Dhambi ya Usaliti

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
4,108
2,000
Habari wakuu bila shaka mko salama.

Leo nataka kushare nanyi hii stori fupi naamini itawafunza pia.Nitangulize samahan mimi si mwandishi mzuri.

Mwenzenu nina mpenzi wangu ambaye zimebaki hatua chache awe mke wangu wa ndoa lakini dhambi ya usaliti inanitesa.Ngoja nianze hapo chini stori yenyewe.

Mwaka 2012 wakati nipo kidato cha nne wakati huo Facebook ndo imeshika moto nilikutana na mpenzi wangu huyu kwenye huo mtandao.Tulianza as marafiki wa kawaida stori hapa na pale mwishowe tulibadilishana namba za simu na tukaanza kuchati na kupigia simu baada ya miezi 2 tukajikuta tumekuwa wapenzi.

Hakika penzi lilikua moto moto tulipendana sana,siku moja alikuja gheto nikaomba mchezo alininyima aliniambia yeye hakuwahi kufanya mapenzi ni kweli alikua bikra nilithibitisha ni bikra.

Baada ya muda matokeo yalitoka mimi nilipata div 2 na yeye alipata 4 ya point 28 alihuzunika sana nikamwambia atulie akanielewa baada ya muda mimi nikapangiwa kuendelea na kidato cha 5 na yeye akaamua kwenda zake chuo Tanga kusoma fani ya uhasibu level ya diploma,hapo ndipo tulipotengana baada ya muda mawasiliano yakawa ya kusuasua mpaka akamaliza mwaka wa kwanza.

Kumbe huko alipata mwanaume mwingine wakawa na uhusiano ulioshiba japo alimwambia mapema kuwa ana mtu wake ambaye ndo mimi,kwahiyo nilipokuwa napiga simu alipokea ila walikua wote na huyo jamaa.Baada ya miaka mitatu kupita 2015 alimaliza masomo yake nami 2016 nilianza chuo X mwaka wa kwanza uhusiano ukarudi upya kama zamani maana alirudi Dar.

2017 Tulihangaika kutafuta kazi sehemu mbalimbali bila mafanikio na hatimae Mungu akajaalia mwezi wa 5 akapata kazi katika mkoa X kama muhasibu wa Mizani lakini alipoipata hiyo kazi hakuniambia kuwa ameipata.Nilipokuwa nampigia simu tuonane nilipata wakati mgumu kutoka kwake mpaka ilipotimia miezi 3 baada ya kupata kazi ndo alinieleza kuwa amepata kazi nilijisikia vibaya kwa sababu hakunitaarifu lakini nikapiga moyo konde.

Nilipokuwa likizo aliniomba nikapajue kwake nikakubali nikasafiri nikaenda hiyo ilikua mwaka 2017 mwezi wa 9 hii safari ndo ilifumbua fumbo lote la maisha ya huyu mpenzi wangu.Baada ya kufika nikaomba tena kupewa tunda kumbuka nilimuacha bikra na sikuwahi kupewa mzigo hapo binti akaanza kulia akaniomba radhi kuwa wakati yupo chuo alirubuniwa akacheat Dah Moyo wangu uliniuma sana hiyo siku maana nilimvumilia kwa miaka 5 lakini akapewa mtu mwingine mwisho wa siku nikasamahe maisha yakaendelea.

Baada ya wiki nikagundua vitu vibaya sana kwake mengine siwezi kusema hapa kwanza alikua na uhusiano na wanaume 5 mbali na mimi 1 ni mfanyakazi mwenzie moyo uliniuma mno safari niliona chungu nikajisikia vibaya kumbuka katika kipindi chote mimi sikuwahi kusaliti kutoka na maisha na changamoto flani nilizopitia kwa mara ya kwanza nikaona ubaya wa usaliti.

Aliniomba msamaha alilia sana nikamsamehe lakini tangu siku hiyo sikumwamini tena kwenye maisha yangu na nilipochunguza nikajua kuwa rafiki zake ndio wanaomshauri vibaya.nikajitahidi kumrekebisha kwa kuwa nampenda kweli alibadilika mno nikaanza kufurahia mapenzi tena.

Baada ya muda likizo iliisha nikarudi Dar kuendelea na masomo ilipokaribia siku yake ya kuzaliwa nikaenda tena nikamfanyia sherehe fupi tukiwa wawili nilimtoa out,siku moja wakati nimekaa nikachukua simu yake nikakuta picha aliyopiga na mwanaume mwingine kwenye kitanda chetu dah moyo uliniuma sana hiyo ilikua mwaka 2018 mwezi wa 3. Nikaongea nae nikasamehe sijui kwanini ilikua rahisi kumsamehe lakini nikagundua nampenda maana home walikua wanmjua na kwao najulikana pia n mama yake alikua ananipenda sana.

Baada ya hapo nisiwe muongo sijawahi kumfumania tena alibadilika total nilipewa mapenzi ambayo sikuwahi kupata popote tangu nizaliwe na namshukuru kwa hilo kwani amekuwa mtu mzuri amenisaidia kwa mengi sana.Balaa likawa kwangu mimi nikaanza kubadilika nikatafuta wanawake wengine wawili kwa siri bila yeye kujua mwaka jana mwezi wa 11 akagundua ikawa penzi limeingia doa alilia sana nikaomba radhi yakaisha nikaachana na wake watu.

Mwaka huu nikarudia tena tabia yangu nikawa na wanawake 4 kwa wakati mmoja mapenzi moto moto alikua ananilalamikia sana kuwa nimechange nikawa namkatalia lakini ikawa ngumu kuamini ilipofika mwezi huu wa 3 nikaenda tena kwenye Birthday yake hapo siku moja wakati nipo naoga akapekua simu yangu akagundua nina wanawake wengine tena sms mbaya mbaya Alilia sana ,hiyo ilikua siku mbaya kwake na kwangu hata mimi niliumia sana maana nilipewa kila kitu na mpenzi wangu alibadilika sana alikua mtu mwema kwangu,kwa marafiki zangu na hata kwa wazazi lakini penzi liliingia doa tena.

Mpaka naandika huu ujumbe Moyo wangu unauma najisikia vibaya sana kweli na yeye aliwahi kunikosea lakini ilikua nyuma sikuwa na sababu ya kumkosea na yeye maana ananipa kila kitu moyo unaniuma mno mpaka sasa nipo kwenye Dailema hatuongei na wala hana hata hamu ya kupoea simu zangu nimetumia njia nyingi kuomba radhi na sihitaji familia ifahamu hii ni aibu kwangu lakini imeshindikana,,,!

Dhambi ya usaliti inanitesa siwezi tena kufanya kazi zangu sina amani tena na hata akinisamehe je,ataniamini au itakuwa na yeye atalipiza kwa hiki kitendo kilichotokea.

Naomba mwenye ushauri mzuri ambao unaweza kunisaidia anaambie hapa maana nafungua chuo soon kumaliza masomo yangu naogopa isije ikanifelisha...

Samahani kwa niliowakwaza kwa hii stori pia sihitaji matusi kama unaona haikuhusu unaweza ukaka kimya tu.

Asanteni
Sent using Jamii Forums mobile app
 

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,900
2,000
Hukusaliti
Yeye ndo alisaliti
Mwanaume hasaliti
Ni haya makanisa ya siku hizi ndo yanapindisha ukweli wa idadi ya wanawake tunaopaswa kuwa nao wanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
 

The man1

JF-Expert Member
Oct 15, 2018
414
500
Sasa hapo unahtaji ushauri upi kama mara yakwanza wewe ndio ulikua mshauri mkuu kwa mpenzi wako.
Jitathimini upya, chukua hatua
 

Khan

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,162
2,000
Hukusaliti
Yeye ndo alisaliti
Mwanaume hasaliti
Ni haya makanisa ya siku hizi ndo yanapindisha ukweli wa idadi ya wanawake tunaopaswa kuwa nao wanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, unakunywa Soda gani? Ukweli ni kwamba bwana mdogo anampenda huyo binti, kinachomuumiza wala si usaliti bali ni kitendo cha binti kutorenspond kwa upendo wake, vivyo hivyo huyo binti alibikiriwa na mwamba ambae huenda alimtia vizuri.. basi ni easy sana kumdump mdogo wetu huyu!.. Anyways kijana sikushauri uendelee na huyo binti.. mmekwishachafua daftari lenu na wanawake huwa hawasahau.. Tafuta mwanamke mwingine!
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
4,108
2,000
Mkuu, unakunywa Soda gani? Ukweli ni kwamba bwana mdogo anampenda huyo binti, kinachomuumiza wala si usaliti bali ni kitendo cha binti kutorenspond kwa upendo wake, vivyo hivyo huyo binti alibikiriwa na mwamba ambae huenda alimtia vizuri.. basi ni easy sana kumdump mdogo wetu huyu!.. Anyways kijana sikushauri uendelee na huyo binti.. mmekwishachafua daftari lenu na wanawake huwa hawasahau.. Tafuta mwanamke mwingine!
Iko ndo kmnachoniuma najua hata akinisamehe bado atakua na kinyongo maana mimi yalipotokea yanayomuhusu sikufanya hivi nilikua na hasira za muda mfupi tu anyway ngoja nipige moyo konde

Sent using Jamii Forums mobile app
 

shalet

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,345
2,000
Mahusiano yenu hayawezi nishakuwa kwenye hali hiyo mtakuwa kwenye cycle ya kusalitiana mpaka mmoja ajiondoe kwenye huo uhusiano na kila mmoja ana sababu ya kumsaliti meenzie

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom