Dhambi isiyokuwa na msamaha( unforgiven sin)

Sio kweli kukufuru ni kunena maneno kinyume chake na kutoa kashfa
Sasa hayo Maneno kinyume chake ni Yapi...?
kumbuka Yohana 3:18(Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu)inasema nini?
na mm nimesema nini? suala la kutokuamini sio Suala Dogo kama unavyo fikiria nitajia hayo maneno yaliyo kunyume na Roho mtakatifu
 
Nimekuelewa sana ila naomba tofauti ya kukufuru Mungu
Kukufuru roho mtakf
Na kumkufuru Yesu Kristo
Je aliemkufuru Mungu na Yesu hukumu yao ni ipi

Mkuu Heri lee.

Kukufuru Mungu ni kumkataa au kumkanusha Mungu.

Kukufuru roho mtakatifu ni kukataa au kukanusha uwezo (kudra) ya Mungu kwa sababu roho mtakatifu ni nguvu za utendaji kazi za Mungu.

Kukufuru Yesu kristo ni kumkataa au kumkana Yesu kristo.

Juu ya hukumu gani mtu atapata kwa kufanya kufuru dhidi Mungu na Yesu kristo., mimi sifahamu ila ukumbuke kuwa Yesu kristo alitumwa kuwakomboa wana wa Israeli tu.
 
Roho mtakatfu kama yuko ndani ya Yesu mbona dhmb yake inasameheka

Usichanganye kati ya Yesu kama binadamu na Yesu kama mja wa Mungu, unapozungumzia juu Yesu mja wa Mungu hapo unazungumzia juu ya roho mtakatifu aliyemo ndani yake na wakati huo huyo Yesu alikuwa anatoa (anahubiri) injili kwa wana wa Israeli na hapa ukimkufuru utakuwa umemkufuru Mungu.

Kipindi kingine Yesu aliishi katika jamii na nduguze na famili yake kama mtu wa kawaida akila,kunywa,kulala,kucheka nk,katika mazingira kama haya ukimkosea /kumkufuru hapo yeye mwenyewe anaweza kukusamehe kwa sababu ni suala binafsi.

Juu ya yote Yesu alitumwa kuwaokoa wana wa Israel tu.
 
Poleni ndugu wananchi Tanzania kwa msiba

On point
Sisi wanadamu tunapitiwa kweli kutenda maovu lakini Mungu hutuhurumia
Kwa upande wa ukristo Yesu aliwai kusema waweza kumkufuru Yeye lakini sio roho mtakatifu hutasamehewa hata mungu lakini sio roho mtakatifu husamehewi kamwe ulimwengu huu na ule ujao hivi nini maana ya kukufuru roho mtakatifu wajuzi naomba utatuzi....

#mfikwa
#mshana jr
#zitto jr
Mkuu kwanza naomba ufahamu kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu.

Na pale tunapokua tumetenda dhambi ina maana tunakua tunamchukiza Roho Mtakatifu na tunakua kama tunamfukuza.
Na ndio maana mwenyezi Mungu akatuwekea toba/kutubu yaani kuweza kurudiaha uhusiano wetu na Mungu.
Na anayetukumbusha kufanya toba ni Roho mtakatifu.

Sasa mtu anapokua anashindwa kuitii ile sauti inayomhimiza kwenda kutubu (yaani sauti ya Roho Mtakatifu) dhambi zake, ndio kufuru inapoanzia. Na ikitokea mtu huyu akaendelea kushupaa pasi kuisikiliza sauti hii inayomhimiza kwenda kutubu na hatimaye akawa haoni kuwa ana dhambi na mwisho akafa pasipo kuzitubu dhambi zake, basi huyu anahesabika kama mmojawapo wa watu waliomkufuru Roho Mtakatifu.
 
Sasa hayo Maneno kinyume chake ni Yapi...?
kumbuka Yohana 3:18(Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu)inasema nini?
na mm nimesema nini? suala la kutokuamini sio Suala Dogo kama unavyo fikiria nitajia hayo maneno yaliyo kunyume na Roho mtakatifu
NI YALE YA KUMKASHIFU NA KWA KUTOA MANENO MACHAFU NA YENYE MAASI MBELE ZA WATU
 
Mkuu kwanza naomba ufahamu kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu.

Na pale tunapokua tumetenda dhambi ina maana tunakua tunamchukiza Roho Mtakatifu na tunakua kama tunamfukuza.
Na ndio maana mwenyezi Mungu akatuwekea toba/kutubu yaani kuweza kurudiaha uhusiano wetu na Mungu.
Na anayetukumbusha kufanya toba ni Roho mtakatifu.

Sasa mtu anapokua anashindwa kuitii ile sauti inayomhimiza kwenda kutubu (yaani sauti ya Roho Mtakatifu) dhambi zake, ndio kufuru inapoanzia. Na ikitokea mtu huyu akaendelea kushupaa pasi kuisikiliza sauti hii inayomhimiza kwenda kutubu na hatimaye akawa haoni kuwa ana dhambi na mwisho akafa pasipo kuzitubu dhambi zake, basi huyu anahesabika kama mmojawapo wa watu waliomkufuru Roho Mtakatifu.
HII MADA INA MAPANA YAKE TENA MAKUBWA BASI KAMA NDIO HIVYO HAKUNA ATAKAYE SALIMIKA KWA MUJIBU WA MAANDIKO YAKO
 
Ukiisoma Mathayo 12:22-33 ndio utaona mtiririko vizuri wa swali la mleta uzi. Na mstari wa 33 ndio hasa unaitaja hiyo dhambi. Hapo kuna kisa cha Yesu kumponya mtu ambaye alikuwa kipofu na bubu sababu ya kupagawa na pepo. Umati ukastaajabu kweli na kujiuliza kama ndiye Mwana wa Daudi lkn Mafarisayo (waalimu wa dini) wakasema kamponya kwa uwezo wa Beelzebuli, yaani pepo mkuu! Kauli na dhana hiyo ya Mafarisayo ndio ilipelekea Yesu kusema hiyo dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Hapo hiyo dhambi ni matendo ya Roho wa MUNGU kuitwa au kufananishwa na matendo ya kipepo au shetani. Na hii pia ndio ilimfanya shetani kutimuliwa mbinguni na msamaha kutokupewa kamwe maana alijifananisha na MUNGU. Nakushukuru mno mleta mada. Tunaendelea kujifunza.
 
Hili swali limenisumbua tangu nikiwa sunday school. Mpaka sasa sijapata majibu
 
Mmmh, sio kweli Biblia inasema wazi kwamba ni Roho Mtakatifu ikimaanisha Roho ya Mungu mwenyeww, wewe unasema roho takatifu ni roho za binadamu wapi na wapi? Biblia inaposema Roho Mtakatifu haizungumzii roho ya binadamu, kwa hyo dhambi ya kumkufuru Mungu haitasamehewa labda turudi kwenye neno la kiswahili maana ya kukufuru au kiingereza blasphemy, lakini ukweli utabaki pale pale Roho Mtakatifu ni Mungu mwenyewe

Yan Mungu nae ana roho kama sisi,kwamba nayy atakufa?
Kuna haja yakusoma biblia zenu mkaelewa maana halisi tena ikiwezekana na kama unaweza ukasoke kwa lugha aliyotukia yesu ili uelewe full content.
Sasa kwa mfano (supposedly) Mungu ana roho kwa iyo unavyosema kwa jina la baba,mwana na roho mtakatifu,

literally unamanisha unamuwakilisha Mungu kwa kusema kua ni roho mtakatifu alaf nayy unamtaja.
Someni sana wakristo kuna errors nying sana kwenye biblia ambapo unakuta one scripture inapingana na nyingine.
Itoshe kusema mnapaswa kusoma sana ili muelewe usije ukaenda kwa Mungu huku huna uhakika dini yako kama ni sasa,nanjia rahis niku cross chek au ku verify kilichoandikwa kwenye biblia
 
Jifunze hapa ndugu .......

1 Wakorintho 2 ►

1Ndugu, mimi nilipokuja kwenu sikuwahubiria siri ya ujumbe wa Mungu kwa ufasaha wa lugha, au kwa hekima ya binadamu. 2Nilipokuwa kwenu niliamua kutojua chochote kile isipokuwa tu kumjua Yesu Kristo; naam, Kristo aliyesulubiwa. 3Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi. 4Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho. 5Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu.

6Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.7Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu. 8Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangalielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.

9Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao."

10Hayo ndiyo mambo Mungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. Maana Roho huchunguza kila kitu hata mambo ya ndani kabisa ya Mungu.11Nani awezaye kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.12Sasa sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu, bali tumepokea Roho atokaye kwa Mungu ili atuwezeshe kujua yale tuliyojaliwa na Mungu. 13Basi sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho.

14Mtu wa kidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtu huyo mambo hayo ni upumbavu mtupu; yanapita akili yake; maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaada wa Roho.15Lakini mtu aliye na huyo Roho anaweza kubainisha ubora wa kila kitu, naye mwenyewe hahukumiwi na mtu mwingine. 16Maandiko yasema: "Nani awezaye kuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?" Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.
 
Kwanza Hakuna roho mtakatifu Kuna roho takatifu
Nikirud kwenye swali lako.unapaswa ufaham kwanza Kama roho hio takatifu ndio inaoleta uzima.sasa kwa kuwa watu wengi hukutwa na kifo kwa SABABU tu ya makosa yao yaani dhambi zao.maana mshahara wa dhambi Ni mauti.hakuna ushahidi kuwa wale wakamilifu wasio tenda dhambi huwa wanakufa roho.wenyewe waga wanachukuliwa roho zao hizo TAKATIFU na kupelekwa SEHEMU NYINGINE.kwa hiyo roho za watenda dhambi huwa zinachoshwa na uovu kiasi kwamba matokeo yake huwa kifo ..yaani Ni Kama ile SAA unayotoa bao unaona jinsi usivyoweza kurudisha wazungu ndani ikitoka imetoka kuwazuia Ni haiwezekan ndo maana halisi ya kuiua roho yaani umeitesa roho kiasi kwamba imeona inatosha kwa hiyo matokeo ya kifo ndo kitu kisichosamehewa you can't reverse the action..ila kwa watenda mazuri wao huwa hawafi.mkiwa mnazika mwili mwenzenu huyo bado mzima bado anaishi na watakatifu wengine na MUNgu..hivyo ndivyo nijuavyo mimi.kutosamehewa is all about death
Hueleweki..
 
Pia kujiona wewe ni zaidi ya Mungu nadhani hyo pia ni kufuru na ndio maana shetani mpaka leo hajasamehewa
 
Kwanza Hakuna roho mtakatifu Kuna roho takatifu
Nikirud kwenye swali lako.unapaswa ufaham kwanza Kama roho hio takatifu ndio inaoleta uzima.sasa kwa kuwa watu wengi hukutwa na kifo kwa SABABU tu ya makosa yao yaani dhambi zao.maana mshahara wa dhambi Ni mauti.hakuna ushahidi kuwa wale wakamilifu wasio tenda dhambi huwa wanakufa roho.wenyewe waga wanachukuliwa roho zao hizo TAKATIFU na kupelekwa SEHEMU NYINGINE.kwa hiyo roho za watenda dhambi huwa zinachoshwa na uovu kiasi kwamba matokeo yake huwa kifo ..yaani Ni Kama ile SAA unayotoa bao unaona jinsi usivyoweza kurudisha wazungu ndani ikitoka imetoka kuwazuia Ni haiwezekan ndo maana halisi ya kuiua roho yaani umeitesa roho kiasi kwamba imeona inatosha kwa hiyo matokeo ya kifo ndo kitu kisichosamehewa you can't reverse the action..ila kwa watenda mazuri wao huwa hawafi.mkiwa mnazika mwili mwenzenu huyo bado mzima bado anaishi na watakatifu wengine na MUNgu..hivyo ndivyo nijuavyo mimi.kutosamehewa is all about death
Acha uongo
 
Poleni ndugu wananchi Tanzania kwa msiba

On point
Sisi wanadamu tunapitiwa kweli kutenda maovu lakini Mungu hutuhurumia
Kwa upande wa ukristo Yesu aliwai kusema waweza kumkufuru Yeye lakini sio roho mtakatifu hutasamehewa hata mungu lakini sio roho mtakatifu husamehewi kamwe ulimwengu huu na ule ujao hivi nini maana ya kukufuru roho mtakatifu wajuzi naomba utatuzi....

#mfikwa
#mshana jr
#zitto jr
Asante kwa mwaliko nitarejea kwa kutulia
 
Kwanza Hakuna roho mtakatifu Kuna roho takatifu
Nikirud kwenye swali lako.unapaswa ufaham kwanza Kama roho hio takatifu ndio inaoleta uzima.sasa kwa kuwa watu wengi hukutwa na kifo kwa SABABU tu ya makosa yao yaani dhambi zao.maana mshahara wa dhambi Ni mauti.hakuna ushahidi kuwa wale wakamilifu wasio tenda dhambi huwa wanakufa roho.wenyewe waga wanachukuliwa roho zao hizo TAKATIFU na kupelekwa SEHEMU NYINGINE.kwa hiyo roho za watenda dhambi huwa zinachoshwa na uovu kiasi kwamba matokeo yake huwa kifo ..yaani Ni Kama ile SAA unayotoa bao unaona jinsi usivyoweza kurudisha wazungu ndani ikitoka imetoka kuwazuia Ni haiwezekan ndo maana halisi ya kuiua roho yaani umeitesa roho kiasi kwamba imeona inatosha kwa hiyo matokeo ya kifo ndo kitu kisichosamehewa you can't reverse the action..ila kwa watenda mazuri wao huwa hawafi.mkiwa mnazika mwili mwenzenu huyo bado mzima bado anaishi na watakatifu wengine na MUNgu..hivyo ndivyo nijuavyo mimi.kutosamehewa is all about death
Kinacho kufa ni roho au nafsi?
 
Back
Top Bottom