,naona umeamua kutafuta fursa avae. PhD za kujitoa akili na kulamba viatu.

Mei mosi ni siku ya wafanyakazi. Kueleza shida,changamoto,mafanikio,maombi,mapendekezo na mustakabali wa wafanyakazi ni dhambi!? Je kuongelea mafanikio ya serikali yasiyohusiana na siku hii ndio halali!? Kuongelea mambo ya chama/vyama siku hii ni sahihi!?
 
Huyu naye anatafuta kick ya Uteuzi au ameeleza Ukweli?
Naona PhD yake ndio ilimpeleka Togo lome kwa sababu Mshahara wa Tz ulikuwa mzuri kuliko wa huko Togo, akaamua kuiacha kazi nzuri yenye maslahi maengi Tz akaaenda kujitolea huko aliko.
Sisi wakazi wa Togo tuna akili nyingi sana kuliko wanaoishi Dar na ndio maaana nawaambia acheni Upumbavu.
Haya sasa kama kua PhD nyingine humu JF ije imjibu Mwl wa Chuo Kikuu
 
PhD zingine zina kwashikor au Stunted na wasting ndani ya siku 1000 za utotoni. Ukizingatia alizaliwa huko milimani,naogopa kama alipata lishe bore
 
Huyu naye anatafuta kick ya Uteuzi au ameeleza Ukweli?
Naona PhD yake ndio ilimpeleka Togo lome kwa sababu Mshahara wa Tz ulikuwa mzuri kuliko wa huko Togo, akaamua kuiacha kazi nzuri yenye maslahi maengi Tz akaaenda kujitolea huko aliko.
Sisi wakazi wa Togo tuna akili nyingi sana kuliko wanaoishi Dar na ndio maaana nawaambia acheni Upumbavu.
Haya sasa kama kua PhD nyingine humu JF ije imjibu Mwl wa Chuo Kikuu
 
Ukimsomaga huko FB utadhani sio msomi, nilipoona jina Yahaya Msangi, my mind told me this, "this guy is not new to you" ndio sasa nimemkumbuka. Anyway, nadhani kwasasa kwa Africa hakuna kazi inalipa kama kazi za siasa; yaani sio udaktari, uinjinia, uwana sharia nk, siasa in Africa ndio mambo yote na ni kazi ambayo hata mjinga anaifanya bila shida yoyote.
 
Mtoa mada,

Samahani kidogo,
UMESAHAU KUAMBATANISHA namba ya simu.
 
Ukimsomaga huko FB utadhani sio msomi, nilipoona jina Yahaya Msangi, my mind told me this, "this guy is not new to you" ndio sasa nimemkumbuka. Anyway, nadhani kwasasa kwa Africa hakuna kazi inalipa kama kazi za siasa; yaani sio udaktari, uinjinia, uwana sharia nk, siasa in Africa ndio mambo yote na ni kazi ambayo hata mjinga anaifanya bila shida yoyote.
Kwanza hiyo PhD yake ni ya nini? Elim duniani au elim akhera? He seems punguani!
 
TUCTA zile hotuba za kudai nyongeza MEI MOSI achaneni nazo. Sasa zama nyingine. Msiimbe kaswida kilabuni! Msiimbe kwaya sokoni! Hailipi tena siku hizi.

Halafu kichekesho ni watu walewale wanaodai hawana ajira ndio wanaolalamika mshahara kutoongezwa!! Walau kwa sasa tuitumie MEI MOSI kudai ongezeko LA nafasi za ajira (employment creation), hifadhi ya jamii (social protection for all), ajira bora na zenye utu (decent work) na ajira zinazojali mazingira (green jobs).
Huu ndio ukweli....TUBADILIKE
 
Ujinga ni vyama vya wafanyakazi kujiweka ndani ya koti la serikali na siku ya Mei mosi mnamualika Rais ambaye ni mwakilishi wa serikali nyonyaji.
 
Na Yahya Msangi
1/05/2018

DHANA POTOFU: NYONGEZA YA MISHAHARA MEI MOSI

Nimepitia kurasa mbalimbali za vijana na wengi wamelalamikia mishahara kutoongezwa na raisi. Siwalaumu sana kwa kuwa ndivyo walivyoaminishwa na hakuna anayewaelimisha.

Wengi wananukuu au kuongozwa na historia; wananukuu "enzi ya Nyerere". Tatizo ni kutochambua mambo kwa kina.

Mshahara popote duniani huongezwa na mwajiri au mwenye hisa. Mfanyakazi kujiongezea mshahara ni hizaya. Ni uhuni. Uhuni uliopo kwenye mabunge ya nchi nyingi za kiafrika. Ni ndani ya mabunge yetu tumeacha tuliowaajiri kujipangia na kujipandishia mshahara na marupurupu watakavyo. Kipare tunaita THE AFRO CURSE OF PARLIAMENTARY SYSTEM. Nje ya mabunge ya kiafrika hakuna hizaya hiyo.
Enzi za Nyerere ilikuwa sawa kupandisha mishahara siku ya MEI mosi kwa kuwa chini ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kundi la wafanyakazi lilikuwa sehemu ya wenye Mali. Ndio maana kulikuwa na mabaraza ya wafanyakazi yaliyokuwa na mamlaka hadi ya kupanga mapato na matumizi.

Waliofuatia baada yake walianza kuacha huu utaratibu kidogo kidogo kwa kuwa umiliki Mali ulibadilika. Sekta binafsi ilianza kuchukua nafasi yake. Kwa hiyo ni kutofahamu au ujinga au upumbavu kudhani kila MEI Mosi mshahara utaongezwa. Wafanyakazi sio wenye Mali tena. Na hats serikali imepunguza umiliki wake na kuichia sekta binafsi chini ya dhana ya PPP (Public Private Partnerships). Kwa Leo sitazungumzia mapungufu ya PPPs. PPPs ni hika ya sekta binafsi ikipigiwa upatu na WORLD BANK NA IMF! Ni mbinu mpya ya kuruhusu sekta binafsi ifadhiliwe kwa hela za umma!
Ukitaka kujua MEI MOSI sio siku ya kupandisha mshahara tena nchini Tanzania jaribu kujiuliza: hivi si imeadhimishwa kote duniani? Ni nchi IPI Ulaya Leo imeongeza mshahara? Je marekani Leo wameongeza dola ngapi kwenye mshahara?Je Japan wameongeza? Kwa nini udhani Tanzania imekosea kutoongeza leo?

Hebu achaneni na ndoto za alinacha. Dunia imebadilika. Hakuna cha nyongeza mshahara siku ya MEI MOSI labda mkubali kurudia SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA!

TUCTA zile hotuba za kudai nyongeza MEI MOSI achaneni nazo. Sasa zama nyingine. Msiimbe kaswida kilabuni! Msiimbe kwaya sokoni! Hailipi tena siku hizi.

Halafu kichekesho ni watu walewale wanaodai hawana ajira ndio wanaolalamika mshahara kutoongezwa!! Walau kwa sasa tuitumie MEI MOSI kudai ongezeko LA nafasi za ajira (employment creation), hifadhi ya jamii (social protection for all), ajira bora na zenye utu (decent work) na ajira zinazojali mazingira (green jobs). Ujinga Wa kudai nyongeza MEI MOSI tuachane nao. Tukachape kazi makazini mwetu tuongeze tija halafu tutumie ILO Convention Number 98 kujadiliana na waajiri wetu (collective bargaining) nyongeza ya mshahara na marupurupu. Tuache uvivu, wizi, uzembe na kuingiza siasa sehemu za kazi.

Niwatakie MEI MOSI njema waajiriwa na familia zenu! Msio na ajira jitahidini kusoma, kuongeza skills na kukataa kupoteza muda kwenye shughuli zisizo na maana kama MAANDAMANO, MIKUTANO, VIJIWE, MAOMBI, DUA, TUNGURI, MITANDAONI, VILABUNI, SHISHI, n.k.
 
Wee kweli ya haya, Collective bargaining ina tofauti gani na kuomba kupandishiwa mshahara kama ilivyofanywa na TUCTA? Unajaribu kutoa mfano wa inchi ambazo hazikuongezewa mshahara lakini zimesherehekea May mosi wakati husemi kuwa wao wanaangalia CPI ya wakati huo ikoje? then wanaongezewa automatically bila kupigishana kelele kama tulivyozoea. Nakubaliana nawe kwa mengi ila hili la kuomba mshahara ni haki ya wafanyakazi kutokana na system yetu ilivyojengeka na kuzoeleka
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom