Dhahabu ya kwanza kupatikana nchini Kenya

Igabiro

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
242
27
Kampuni ya GoldPlat imefanikiwa kupata mche wa kwanza wa dhahabu (first bar of gold) kutoka katika mgodi wa Kilimapesa, hiyo ndio dhahabu ya kwanza kupatika katika nchi ya Kenya, Sasa hapa ngoja tuone hawa jirani zetu watafaidika vipi na huo mgodi wao, labda inaweza kutusaidia hata sisi Tanzania wenye migodi lukuki ya dhahabu ambayo hatuna faida nayo.

Nawakilisha
 
tz itafaidika km ikiwa mjanja km wwao kwa kusema that gold found in kenya is fake the real one is in tz

as wao wanavyounad mt.kilimanjaro
 
Maskini kenya kumbe walikuwa hawana hata mgodi mmoja wa dhahabu? Btw nawatakia kila la heri waweze kufaidika nayo na sio wafanye makosa kama yetu.
 
Maskini kenya kumbe walikuwa hawana hata mgodi mmoja wa dhahabu? Btw nawatakia kila la heri waweze kufaidika nayo na sio wafanye makosa kama yetu.

Tutegemee uchumi wao kukua mara dufu!
 
kwa nchi kama kenya,nazani hata wakiwa na huo mgodi mmojha tu unawatosha,ndani ya muda mchache watakuwa wameshafanikiwa zaid ya hapo walipo,
tz ni ya tatu katika uchimbaji baran africa,lakini hatuna tofauti na watu wanaoishi haiti
 
Dhahabu ndio inakuza uchumi? mnanchekesha!

south africa hii mambo imewasaidia-wameweza kusonga mbele
sisi watu wakishaweka vidani vya dhahabu puani wanakuwa wameridhika,hata kama thousand of tons zinaibiwa hawana mpango nazo
 
Wakenya wako SMART kwenye mambo yao na hilo liko wazi kabisa, usitegemee watu kuleta ujanja ujanja na natural resources za wakenya, kwa kweli muamko wawakenya ni moja ya mtaji wao mkubwa kwa sasa.
 
Dhahabu ndio inakuza uchumi? mnanchekesha!

dhahabu ndiyo inabainishwa na sarafu za nchi. kwa mfano uzito au thamana ya dola ya marekani itabainishwa na kiwango cha dhahabu wameweza kuweka katika benki zao. kwahivyo, ndio dhahabu inakuza uchumi
 
Maskini kenya kumbe walikuwa hawana hata mgodi mmoja wa dhahabu? Btw nawatakia kila la heri waweze kufaidika nayo na sio wafanye makosa kama yetu.

kwani watanzania tuna mgodi gani wa dhahabu? migodi yote ni ya makaburu na wamarekani! HATUNA mgodi hata mmoja.
 
Kampuni ya GoldPlat imefanikiwa kupata mche wa kwanza wa dhahabu (first bar of gold) kutoka katika mgodi wa Kilimapesa, hiyo ndio dhahabu ya kwanza kupatika katika nchi ya Kenya, Sasa hapa ngoja tuone hawa jirani zetu watafaidika vipi na huo mgodi wao, labda inaweza kutusaidia hata sisi Tanzania wenye migodi lukuki ya dhahabu ambayo hatuna faida nayo.

Nawakilisha
Kuna uwezekano mkubwa kuwa kwa kuwa na mgodi huo mmoja, ambao uzalishaji wake si wa juu, Kenya ikauza nje dhahabu nyingi. Uzoefu unaonyesha kuwa ingawa kenya haina tanzanite, lakini takwimu za mauzo ya vito hivyo duniani zinaonyesha kuwa Kenya inauza sana tanzanite. Sitashangaa kama dhahabu ya tanzania ikavushwa mpaka Kenya kimagendo na kisha ikauzwa na kuwanufaisha jirani zetu
 
Back
Top Bottom