Dhahabu iliyotaka kuibwa Geita ina thamani ya Sh. bilioni 40 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhahabu iliyotaka kuibwa Geita ina thamani ya Sh. bilioni 40

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jan 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Polisi limesema dhahabu iliyotaka kuibiwa na majambazi katika tukio la uvamizi wa mgodi wa Geita, ni miche 26 yenye uzito wa kilo 586.57 zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 40.

  Aidha, Jeshi kilo limegundua silaha zaidi kutoka jirani na eneo la tukio bunduki bandia ya kutungulia ndege,majengo na magari ya delaya iiitwayo RPG-7Viliyoitengenezwa kwa mbao.

  Nyingine ni SMG namba UG 81151998 na risasi 21pamoja na pea mbili za sare za jeshi, suruali na makoti ambavyo vilipatikana eneo la tukio juzi jioni hivyo na kufanyaa idadai ya silaha zilizopatikana eneo hilo kufikia bunduki mbili aina ya SMG, na risasi 89 na mabomu matano ya kurusha kwa mkono.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Deusdedith Nsimeki, amesema kuwa upelelezi ilishaanza kwa kutumia baadhi ya vitu vilivyopatikana eneo la tukio.

  Vitu hivyo ni simu mbili alizokutwa nazo marehemu eneo la tukio, baada ya kupigwa risasi kwa ushirikiano wa walizni wa mgodi na polisi katika tukio la kujaribu kupora dhahabu iliyokuwa katika hatua ya kusafirishwa kwa ndege kupelekwa nje ya nchi.

  "Mpaka sasa hakuna anayeshikiliwa, lakini uchunguzi wa awali umeanza kutoa dira na ili kuthibitisha iwapo watuhumiwa waliotoroka na aliyeuawa walikuwa ni raia au sio raia," alisema.

  Kuhusu kiasi cha dhahabu kilichoibiwa, Nsimeki alisema ni kilo 586.57 na thamani yake inategemea thamani ya dola kwenye soko kwa siku hiyo, lakini alisema ni zaidi ya Sh. bilioni 40.

  Juzi katika eneo la tukio kzilipatikana risasi 62 za SMG na risasi mbili za bastola ambapo inasaiwa kuwa huenda majambazi hao walikuwa na zaidi ya risasi 100 za SMG na kuwa polisi walikuwa wanajaribu kuchunguza eneo la tukio kwa kuhisi kuwa kunaweza kupatikana vielelezo zaidi.

  Katika tukio hilo, walinzi wawili waliokuwa wakishiriki katika upakuaji dhahabu hiyo ili kusafirishwa walijeruhiwa vibaya kwa risasi ikiwa ni pamoja na gari moja kuharibiwa katika uwanja wa ndege wakijiandaa kuisafirisha kwenda jijini Dar es Salaam.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hii ni dalili tosha kwamba kila wiki wachimba dhahabu wanasafirisha dhahabu ya billioni 40 bila mamlaka yetu kuwa na taarifa yeyote na taifa likiendelea kuambulia patupu.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Serikali hapo penye dhahabu haipo imelifumbia macho hilo tatizo nchi yetu inazidi kufa bado kuzikwa hatuna viongozi jamani.
   
Loading...