SoC03 Dhamana zinavyoathiri kesi ukatili wa kijinsia

Stories of Change - 2023 Competition

Mponji123

New Member
Jul 9, 2023
1
1
Utoaji wa dhamana mahakamani hasa kwa kesi za ukatili wa kijinsi kwa watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti kwa kiasi kikubwa zimeendelea kuathiri mwenendo wa kesi hizo kutokana na mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana na hivyo kutumia njia mbalimbali kuharibu mwenendo wa ushahidi.

Kuna haja kubwa ya serikali kupeleka mapendekezo Bungeni ili kubadilisha sheria iliyopo katika katiba ya jamhuri ya muungano inayoelekeza mtuhumiwa yeyote anayekabiliwa na kesi ya jinai kuwa na haki ya kupata Dhamana.

Katika Sehemu ya tatu ya Haki na Usawa katika Katiba Kifungu cha 13 Kifungu kidogo cha kwanza kinaeleza ‘’Watu wote ni sawa mbele ya sheria,na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote,kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria’’.

Lakini pia katika kifungu hicho hicho cha 13 kifungu kidogo cha Sita B kinasema ‘’Ni marufuku wa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinaikutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo anayo hatia ya kutenda kosa hilo’’

Kutokana na vifungu hivyo kesi nyingi Ukatili wa kingono Mkoani Iringa Ubakaji na Ulawiti zimekufa kutokana na Watuhumiwa kuachiwa kwa dhamana na kwenda kutengeneza kesi hizo nje ya mahakama a mashahidi kuhonga au kuahidi kufanyiwa chochote.

Moja wa mfao wa kesi ya mwanafunzi ambaye alidhaniwa kubakwa na Mwalimu wake wa somo la kingereza na baada ya kesi kusomwa mtuhumiwa alikana kosa na akomba kupemwa dhamana na mahakama ikatoa kutokana na kuwa na haki yake ya kikatiba ya kupata Dhamana.

Katika mahakama hiyo Mwalim huyo alisomewa kesi mobile moja ni ya kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akisoma kidato cha tatu na kesi ya pili ilikuwa ni kumpa mimba mwanafunzi huyo licha ya kuwa mwanafunzi alikuwa na Ujauzito unaoonekana lakini Ushaidi huo haukutosha kuendelea kumttia hatiani Mtuhumiwa na aliachiwa kwa Dhamana.

Mama mkubwa wa Muathirika aliamua kumchukua Mtoto huyo na kuishi naye ili kesi hiyo iweze kuendelea kutokana na mazingira aliyokuwa akiishi binti huyo hayakuwa rafiki kiuchumi hivyo ni dahiri mama yake mkubwa alihisi kuwa kesi hiyo itaharibika kutokana na mtuhumiwa kujiweza kwa kiasi Fulani kiuchumi.

Hapa ndio unaona kuna haja kubwa ya serikali kupeleka hati ya Dharura ili kuweza kurekebisha vifungu vya sheria vinavyoruhusu mtuhumiwa wa ubakaji wa ulawiti kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo linazifanya kesi nyingi kushindwa kuendelea kutokana na mashahidi kukutana na mtuhumiwa na kupangwa au kutokwenda kabisa mahakamani.

Licha ya baadhi ya kesi kuendelea kupatikana mashahidi na kutolewa hukumu lakini kesi zilizonyingi zinaharibika kutokana na kukosa ushirikiano kutoka kwa aidha Mlalamikaji ambaye amefanyiwa vitendo vya ukatili kutokana na mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana hivyo mambo mengi kuongea nje ya mahakama na hivyo kuharibu ushahidi.

Mtuhumiwa wa ukatili wa kingono anapokuwa nje kwa dhamana anaweza akawatumia wazee kwa kuwashirikisha na kwenda kwenye familia ya muhanga ili kuweza kuomba msamaha au kutoa fidia na hivyo kuharibu vielelezo na ushahidi wa kesi kwa sababu yeye ndio anakuwa mratibu mkuu na baada ya hapo hakuna shahidi anayeweza kutoa ushirikiano kwa mahakama.

Limekuwa jambo la kawaida kusikia kuna binti amebakwa na kupewa mimba lakini mzazi hana muda wa kwenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa au hata katika kituo cha polisi kutokana na mtuhumiwa kuwa na nguvu ya kiuchumi.

Mfano mwingine ni Mtoto ndani ya familia anaweza kuwa amebakwa na baba yake mzazi au wa kufikia ila mama yake ndio anakuwa wa kwanza kwenda kumtolea dhamana mumewe na baadae kuharibu ushahidi kwa kumsafirisha binti aliyefanyiwa ukatili wa akingono nje ya mkoa au kumpeleka kijijini na hivyo kesi kufa kifo cha kawaida.

Moja ya kesi nyingine nimewahi kuhudhuria ni kesi ya mfanyabiasara kutoka Tunduma kubaka mama yake mzazi na baba wa mtoto ambaye ni mumwe wa mama huyo ndio aliyemuwekea dhamana mwanae ili awe nje na baada ya hapo mtoto huyo ambaye mtuuhumiwa na baba yake woote wakatoweka kusikojulikana jambo ambalo liliifanya mahakama kushindwa kusikiliza upande wa mtuhumiwa licha ya kwamba mahakama ili amuru atafutwe aliyemuwekea dhamana.

Hayo yoote ni baadhi ya matokea ya kifungu hichi cha katiba kinachotoa nafasi kwa watuhumiwa wa ukatili wa kingono kupewa dhamana Mahakamani.

Hapa ndipo unapoona umuhimu wa serikali kupeleka mabadiliko ya sheria hii iliyopo kwenye katiba inayotoa nafasi ya kupewa dhamana badala yake izuie utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa wa makosa ya Ukatili wa kingono.

IMG_20230710_105726_273.jpg
 
Ujue kuna watu wanawekwa ndani afu mwisho ushahidi hakuna, sasa kama umekorofishana na mtu kisha anaamua kukufanyizia huoni utapoteza muda wakati ni uongo?
 
Mkuu umeandika wazo lako kihisia zaidi Ila Sio professional kabsa Wew unataka kusema inamaana mtu akituhumiwa tu kubaka au kulawiti akae ndani bila ya dhamana na jinsi kesi zetu zinavoenda kwa mda Miaka SAA zngne umefikiria wale wanaobambikia wenzao mashtaka au Wew unaona upande mmoja tu,, kwa wenzetu walioendelea hata kesi za mauaji Zina dhamana na Kama mtu akinyimwa Lazma Kuwe na sababu maalum SAS wew unaleta mambo yakihisia zaidi
 
Back
Top Bottom