Dhana nzima ya Futari na Daku

Ebu chukulia wewe Numbisa let's say upo na wapangaji wenzako karibia wote wamefunga je itakuwa Busara ukiwa nao barazani mnabadilishana mawili matatu basi ukawa na msosi wako unakula mbele yao je ni Sawa?
Mbona leo yupo Mkristo katikati ya Waislam wanakula na kufurahia chai zao,kahawa wengine wanakunywa supu lakini hakuna mwenye shida na hilo siyo mfungaji wala waliokuwa hawajafunga?labda kwa sababu hajawaambia kama amefunga?

Haya mambo ni utu tu uzingatiwe,wewe uliyefunga acha asiyefunga afanye yake maana mwisho kila mtu ana hukumu yake tatizo ni pale baadhi ya watu wanapoanza kujiona wao ni muhimu zaidi ya wengine kutaka kuingiza itikadi zao kwenye maisha ya watu wasiofanana nao.
 
Mbona leo yupo Mkristo katikati ya waislam wanakula na kufurahia chai zao,kahawa wengine wanakunywa supu lakini hakuna mwenye shida na hilo siyo mfungaji wala waliokuwa hawajafunga?

Haya mambo ni utu tu uzingatiwe,wewe uliyefunga acha asiyefunga afanye yake maana mwisho kila mtu ana hukumu yake.
Chief

Ni kweli usemayo nami nakubaliana na wewe Kwa asilimia zote kabisa.

Na hata mtu ambaye haja funga akila mbele yako bado sioni tatizo Sana kwasababu mfungaji amefunga kama ibada hivyo kama ni muumini WA kweli na kafunga Kwa dhati Kwa kutarajia malipo hawezi athirika na kumuona mtu anakula mbele yake, ingawa Busara inatakiwa Sana Kwa mtu binafsi kutafakari na kuepuka kumkwaza mwenzake

Hivyo hakuna haja ya kutoleana maneno mabaya
 
Unafunga kwa hiyari yako hakuna haja ya kuzuia wengine kula popote, wawe wa dini yako au dini nyingine.
Swali zuri Sana madam Numbisa

Kama nilivyoeleza awali maana halisi ya Daku,pamoja na mambo mengine ni kumuwezesha mfungaji kuwa na stamina ili apate kuendelea na majukumu yake kama kawaida pasina kuwa na uchovu mwingi

Sasa,

Dhana nzima ya kuwazuia watu Kula chakula hadharani au kuuza vyakula ni Kwa Nia moja Tu kuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani na kuwahimiza watu wafunge au watekeleze ibada ya funga.

Na utaratibu huo hufanywa kwenye maeneo yenye waislamu wengi kama Zanzibar Kwa maana wengi wao ni waumini WA kiislamu hivyo hawana budi kufunga,na si rahisi kukuta huku bara kuna mambo kama hayo.

Lakini hata Kwa utashi WA kawaida Tu Kwa ibada kama ya mwezi wa ramadhani ambayo ni maarufu Sana na waislamu wengi wanafunga je si Busara basi kutokula hovyo hovyo hadharani?

Ebu chukulia wewe Numbisa let's say upo na wapangaji wenzako karibia wote wamefunga je itakuwa Busara ukiwa nao barazani mnabadilishana mawili matatu basi ukawa na msosi wako unakula mbele yao je ni Sawa?
 
Kuna post moja nimeiyona ingawa ilikuwa inazungumzia kwaresma lakini mwandishi wa post hiyo alikuwa na lengo la kukashifu dhana nzima ya Futari na Daku.

Kwake yeye Kwa mujibu wa Imani yao wanakula chakula chochote kile tofauti na watu wa Imani nyingine ambayo pasina kuficha na Imani hii ni Uislamu.

Kwa uelewa wa mwandishi anachoelewa yeye kuhusu Futari cha kwanza kinachomjia kichwani kwake ni uji, viazi au mihogo na tambi, kwake yeye hiyo ndio Futari.

Na Daku ni chakula ambacho kinaliwa usiku sana kama ugali, wali na ndizi na kadhalika, kwahiyo kana kwamba anaona fahari kwamba wao hawana mambo hayo kwahiyo mambo yao yapo super.

Ningependa nimpe elimu juu ya mambo haya ili ukungu umtoke katika ubongo wake na apate kujua usahihi wa dhana ya Futari na Daku ili kesho na kesho kutwa asirudie tena kuongea huo upuuzi.

Futari imetokana na neno kufuturu kwa Kiswahili chepesi ni mlo wa kwanza baada ya kufunga swaumu, kwahiyo kile chakula cha kwanza kukila baada ya kufungua ndio huitwa Futari, na yaweza kuwa tende au maji, ukipata kimoja kati ya hicho hapo tunasema umefuturu, na chakula kingine ni ziada tu kwa maana kinahesabika kama chakula kingine tu.

Tofauti na watu wa Imani nyingine, Futari au kufuturu ni ibada na ina utaratibu wake, miongoni mwa mambo muhimu ya kufanya kwa mwenye kufunga ni kutakiwa kufuturu mapema au haraka mara baada tu ya kuingia Magharibi baada ya jua kuzama.

Hapo hutakiwa kupata tende au maji kwani hivyo ndio vitu ambavyo ni Sunna kutoka kwa Mtume wetu, lakini hata hivyo hakuna aweza kufuturu Kwa biskuti, matunda, karanga au na chochote kile ambacho anaweza kuipata Kwa wakati huo, hapo ndio tunasema kufuturu.

Kwahiyo funga ya muislamu au mwezi wa Ramadhani unaweza kufungwa hata bila ya uwepo wa uji, au viazi, ndizi, magimbi na kadhalika, hivyo ni vyakula tu ambavyo vimezoeleka lakini sio kwamba bila hivyo haipatikani funga, mtu anaweza kufuturu kwa chai na mkate au chapati na hiyo ndo ikawa Futari yake.

Daku ni chakula ambacho huliwa usiku Sana na inashauriwa kuanzia saa nane, tisa mpaka saa kumi usiku, lakini hii nayo ni ibada pia, kwa maana ni bora zaidi kuchelewa kula Daku kama ambavyo ni bora zaidi kuwahi kufuturu, na unapata thawabu kwa kufanya haya.

Daku ni chakula kilicho barikiwa na ndio maana waislamu wanasisitizwa sana mwezi wa Ramadhani wajitahidi Kula Daku, lakini ifahamike kwamba Daku inaweza kuwa glasi moja ya maji au maziwa, au chai na andazi au chapati, ili mradi tu upate chochote kidogo cha kula usiku huo, na hiyo ndio Daku.

Kwa mfano unaweza kula wali wako au ugali saa tano usiku halafu usiku ukaamka kunywa chai tupu au juisi au maziwa ndio ikawa Daku yako, hapo unapata baraka.

Na haya mambo ya kudhani Futari ni viazi, mihogo, ndizi, magimbi na uji au chai huwa tatiza hata baadhi ya waislamu kwa kusema hawana hela ya Futari na hivyo kushindwa kufunga swaumu, huo ni uelewa mbaya sana na ni kukosa maarifa kabisa.

Tupende kujifunza na kupata elimu ili tufanye mambo sahihi kwa wakati sahihi kabisa.

Natumaini wale ambao walikuwa na uelewa mbaya kuhusu Futari na Daku walau kwa uchache watakuwa wamepata maarifa na kutoa ukungu katika vichwa vyao.

Ni hayo tu!

johnthebaptist
Numbisa
Sawa, sisi huku kwa Pengo tunaendelea kama kawa.
 
Unafunga kwa hiyari yako hakuna haja ya kuzuia wengine kula popote, wawe wa dini yako au dini nyingine.

Mkuu unajua huwa tunajifunza kupitia wengine, mfano daktari tunaamini ni mtu ambaye anajua umuhimu wa afya na tunatarajia atakuwa WA kwanza kulinda afya yake,hivyo mtu WA kawaida akimuona daktari huyo huyo anakunywa pombe au kuvuta sigara huenda asione Athari ya vitu kwakuwa anaona kama daktari anatumia basi kumbe ni bla bla Tu

Sasa wakati mwingine tunajitajidi kuelimisha au kuwataka watu wasile hovyo hadharani ili hawa watoto ambao wanakuwa Leo basi wajifunze umuhimu wa ibada hii kwa kutoona wengine wanakula hovyo hadharani hasa katika maeneo ambayo waislamu wapo wengi.

Sijui kama nimetoa mfano sahihi lkn anyways hope imeeleweka
 
DINI ya kuabudu Miungu Mwezi na Jua KUZAMA.

Mungu anasema mumuabudu yeye msiabudu kitu kingine chochote zaidi yake yeye.

Endeleeni kumkufuru
MWEZI WA MUNGU MNASEMA MWEZI WA Lama Hovyo sana nyie.
 
DINI ya kuabudu Miungu Mwezi na Jua KUZAMA.

Mungu anasema mumuabudu yeye msiabudu kitu kingine chochote zaidi yake yeye.

Endeleeni kumkufuru
MWEZI WA MUNGU MNASEMA MWEZI WA Lama Hovyo sana nyie.
Ingawa sijakuelewa unakusudia nini chief

Sijui unaandika huku unatembea au upo kwenye mwendo Kasi?
 
Chief

Ni kweli usemayo nami nakubaliana na wewe Kwa asilimia zote kabisa.
Na hata mtu ambaye haja funga akila mbele yako bado sioni tatizo Sana kwasababu mfungaji amefunga kama ibada hivyo kama ni muumini WA kweli na kafunga Kwa dhati Kwa kutarajia malipo hawezi athirika na kumuona mtu anakula mbele yake, ingawa Busara inatakiwa Sana Kwa mtu binafsi kutafakari na kuepuka kumkwaza mwenzake

Hivyo hakuna haja ya kutoleana maneno mabaya
Huwa inasemwa hivi lakini inapokuja kwenye kuigeuza hii kauli kuwa ukweli unakutana na mtu kuitwa majina ya ajabu na kukera kama Kobe,Kaffir wengine kwenda mbali zaidi na kumnyanyapaa yule anayekula!

By the way,hizi imani zina mafundisho tofauti yenye ladha tofauti naamini hata Mungu wa hizi imani ni tofauti so sitegemei kuwa sawa hata siku moja.
 
Kuhusu wasemaje WA maneno mabaya hawa hawakosekani siku zote maadam tunashare nao hii sayari ya dunia,kwahiyo wakati mwingine ni kuwapuuza Tu.

Kuhusu swala la Mungu kuwa tofauti,Kwa upande wangu naamini tunaye mmoja Tu Ila mapokeo ndio tofauti lkn hii haikufanyi wewe usiamini vinginevyo
 
common sense inanileta kuelewa kuwa daku ni kujiandaa masaa mengi kuhimili njaa! Unakula /inakunywa saa kumi hayo maji/uji ili ikusaidie kufika saa 12 , maana si rahisi/ni mateso kuhimili njaa,, kiu etc kwa saa zaisi ya 12 kesho yake.

Hivi tabu yote ya nini? Unatafuta nini? Bada? Kwani lazima ujitese? Ili iweje? Kuingia mbinguni? Who knows kama kuna Mungu? IMANI, IMANI IMANI
We babu unazeeka vibaya,
Usahasema Imani sasa Imani ya Mtu anaonaje mateso sio kama wewe ndie utesekaye kwa kuumizwa na matendo ya Imani ya mwengine.
 
Mfano.

Wanafunzi waanze kwenda shule saa moja usiku Hadi saa kumi na moja Asubuhi.

Alafu waje watuambie eti wamefunga shule.
Imani ya DINI ya MAKOBAZI ni ya Hovyo sana.

Kila siku tunasema imetengenezwa Roma hamuelewi
Kwa hiyo Roma ndio wanabadilisha Mchana kua Usiku?
 
Daku inaambata na Vigoma siku hizi ukifika mwezi wa Ramadhan vile Vigoma vya Kula Kula Daku Mpemba na kinyago anaecheza Vigoma hakuna tena, sijui nani alieua vile Vigoma vya Daku siku hizi hakuna watu wanawaza kula tu na kula kwenyewe wanakula kiuchoyo zamani ukifika mda wa futari unachagua Baraza la kwenda kula na hufukuzwi na kingine utakuta umeletewa nyumbani ule,

Yaan zamani mwezi wa Ramadhani waislamu walikua wakalimu sana nazungumzia waislamu wote sio wahisani Ila siku hizi sijui njaa imezidi Ramadhan waislamu wanakula wenyewe ule utaratibu wa kula kibarazani umekufa hakuna kukaribisha mtu na hakuna kumpelekea mtu (jirani) chakula,
Ukichoniandika ni kweli.....ila sababu kubwa pia mie ninayoiona ni ugumu wa maisha na umimi.....coz wapo wenye nazo ila pia hawafanyi hivyo!
 
Daku inaambata na Vigoma siku hizi ukifika mwezi wa Ramadhan vile Vigoma vya Kula Kula Daku Mpemba na kinyago anaecheza Vigoma hakuna tena, sijui nani alieua vile Vigoma vya Daku siku hizi hakuna watu wanawaza kula tu na kula kwenyewe wanakula kiuchoyo zamani ukifika mda wa futari unachagua Baraza la kwenda kula na hufukuzwi na kingine utakuta umeletewa nyumbani ule,

Yaan zamani mwezi wa Ramadhani waislamu walikua wakalimu sana nazungumzia waislamu wote sio wahisani Ila siku hizi sijui njaa imezidi Ramadhan waislamu wanakula wenyewe ule utaratibu wa kula kibarazani umekufa hakuna kukaribisha mtu na hakuna kumpelekea mtu (jirani) chakula,
Daah hii comment niilipita mpaka mdau mmoja alipoquote ndio nimeiyona chief

Ni kweli kabisa zamani ilikuwa Raha Sana yaani mida ya usiku lazima wadau WA kuamsha amsha Kula Daku na dufu zao lazima wachangamshe mambo,sijui vimeishia wapi vile.

Na ni kweli kabisa zamani vile vile kuanzia mtaa mmoja mpaka mwingine ni watu mabarazani kufuturu kiasi kwamba huenda mpaka unafikia kwako ushashiba tayar maana kila mtu anakukaribisha na kutaka upate chochote kutoka kwake.

Naweza sema siku hizi Imani zile hakuna tena, zilishaenda na wazee wetu tumebaki Sisi Tia maji Tia maji
 
common sense inanileta kuelewa kuwa daku ni kujiandaa masaa mengi kuhimili njaa! Unakula /inakunywa saa kumi hayo maji/uji ili ikusaidie kufika saa 12 , maana si rahisi/ni mateso kuhimili njaa,, kiu etc kwa saa zaisi ya 12 kesho yake.

Hivi tabu yote ya nini? Unatafuta nini? Bada? Kwani lazima ujitese? Ili iweje? Kuingia mbinguni? Who knows kama kuna Mungu? IMANI, IMANI IMANI
Mwaka 2023 bado mnakataa kufunga? Kuna tafiti nyingi sana za Kisayansi zinaonesha kufunga kuna faida kubwa za Ki Afya

Hii ramani ya Kansa Duniani ikionesha rate ya Cancer
images (18).jpg

Ukiangalia kwa Makini hapo Nchi Za Africa Masikini, Middle East, South Asia na South East Asia kuna low rate ya Cancer compare na Nchi za Ulaya, Marekani, Australia, Japan na Asia ya Mbali kwa Ujumla.

Nchi nyingi za Ghuba ni matajiri wana Consume Sugar kwa wingi na matatizo mengine ya Obesity wanayo kwanini cancer sio nyingi huko? Jibu walilotupa wanasayansi ni kwamba wanafunga.

Kufunga husaidia mambo kama

1. Kufunga kuna Trigger Autophagy
Hii ni process ya ku recycle old damaged protein, unapo recyle hizi protein una recyle pia Mitochndria, hizi Mitochondria zikiwa damaged husababisha cancer.

2.kufunga kunapunguza Inflammation ambayo ikipungua inapunguza Risk ya Chronic deseases kama Cancer

3. Ukifunga unaua Seli na kusababisha kutengenezwa seli mpya zenye nguvu kama killer na Helper T cell, hizi husaidia kupambana na Cancer.

Na sio cancer tu Kufunga kunareset immune system kwa ujumla unapata mwili wenye Afya kuliko mtu asiefunga

Pamoja na Kufunga kukupa Afya kunakusaidia kiimani kuweza kuwafikiria wasio na Chakula ama uwezo, hii hukusaidia kuwa Binadamu bora zaidi.
 
Back
Top Bottom