DEVIL’S FAMILY (FAMILIA YA MASHETANI) 17
ANGALIZO: KAMA UPO CHINI YA UMRI WA MIAKA 18. TAFADHALI USISOME HII HADITHI.
ILIPOISHIA
Mlango wa nyuma ukafunguliwa na akaingia ndani ya gari hilo. Akawatazama wasichana wengine sita alio wakuta ndani ya gari hiyo ambao nao pia wamejiremba na kupendeza. Akawasalimia wasichana hao na safari ikaendelaa. Kwa mwendo wa dakika ishirini, wakawa wamefika katika jumba la kifahari linalo milikiwa na James.
“Huyu ni mteja wangu namba moja. Sinto hitaji malalamiko yoyote kutoka kwake. Chochote atakacho kitaka mukifanye tuna elewana”
Manamama aliye kaa siti ya mbele akiwa na dereva alizungumza.
“Sawa madam”
Wasichana wote walijibu huku Rose akitajibu kimya kimya. Wakashuka ndani ya gari na wakaingia ndani jumba la James.
“Warembooo karibuni sanaaaaa”
James alizungumza kwa furaha hukua kishuka kwenye ngazi akiwa amevalia boksa pekee na mkononi mwake akiwa na chupa ya pombe kali ikimaanisha tayari kichwa chake kimesha waka moto.
ENDELEA
“Nimekuletea pisi kali za kwenda. Watoto wazuri kama hawa huwezi kuwapata popote hapa Tanzania”
Mwanamama ambaye ni dalali alizungumza na kumfanya James kuwasogelea wasichana hao. Akamshika mmoja na kumgeuza nyuma na kuangalia makalio yake. Akamsogelea Rose na kumgeuza. Akayaminya makalio ya Rose.
“Una matak** malaini sana aissiii”
Rose akatabasamu huku akiyatingisha tingisha makalio yake.
“Huyu nimuemuelewa sana”
James alizungumza akimtazama Rose usoni mwake.
“Kweli”
“Yaah wengine rudi nao leo nahitaji mmoja tu na nitamchukua huyu”
“Sio kawaida yako tajiri”
“Unajua mishe mishe za harusi zimenichosha sana. Namuhitaji huyu mmoja ni relax naye hata kwa siku mbili.”
“Sawa kwa kuwa umewalipia mimi sina tatizo tajiri wangu”
Mwanamama akaondoka na wasichana wengine na kumuacha Rose.
‘Asije akawa amenishtukia?’
Rose aliwaza akilini mwake akimtazama James akifunga mlango wa nyumba yake.
“Utatumia kinywaji gani?”
“Chochote mpenzi”
Rose alizungumza kwa sauti laini iliyo mfanya James kuzidi kuchanganyikiwa.
“Kwa mrembo kama wewe wine ita kufaaa”
James alizungumza huku akitembea hadi kwenye kaunta iliyopo sebleni kwake, ambayo imejaa vinywaji vya kila aina. Akachukua chupa ya wine na kurudi alipo kaa Rose. Akamiminia katika glasi na Rose akaanza kunywa wine hiyo.
‘Nita kuua siku ya leo’
Rose alizungumza akimpigia mahesabu James namna gani ya kumuua/
“Wewe sio malaya”
James alizungumza kumfanya Rose kushtuka kidogo.
“Una maanisha nini?”
“Nimetembea na wanawake wengi sana wanao jiuza. Ila wewe ni wa tofauti sana. Hujaguswa”
“Nisiwe muongo ndio nina anza”
“Hahahaaa……Nifwate”
Wakanyanyuka sebleni na wakaingia chumbani kwa James.
“Una chumba kizuri”
“Asante”
James alizungumza huku akiwasha tv. Rose akashtuka kujiona picha yake katika tv hiyo.
“Nakufahamu. Wewe ni Rose mtoto wa mzee Chiko. Kama umekuja kunilipizia kisasi tafadhali huto weza kufanya hivyo”
Rose akashtuka kwani alicho kuwa ana kipanga kimeshtukiwa mapema sana.
“Baba yako amemuua baba yangu na kaka zangu kwa kuwatupa katika bwawa la Mamba?”
“Sina taarifa hiyo”
“Hilo ndio lililo tokea. Wamewaua kikatili sana. Sina budi zaidi ya wewe kuwa atakaye peleka uchungu kwao”
Rose akaitupa glasi ya wine aliyo kuwa chini.
“Kabla ya kufanya hivyo unapaswa kujua jambo moja. Wine uliyo kuwa ina sumu ambayo baada ya dakika mbili zijazo ita kuua”
Rose akashtuka huku akihisi mwili wake kumlegea. Akajigusa puani na kuona damu zikianza kumchuruzika.
“Kwa nini nimekufa kizembe namna hii”
Rose akaanguka chini. James akachukua kichupa kidogo juu ya dreasing table.
“Hii ni antidote itakayo yaokoa maisha yako”
“Na….an…..aaomba unipatie”
Rose alizungumza kwa shida kwani tayari sumu imesha udhohofisha mwili wake. James akamsogelea alipo lala. Akamnywesha dawa ya kuondoa simu mwilini. Akamnyanyua Rose na kumlaza kitandani ajisikilizie afya yake.
“Imekuwaje ukanijua?”
Rose alimuuliza James kwa sauti kavu baada ya dakika arobaini kumalizika toka apewe sawa ya kumsaidia kuondoa sumu aliyo kunywa.
“Hakuna anaye ingianyumbani kwangu bila ya kutambua taarifa zake. Hivyo nilitamba taarifa zako wakati tu mulipo shuka kwenye gari. Taratibu Rose akaka kitandani, mwili wake ukiwa hauna nguvu.
“Mimi sio muuaji. Japo nina unda silaha ambazo hutumika kuuua watu”
“Kwa nini hujataka kuniau?”
“Hakuna sababu ya mimi kukuua wewe”
“Ina maana wewe hushrikiani na wazazi wako?”
“Mimi ni watofauti. Maisha yangu ni ya tofauti na hata moyo wangu ni watofauti.”
James akanyanyuka kwenye sofa alilo kali na akamfwata Rose kitandani alipo kaa.
“Katika maisha yangu nilisha wahi kuumizwa na mapenzi. Nikaamua kuwa malaya wa kutembea na kila aina ya wanawake. Ila siku nilipo iona picha yako nikajihisi kitu cha tofauti sana moyoni mwangu”
Rose akamtazama James kwa mshangao.
“Ndio Rose. Mimi sina kawaida ya wanawake kuingia ndani kwangu hapa na nisimshuhulikie. Ndio maana hata yule mwan amama dalali wa wanawake naye alishangaa leo nina mrudishia wanawake wake na kukuchukua wewe pekee”
“Sikukuchukua kwa sababu ya kutaka kukudhuru. Ila nimekuchukua kwa sababu nataka nikuambia yale yaliyo moyoni mwangu kuhusiana na wewe”
Rose akakaa kimya akimshangaa James.
“Rose una maisha na ndoto katoka maisha yako. Leo una weza kuelewa kwamba ulibakisha dakika chache kabla ya kila aina ya ndoto kwenye maisha yako kutoweka. Na zikeisha leo ndoto zako na historia ya maisha yako ingekufa leo. Yale yote uliyo yasomea South Korea leo hii yangebaki kama stori.”
“Nakuomba sana kwa sasa usimame na kuendeleza kile kilicho achwa na baba yako na mama yako. Una nafasi ya kufanya kapumzi zenu kukua kuliko kuwekeza nguvu kubwa kwa ajili ya kulipa kisasi ambacho leo hii maisha yako yangefikia mwisho”
Rose machozi yakaanza kumlenga lenga.
“Nje watu wengi huniona mimi kama sina akili nzuri na ni play boy ndio maana hata kwenye mambo makubwa ya kampuni zetu huwa sishirikishwi na anaye play part zote ni mdogo wangu Jack. Ila ukweli nina akili kubwa sana na muda mwengine sipendezwi na mienendo ya maisha ya familia yangu ila ndio nimesha zaliwa ndani ya hii familia”
James akamtazama Rose.
“Una taka nini kwangu?”
“Nataka nikuoe”
“Hahahaaaaa”
Rose akacheka sana.
“Kwa nini una cheka?”
“Kweli mtoto kutoka familia ya Tiger aje kunioa mtoto kutoka familia ya Chiko….Haijawahi kutokea”
“Ni kweli ila sisi tuna weza kubadilisha histori hiyo kutoka kuwa wapinzani hadi kuwa mke na mume”
“Kwenye maisha yangu sijapanga kuolewa na sihitaji kuwa mke wa mtu”
“Rose. Najua huna roho mbaya. Hata mimi sina roho mbaya. Tafadhali naomba ufikirie wazo langu”
“Nahitaji kuondoka”
Rose akashuka kitandani, akapepesuka kidogo ila James akamdaka.
“Naomba ufikiria nilicho kuambia”
“Sina cha kufikiria. Asante kwa kuto niua leo”
Rose akafungua mlango na akatoka chumbani kwa James. James naye akashuka na akamkuta Rose sebleni.
“Wakati mwengine tukikutana uadui uta endelea kati yetu na lolote lina weza kutokea”
“Sawa mke wangu mtarajiwa”
“Siwezi kuwa mkeo na isitoshe kiumri umenipita sana”
“Najua ila kwenye ndoa umri sio tatizo”
Rose akamtazama James kuanzia juu mpaka chini.
“Nyumba yangu ipo mbali na mji. Usafiri huku ni kipengele na ukiangalia sasa tayari giza limesha tanda. Una onaje nikakusindikiza na gari yangu”
“Hapana”
“Tafadhli. Sina bifu na wewe Rose”
Rose akashusha pumzi taratibu.
“Sawa”
“Nachukua funguo ya gari na kuvaa nguo”
James akapandisha gorofani, akavaa nguo haraka haraka na akarudi sebleni. Akamkuta Rose akimrubiria. Wakaingia ndani ya hari na kuondoka nyumbani kwa James. Kwa mara kadhaa Rose macho yake yana mtazama James.
‘Kuna nini ana kitaka kwangu huyu kaka. Alikuwa na uwezo wa kuniua kwa nini hajaniua?’
Rose aliendelea kijiuliza huku akimtazama Jamse na kukosa majibu ya maswali yake.
***
Mrs Tiger akakurupka kitandani. Akatazama nje ya tayari giza limetanda.
“Umeamkaje mpenzi wangu”
Dany alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa alilo kaa.
“Saa ngapi sasa hivi?”
“Saa nne usiku”
‘Fuc** ina maana…..”
Mrs Tiger akashuka kitandani. Akafungua pochi yake na akatoa simu yake. Hapakuwa na missed call yoyote. Akashusha pumzi taratibu.
“Niliona nisikusumbue baada ya kumaliza kipindi cha pili cha show”
Dany alizungumza akimshika Mrs Tiger mkono.
“Nahitaji kuondoka”
“Huitaji bao la tatu”
“Sina nguvu za kufanya mapenzi tena. Hamu yangu imeniiisha”
Mrs Tiger akaingia bafuni na Dany akamfwata kwa nyuma.
“Ngoja nikuogeshe”
Dany akafungua koki ya maji ya bomba la mvua. Maji yakaanza kumwagikia Mrs Tiger mwilini mwake. Jack akachukua sabuni ya maji na kuanza kumwagia Mrs Tiger sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsafisha.
“Una mwanamke?”
Swali la Mrs Tiger aliye mpa mngongo Dany, likamfanya Dany kumgeuza taratibu Mrs Tiger na akatazamana naye.
“Mwanamke sina. Ila nina fanya mapenzi kwa pesa”
“Kwa hiyo una nunuliwa kama nilivyo kununua?”
“Ndio ukweli wangu”
Dany alizungumza akiyatomasa maziwa ya Mrs Tiger taratibu.
“Sawa”
“Mbona kama una taka kuzungumza jambo”
“Umeujua uchi wangu wangu. Biashara yako ya kununuliwa na wanawake imeishia leo”
“Nitaishije mjini”
“Nita kuhudumia. Endapo nita sikia au nita jua una mwanamke mwengine unaye mtomb*** nita kata hizi pumb** zako na zitakuwa chakula cha mbwa wangu”
“Umeipenda show yangu?”
Mrs Tiger hakujibu chochote ila moyoni mwake ana furahia alicho pewa kwani amekofikishwa kileleni mara nyingi tena mfululizo mfulizo.
“Eti babe umependa show”
“Niogeshe nahitaji kuondoka”
Mrs Tiger hakutaka kuonyesha udhaifu wake mbele ya Dany kijana mdogo kiumri ambaye hata mwanaye wa mwisho Jack ni mkubwa kuliko Dany. Wakatoka bafuni mara baada ya kuoga. Mrs Tiger akaanza kuvaa nguo zake.
“Narudi nikisikia stori ya wewe kuonana na mimi mahala popote nita kuua.”
“Siwezi”
“Usiseme huwezi una marafikia au rafiki. Ukienda ukajisifia jua una yaweka reheni maisha yako na familia yako”
“Nakuahidi, kwa utamu wa kum** yako sinto muambia yoyote yule. Ukiona siri imevuja basi umkabe rafiki yako”
“Ni rafiki yangu na nina mjua vizuri hawezi kuongea ujinga huu”
“Sawa”
“Nitajie namba yako”
Dany akamtajia Mrs Tiger namba yake na akainakili kwenye simu.
“Mimi ndio nitakuwa nina kutafuta umenielewa?”
“Nakuelewa”
Mrs Tiger akatoa vibunda viwili.
“Dola elfu kumi najua hujawahi pewa pesa ndefu kama hii. Hivyo mbo** yako kuanzia hivi sasa mimi ndio mmiliki halali. Kula shiba, fanya mazoezi nitakuwa nina kuhitaji ninapo jisikia mimi”
“Sawa mpenzi. Asante sana”
Dany alizungumza furaha kwani kwenye maisha yake ya kujiuza kwa wanawake wenye uhitaji, kubwa aliyo wahi kulipwa ni milioni mbili za Kitanznaia ila leo hii ana lipwa dola za kimarekani elfu kumi tena kwa bao mbili tu zilizo mpagawisha Mrs Tiger.
“Nasisitiza tena Dany. Mimi ni mtu mbaya sana. Ukinizingua nita kuzingua unanielewa?”
“Nakuelewa madam”
“Sitanii”
“Sinto kuangusha nina tulia na wewe. Vipi usalmaa wangu kutoka kwa mume wangu”
“Usiri ndio uta kufanya uishi na mimi miaka mingi. Mume wangu ana watu kila mahala. Kila sehemu hivyo ukiongea neno moja kuhusiana na mimi lita mfikia na atakacho kufanya shauri yako”
“Sawa”
“Unatumia usafiri gani?”
“Mimi sina usafiri”
“Una maanisha?”
“Mara nyingi usafiri wangu ni pikipiki na bajaji. Bado maisha kwa upande wangu yapo kinyume sana. Kwani nimepanga room na seble tu. Bado nina jitafuta kimaisha”
Mrs Tiger akamtazama Dany.
“Nita fwatilia hayo unayo niambia nikigundua ni kweli basi nita kubadilishia maisha yako ila nikijua una nidanganya basi uta juti hii siku ya kwanza kuonana na mimi. Nina chukia uongo, sipendi uongo na simpendi mtu muongo. Unanielewa?”
“Nakuelewa”
Mrs Tiger akatoa shilingi laki moja na kumpatia Dany.
“Pesa hii utatumi kwenye usafiri. Ukitoka hapo nje uta tembea hadi barabarani kule japo kuna tisha tisha ila tembea wewe ni mwanaume. Ukifika uta panda boda”
“Naonba unipatie lifti”
“Gari yangu una kamera ndani. Mume wangu ana weza kuangalia kinacho endelea ndani ya gari langu hivyo sitaku kukuhatarishia maisha yako mapema kiasi hichi”
“Sawa. Asante”
Dany akaziweka pesa zake mfukoni mwa suruali yake na akaondoka nyumbani kwa Mrs Tiger huku Mrs Tiger akimfwatilia Dany kupitia juu ya gorofa jinsi anavyo katiza katika njia ya kuingilia katika nyumba hiyo ambapo njia hiyo hiyo imejaa miti mingi inayo fanya usiku patishe.
ITAENDELEA
Mchaka mchaka mpya umeanza. Japo ametembea na wanawake wengi ila moyo wa James umeangukia kwa mtoto wa adui wa fmailia yao Rose ambaye naye ana uadui na familia ya mzee Tiger. Je Rose ata kubaliana na ombi la James kumpenda na kutaka kumuoa? Ungana nami katika stori hii ya kusisimua sehemu ya 18.