Dhambi ya asili kujadiliwa WAPO Redio

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Siku za hivi karibuni nimeweka thread iliyokuwa inataka kujua dhambi ya asili iliyotendwa na Adamu na Eva, (Uzinifu au ni tunda kweli?)

Siku ya Alhamis 14/1/2010 saa 4 asubuhi, WAPO Redio iliyoko dar, itaendesha mjadala huu, na kutakuwa na mgeni studioni atakayefafanua kuwa hawakula tunda ila walifanya uzinifu, bila shaka atakuwa na ushahidi

Wote tunatakiwa kufuatilia mjadala huu na kupiga simu kuuliza maswali.
 
I doubt kama atakuwa na anything new! Mambo haya ni mapokeo na imani zaidi ya ushahidi. Sanasana ataishia kutoa interpretation tofauti ya vifungu vilevile ya vitabu tunavyovijua. I will stay tuned anyway!
 
Hata kama ni mapokeo, lazima kuwe na ushahidi wa mazingira, na ndio chanzo kikuu cha kuamini, vinginevyo hata kuamini kama MUNGU yupo tusingeamini, lakini tukiangalia mambo ya asili tunashindwa kujua yalianzaje, ndipo tunaamini kuwa yupo mungu, hivyo na huyu jamaa ushahidi wakimazingira atakaokuwa nao ndio tutautumia kuamini kuwa walifanya uzinifu na sio tunda
 
Cha muhimu ni uasi (kukiuka 'maagizo' halali ya Mungu) wa Adam na Hawa. Kujua kama 'tunda' walilokula Adam na Hawa ni 'zinaa' ama la, sidhani kama linaweza kubadilisha chochote katika imani yako. Unless kama atasema kwa kufanya zinaa hiyo, hikuwa uasi mbele ya Mungu!
 
Ni vyema kufahamu ni tunda gani ili tusije kulila pasipo kujua, na kama ni jambo jingine pia tujue, hata hivyo huyu jamaa atatusaidia ktk hili,
 
Radio wapo ni radio nzuri kwani inaweka mijadala wazi kabisa na wenye hoja katika mada husika kuzimwaga kinaga ubaga. Na wachangiaji hutuma michango yao kwa njia ya simu. Natamani kama ningekuwa bongo nami ningefuatilia kipindi. Sijui itakavyokuwa ila kwa uelewa wangu kuhusu dhambi ya asili ina mahusiano na kukutana kimwili. Sasa kosa sii Adamu kumjua hawa la hasha, kwani Mungu alipowaumba aliwataka wazae na kuijaza nchi hivyo uzao ungekuja je ila kwa kukutana? Kosa pale ni Hawa kuwahiwa na serpent mnyama kwa ushawishi wa shetani kabla ya Adamu. Adamu yeye alipaswa asimkaribie tena hawa baada ya kugundua kwamba serpent keshafungua utape. Sawa sawa na sheria ya Mungu ambayo ni Neno lake kwamba mke ni kwa mme mmoja tu na kila kiumbe kitazaana kwa jinsi yake. Adamu alimchukua hawa kama mkewe hata hivyo na kusababisha sasa mchanganyo wa damu na tabia za kinyama katika kizazi cha Adamu na hiyo ndio asili ya dhambi tuliyonayo watu. daudi katika zaburi ya 51 akiungama uovu wake anasema 'nimechukuliwa mimba hatiani na nimekuja duniani ni muovu' na ktk Ayubu 14 anasema 'kila aliyezaliwa na mwanamke siku zake sii nyingi nazo zimejaa taabu na atairudia ardhi(kufa). Lakini hakuna kifungu hata kimoja kinachoweza kuthibitisha kwamba aliyezaliwa na Mungu hufa. Kitabu cha mwanzo kina facts nyingi kuhusu mwanzo wa mtu, mwanzo wa shetani ndani ya uzao wa Adam tulitoka wapi na tunaenda wapi. Kitabu cha ufunuo kina facts za shetani yupo wapi kwa kila zama na jinsi ya kuangamizwa kwake. Baada ya kosa ktk bustani ya Edeni tunaona Mungu akiwapa hukumu ya kosa la kutotii na kwa sababu Mungu ameazimia kumkomboa huyu mtu alieanguka kutoka kwenye neno lake aliweka uadui kati ya uzao wa nyoka, na mzao wa mwanamke. Swali linakuja uzao wa nyoka ni upi na mzao wa mwanamke ni upi. Jibu lipo kwamba uzao wa nyoka ni kaini na mzao wa mwanamke ni Yesu kwa mfuatano wa Mungu-Adamu-seth-mpakaAbrahamu-kupitia Daudi-hadi kwa bikira maria-YESU. Kuna namna fulani ya kujichanganya watu kusema uzao wa nyoka ni kiroho basi kama ni wa kiroho basi itapaswa iwe kwamba Yesu nae ni wa kiroho na kwamba hakuwa mtu wa nyama na damu. Sasa ukiri wa namna hiyo utasababisha mtu kuwa mpinga kristo. Uzao wa nyoka kimwili ulikomeshwa baada ya safina ya Nuhu. Nuhu alikuwa ni kutoka kwa uzao wa Adamu kwa Seth na ndie aliyepata kibali machoni pa Bwana. Na hata kama kuna shaka la wake za watoto wa Nuhu ni kwamba kwa asili mtoto ni mbugu ya uhai ya mwanamume na mwanamke ana yai linaloirutubisha.
 
Back
Top Bottom