Dhamana kwa murder suspects

Blaine

JF-Expert Member
Jan 11, 2012
2,275
1,655
Good afternoon wanajf. ninapenda kujua maoni ya watu kuhusu dhamana kwa watuhumiwa wa mauaji. kama tujuavyo murder cases hazina bail na suspect hulazimika kukaa rumamne mpaka uchunguzi ukamilike na hii huweza kuchukua miaka kadhaa. personally naona hii sio sawa kwa sababu zifuatazo
  1. kumweka mtu rumande for years on end sio vizuri kisaikolojia na kiuchumi. akiwa huku hawezi kufanya kazi na kusaidia familia yake, instead analishwa na hela ya walipa kodi na kuwa mzigo kwa walio huru.
  2. hajui lini progress ya uchunguzi. so anakua psychologically affected without knowing when 'kifungo' chake kitaisha
  3. in case akikutwa hana hatia, hakuna namna ya kufidia muda 'alioupoteza' akiwa detained
  4. criteria za kuitwa murder suspect ziko 'too broad', simply being with the deceased shortly before inaweza kukutia matatani. hii inapaswa kuwa confirmed na daktari kuwepo kwa 'foul play', before kumsweka mtu rumande kwa uchunguzi. kuna small tests zinazoweza ku-establish this bila kuchukua miaka
  5. kutoroka kwa mtuhumiwa kunaweza kuepushwa kwa kumnyang'anya passport au kumtembelea randomly nyumbani kwake. hii ni rahisi tuu
  6. hii restriction iliwekwa zamani ambapo technolojia haikuruhusu lakini times have changed, hakuna haja ya kuendelea na sheria za kizamani
Napenda kuona maoni ya wengine
 
Mashitaka ya mauaji hayana dhamana mpaka sasa isipokuwa polisi wanafanya uzembe ktk upelelezi hakuna kesi rahisi ktk upelelezi kama kesi ya mauaji .Ukishakagua sehemu ya tukio na kukusanya vielelezo na maelezo ya mashahidi. Ni kuandikia jalada kulituma kwa DPP kwa uamuzi kama kuna kesi ya kujibu au hapana.
 
Mkuu Blaine maelezo yako ni mazuri sana na yanaibua mjadala though sio kesi za murder peke yake ambazo hazina dhamana hata armed robbery na uhujumu uchumi na uhaini nazo hazina dhamana
Kesi za murder kwa kweli nyingi zinachukua muda sana na upelelezi wake nao unachukua muda sana may be kutokana na polisi wetu kutokuwa na vifaa au na utendaji wao wa kazi nao unachangia
Kumwachia mtuhumiwa wa mauaji kwa dhamana bado serikali ina wasi wasi na reaction ya wananchi au ndugu wa aliyeuwawa na ndo maana wana wasi wasi kuwa akiachiliwa na huu ulimwengu wa visasi ndugu wa aliyeuwawa bado wanaweza kulipiza kisasi kwa maana ile kumuona mtaani hata kama hafanyi kazi kwa ndugu wa aliyeuwawa bado ni issue

Pia kesi za mauaji inatakiwa upepelezi wake uhakikishe kuwa hauachi doubt yoyote maana file litakapopelewa kwa DPP bila ushahidi wa kutosha DPP ana mamlaka lya kuiondoa kesi hikyo mahakamani na ndo maana wanahitaji kukusanya kila aina ya ushahidi ili kumsaidia DPP na judge aliyepangiwa kesi hiyo kuweza kufikia maamuzi sahihi na pia kuhakikisha kuwa wanawapata mashahidi muhimu na wale walioona lile tukio moja kwa moja na sio wale wa hear say ili kuweza kuthibitisha kosa la mtuhumiwa
 
Last edited by a moderator:
Mashitaka ya mauaji hayana dhamana mpaka sasa isipokuwa polisi wanafanya uzembe ktk upelelezi hakuna kesi rahisi ktk upelelezi kama kesi ya mauaji .Ukishakagua sehemu ya tukio na kukusanya vielelezo na maelezo ya mashahidi. Ni kuandikia jalada kulituma kwa DPP kwa uamuzi kama kuna kesi ya kujibu au hapana.
thx for hapo juu. mtu anawekwa rumande w/o ushahidi wowote, process ya DPP ku-determine kama kuna kesi au la isichukue muda mrefu.

Mkuu Blaine maelezo yako ni mazuri sana na yanaibua mjadala though sio kesi za murder peke yake ambazo hazina dhamana hata armed robbery na uhujumu uchumi na uhaini nazo hazina dhamana
Kesi za murder kwa kweli nyingi zinachukua muda sana na upelelezi wake nao unachukua muda sana may be kutokana na polisi wetu kutokuwa na vifaa au na utendaji wao wa kazi nao unachangia. huoni kama kuboreshwa kazi ndio jambo sahihi kuliko kumsweka mtu indefinetly?
Kumwachia mtuhumiwa wa mauaji kwa dhamana bado serikali ina wasi wasi na reaction ya wananchi au ndugu wa aliyeuwawa na ndo maana wana wasi wasi kuwa akiachiliwa na huu ulimwengu wa visasi ndugu wa aliyeuwawa bado wanaweza kulipiza kisasi kwa maana ile kumuona mtaani hata kama hafanyi kazi kwa ndugu wa aliyeuwawa bado ni issue. nadhani tunahitaji poll kujua public opinion kuhusu dhamana. innocent till proven guilty lakini. nchi zingine mbona hakuna 'visasi vya ndugu', tuache sheria ichukue mkondo wake. pia mtuhumiwa atakuwa na staha na 'kutowachokoa' ndugu wa wafiwa.

Pia kesi za mauaji inatakiwa upepelezi wake uhakikishe kuwa hauachi doubt yoyote maana file litakapopelewa kwa DPP bila ushahidi wa kutosha DPP ana mamlaka lya kuiondoa kesi hikyo mahakamani na ndo maana wanahitaji kukusanya kila aina ya ushahidi ili kumsaidia DPP na judge aliyepangiwa kesi hiyo kuweza kufikia maamuzi sahihi na pia kuhakikisha kuwa wanawapata mashahidi muhimu na wale walioona lile tukio moja kwa moja na sio wale wa hear say ili kuweza kuthibitisha kosa la mtuhumiwa. hii process takes 'too long'. kama kuna 'foul play' itaonekana kwenye vipimo vya daktari na upelelezi mwingine, sio lazima wawepo mashahidi walioona tukio.
red replies for anayetumia picha ya mume wa mariah carey kama avatar.
 
Back
Top Bottom