Dhana nzima ya Futari na Daku

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,522
6,504
Kuna post moja nimeiyona ingawa ilikuwa inazungumzia kwaresma lakini mwandishi wa post hiyo alikuwa na lengo la kukashifu dhana nzima ya Futari na Daku.

Kwake yeye Kwa mujibu wa Imani yao wanakula chakula chochote kile tofauti na watu wa Imani nyingine ambayo pasina kuficha na Imani hii ni Uislamu.

Kwa uelewa wa mwandishi anachoelewa yeye kuhusu Futari cha kwanza kinachomjia kichwani kwake ni uji, viazi au mihogo na tambi, kwake yeye hiyo ndio Futari.

Na Daku ni chakula ambacho kinaliwa usiku sana kama ugali, wali na ndizi na kadhalika, kwahiyo kana kwamba anaona fahari kwamba wao hawana mambo hayo kwahiyo mambo yao yapo super.

Ningependa nimpe elimu juu ya mambo haya ili ukungu umtoke katika ubongo wake na apate kujua usahihi wa dhana ya Futari na Daku ili kesho na kesho kutwa asirudie tena kuongea huo upuuzi.

Futari imetokana na neno kufuturu kwa Kiswahili chepesi ni mlo wa kwanza baada ya kufunga swaumu, kwahiyo kile chakula cha kwanza kukila baada ya kufungua ndio huitwa Futari, na yaweza kuwa tende au maji, ukipata kimoja kati ya hicho hapo tunasema umefuturu, na chakula kingine ni ziada tu kwa maana kinahesabika kama chakula kingine tu.

Tofauti na watu wa Imani nyingine, Futari au kufuturu ni ibada na ina utaratibu wake, miongoni mwa mambo muhimu ya kufanya kwa mwenye kufunga ni kutakiwa kufuturu mapema au haraka mara baada tu ya kuingia Magharibi baada ya jua kuzama.

Hapo hutakiwa kupata tende au maji kwani hivyo ndio vitu ambavyo ni Sunna kutoka kwa Mtume wetu, lakini hata hivyo hakuna aweza kufuturu Kwa biskuti, matunda, karanga au na chochote kile ambacho anaweza kuipata Kwa wakati huo, hapo ndio tunasema kufuturu.

Kwahiyo funga ya muislamu au mwezi wa Ramadhani unaweza kufungwa hata bila ya uwepo wa uji, au viazi, ndizi, magimbi na kadhalika, hivyo ni vyakula tu ambavyo vimezoeleka lakini sio kwamba bila hivyo haipatikani funga, mtu anaweza kufuturu kwa chai na mkate au chapati na hiyo ndo ikawa Futari yake.

Daku ni chakula ambacho huliwa usiku Sana na inashauriwa kuanzia saa nane, tisa mpaka saa kumi usiku, lakini hii nayo ni ibada pia, kwa maana ni bora zaidi kuchelewa kula Daku kama ambavyo ni bora zaidi kuwahi kufuturu, na unapata thawabu kwa kufanya haya.

Daku ni chakula kilicho barikiwa na ndio maana waislamu wanasisitizwa sana mwezi wa Ramadhani wajitahidi Kula Daku, lakini ifahamike kwamba Daku inaweza kuwa glasi moja ya maji au maziwa, au chai na andazi au chapati, ili mradi tu upate chochote kidogo cha kula usiku huo, na hiyo ndio Daku.

Kwa mfano unaweza kula wali wako au ugali saa tano usiku halafu usiku ukaamka kunywa chai tupu au juisi au maziwa ndio ikawa Daku yako, hapo unapata baraka.

Na haya mambo ya kudhani Futari ni viazi, mihogo, ndizi, magimbi na uji au chai huwa tatiza hata baadhi ya waislamu kwa kusema hawana hela ya Futari na hivyo kushindwa kufunga swaumu, huo ni uelewa mbaya sana na ni kukosa maarifa kabisa.

Tupende kujifunza na kupata elimu ili tufanye mambo sahihi kwa wakati sahihi kabisa.

Natumaini wale ambao walikuwa na uelewa mbaya kuhusu Futari na Daku walau kwa uchache watakuwa wamepata maarifa na kutoa ukungu katika vichwa vyao.

Ni hayo tu!

johnthebaptist
Numbisa
 
Daku inaambata na Vigoma siku hizi ukifika mwezi wa Ramadhan vile Vigoma vya Kula Kula Daku Mpemba na kinyago anaecheza Vigoma hakuna tena, sijui nani alieua vile Vigoma vya Daku siku hizi hakuna watu wanawaza kula tu na kula kwenyewe wanakula kiuchoyo zamani ukifika mda wa futari unachagua Baraza la kwenda kula na hufukuzwi na kingine utakuta umeletewa nyumbani ule,

Yaan zamani mwezi wa Ramadhani waislamu walikua wakalimu sana nazungumzia waislamu wote sio wahisani Ila siku hizi sijui njaa imezidi Ramadhan waislamu wanakula wenyewe ule utaratibu wa kula kibarazani umekufa hakuna kukaribisha mtu na hakuna kumpelekea mtu (jirani) chakula,
 
Daku ni chakula kilicho barikiwa na ndio maana waislamu wanasisitizwa sana mwezi wa Ramadhani wajitahidi Kula Daku, lakini ifahamike kwamba Daku inaweza kuwa glasi moja ya maji au maziwa, au chai na andazi au chapati, ili mradi tu upate chochote kidogo cha kula usiku huo, na hiyo ndio Daku.

Kwa mfano unaweza kula wali wako au ugali saa tano usiku halafu usiku ukaamka kunywa chai tupu au juisi au maziwa ndio ikawa Daku yako, hapo unapata baraka.
common sense inanileta kuelewa kuwa daku ni kujiandaa masaa mengi kuhimili njaa! Unakula /inakunywa saa kumi hayo maji/uji ili ikusaidie kufika saa 12 , maana si rahisi/ni mateso kuhimili njaa,, kiu etc kwa saa zaisi ya 12 kesho yake.

Hivi tabu yote ya nini? Unatafuta nini? Bada? Kwani lazima ujitese? Ili iweje? Kuingia mbinguni? Who knows kama kuna Mungu? IMANI, IMANI IMANI
 
... usiku sana; ufafanuzi tafadhali. Niko Sweden hapa.
Naam chief

Inapo semwa usiku Sana inamaanisha kwenye mida ya saa nane au saa Tisa au saa Kumi, hiyo ndio mida mizuri ya Kula Daku.

Kama unaweza kula chakula kizito mida hiyo ni vizuri ili ikupe nguvu/ stamina ya kufunga vizur mchana, lakini kama huwezi Kula chakula kizito basi waeza kupata kitu chepesi na ukakusudia au kunuia kuwa ndio Daku kwako,mfano kahawa/chai,maziwa au tende na kadhalika na hapo utakuwa umepata fadhila za Kula daku
 
common sense inanileta kuelewa kuwa daku ni kujiandaa masaa mengi kuhimili njaa! Unakula /inakunywa saa kumi hayo maji/uji ili ikusaidie kufika saa 12 , maana si rahisi/ni mateso kuhimili njaa,, kiu etc kwa saa zaisi ya 12 kesho yake.

Hivi tabu yote ya nini? Unatafuta nini? Bada? Kwani lazima ujitese? Ili iweje? Kuingia mbinguni? Who knows kama kuna Mungu? IMANI, IMANI IMANI
Chief

Upo sahihi moja wapo ya hekima ya Daku ni kumuwezesha mfungaji siku inayofuata awe na stamina itayo muwezesha kuwa na nguvu na asinyong'onyee Sana,kwasababu funga si adhabu Bali ni ibada.

Lakini kuna ambao hawawezi Kula chakula kizito usiku, wao Sana Sana watakula saq tano au saa sita usiku mfano mmoja wapo ni Mimi binafsi, lakini pamoja na hayo kwakuwa Daku ni chakula chenye baraka na kusisitizwa kukila basi watu kama Sisi tutaamka na Kula kitu chepesi Kwa kukusudia au kunuia kuwa ndio Daku yetu.

Na kila kitu kina mazoea yake,wengine tunakula chakula kizito mapema around saa tano au sita na bado siku ya pili tuko vizuri Tu.

Unaposema tunajitesa unakosea chifu,au nitakuelewa kwasababu huenda hujawahi kufunga hivyo unaona Jambo gumu Sana au la ajabu Sana.

Hiyo kwetu ni ibada na tunaitekeleza Kwa roho Safi kabisa,kwani tunajua ni amri ya Allah na hatuna budi kuwa viumbe watiifu Kwa Muumba wetu na kubwa zaidi tunatarajia malipo makubwa kutoka kwake.

Mungu yupo chief na Hilo usiwe na Shaka nalo hata kidogo,siku ya kufumba macho yako basi utaujua ukweli wote.
 
Mkuu kule nilimuambia mdau aniletee ushahidi wa umiliki wa neno daku na futari kwa dini aliyokua anaishabikia. Maana povu lilimtoka kuwa kachokozwa.

Sasa kama mnakula daku mida hio ya usiku inamaanisha asubuh na mchana hamtakuwa na njaa iweje baadhi ya maeneo mnapiga marufuku watu kula na kufanya biashara ya chakula kuwa mtatamanishwa wakati mnakua mmeshiba?

Inakuaje mnamcharaza mtu viboko huku mkimuita kobe wakati ni maamuzi yake kula,kwann funga iwe lazima?
 
Swali zuri Sana madam Numbisa

Kama nilivyoeleza awali maana halisi ya Daku,pamoja na mambo mengine ni kumuwezesha mfungaji kuwa na stamina ili apate kuendelea na majukumu yake kama kawaida pasina kuwa na uchovu mwingi

Sasa,

Dhana nzima ya kuwazuia watu Kula chakula hadharani au kuuza vyakula ni Kwa Nia moja Tu kuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani na kuwahimiza watu wafunge au watekeleze ibada ya funga.

Na utaratibu huo hufanywa kwenye maeneo yenye waislamu wengi kama Zanzibar Kwa maana wengi wao ni waumini WA kiislamu hivyo hawana budi kufunga,na si rahisi kukuta huku bara kuna mambo kama hayo.

Lakini hata Kwa utashi WA kawaida Tu Kwa ibada kama ya mwezi wa ramadhani ambayo ni maarufu Sana na waislamu wengi wanafunga je si Busara basi kutokula hovyo hovyo hadharani?

Ebu chukulia wewe Numbisa let's say upo na wapangaji wenzako karibia wote wamefunga je itakuwa Busara ukiwa nao barazani mnabadilishana mawili matatu basi ukawa na msosi wako unakula mbele yao je ni Sawa?
 
Awesome hujajibu kwa mapovu kwa busara ulizonazo mkuu upo vizuri.

Ila swali ungeuliza hivi,numbi umekaa na wenzio kibarazani wana kula ugali ndondo wewe unakuja na chips kuku kula hapo walipo wenzio,ni busara hio. Sema ule ukweli sio busara. Busara ni kwenda kula ndani,jirani akija kunusa harufu ya kiepe kuku hicho ni kiranga chake

Conclusion yangu ni kwamba kila mmoja afate anachoamini katika funga yake. Maana kwaresma imewaibua watu na kuleta dhihaka mara tunakula nusu,mara hatuna mfungo.

Nami nasubiri kutolewa tongotongo
 
Asante Sana madam

Nimekuelewa vizuri Sana na ni kweli kuna uelewa mbaya juu ya funga ya kwaresma kuwa mnafunga nusu au unakula kidogo na kuacha hiki na Kula kile hata Mimi binafsi niliyasikia Sana na kuyaamini kipindi Fulani lkn baadae nilikuja kujua ukweli.

Kwahiyo endeleeni kuelimisha watakuja kuelewa Tu.

Nimekupenda bure madam

Shukrani.
 
Back
Top Bottom