TuntemekeSanga
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 1,346
- 863
kumbuka kuwa, kunena ni rahisi kuliko kutenda. just imagine kwamba, wewe ndo umeishikilia taasisi. could you perform more than him?Sasa kwa mfano kama anayeishika hiyo nafasi hajiheshimu watu watafanyaje? Kama kweli urais ni taasisi inapaswa kuanza na anayeishika hiyo nafasi afanye kazi akitambua kwamba ni taasisi na siyo yeye peke yake ndo mwenye maamuzi. Vinginevyo itakuwa ngumu kwa mtu wa kawaida kuiheshimu hiyo taasisi!
Ukisema uraisi ni taasisi "tukufu" una maana haina mawaa wala makosa na hivyo haiwezi kukosolewa? Hapana, ni lazima ikosolewe tena wazi wazi. Kama serikali hiyo hiyo inateua, tengua, tumbua na ukosoa wengine wazi wazi kwa nini na yenyewe isitarajie yayo hayo?yuko sahihi ndg.kibamba. urais ni taasisi kubwa na tukufu kimsingi. inapaswa kuheshimiwa
Anatafuta cheo huyoooKibamba ashaanza kuisoma namba, naona anataka kujipendekeza. Amepingwa, Obama na sasa Trump anapingwa anasema eti Rais harakiwi kukosolewa!!! Duh njaa mbaya.
Like ni moja kutoka kwangu,odherwise ungezipata lukuki.Kule Marekani pamoja na Donald Trump kuapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani lakini maelfu ya Wamarekani wanafanya maandamano kumpinga Rais Trump. Kitu kizuri kabisa ni kwamba Polisi wanawapa ulinzi hao waandamanaji kuonesha hisia zao.
Eti Kibamba anasema hapa kwetu huruhusiwi hata kusema Rais hadharani kama una mtazamo hasi. Halafu huyu Kibamba eti ni mwanasheria.
Jamani kweli hizi nafasi za kuteuliwa zinatutoa UFAHAMU. Na hizi nafasi ndiyo shetani mkubwa kwa wasomi wetu. As far as nafasi hizi zitaendelea kuwa mikononi mwa mtu mmoja. Wasomi wa Tanzania wataendelea kufikiri kwa kutumia MATUMBO yao badala ya kufikiri kwa kutumia VICHWA vyao. Poor Tanzanians!
Kishakuwa kama yuleeeeKibamba nae ni wale wale
acha uongo wewe mimi nilimsikiliza, alisema kuna baadhi ya mambo ambayo upinzani hawatakiwi kuyaongea waziwazi, mfano akatolea mfano Raisi wa Gambia mwaka jana Upinzani walimwambia kuwa siku ukitoka Ikulu tunakupeleka mahakama ya ICC, kwahiyo kiongozi kama alikuwa ananyanyasa watu au alifanya mabo ambayo sio ndio unakuwa mwanzo wa kugoma kutoka madarakani sababu anajua kitakachofuata mbele yake, hivyo akawa ametoa tahadhari kwa upinzani kutafakari baadhi ya mambo wakae nayo kisiri maana wakiyatoa na raisi akaona baadae yanaweza kumletea shida mbeleni, ndio unakuwa mwanzo wa kuiweka kinga ya utawala.Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini Dar es Salaam , ndugu Deus Kibamba asema Rais hawezi kupingwa waziwazi,amedokeza iwapo mtu ana mtazamo hasi kwa rais anapaswa kutafakari moyoni badala ya kumzungumzia vibaya rais. Amewaelezea wapinzani wa Tanzania jinsi wanavyomkosoa rais bila kuona mema yake.
Ameyasema hayo katika kipindi cha 360 cha Clouds TV .
Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini Dar es Salaam , ndugu Deus Kibamba asema Rais hawezi kupingwa waziwazi,amedokeza iwapo mtu ana mtazamo hasi kwa rais anapaswa kutafakari moyoni badala ya kumzungumzia vibaya rais. Amewaelezea wapinzani wa Tanzania jinsi wanavyomkosoa rais bila kuona mema yake.
Ameyasema hayo katika kipindi cha 360 cha Clouds TV .
Kama hukutaka kuiga mngeendelea na tawala zenu za kitemi ...na si tawala za kidemokrasia..pumba kweli nyie .,eti kiti kitukufu......Sio kila kitu tunaiga Wa-Marekani, mbona hamtaki kuiga na U-shoga??..anachomaanisha Bwana Kibamba ni kwamba kuna jinsi na taratibu za kuikosoa taasisi ya Uraisi..ndio maana amesema, kabla ya kuamua kuongea inafaa kufikiri kwa makini, utaratibu utakaoutumia kufikisha ujumbe wako. Na endapo busara itatumika, huo ujumbe utafika vizuri zaidi, na utafanyiwa kazi.
Kwa sisi Wa-Tanzania, tunafahamu, humo majumbani kwetu, Baba au Mama anaweza kukosea, na tunajua jinsi ya kuwaambia wamekosea.Utaratibu tunaitumia kuwakosoa watu tunaowaheshimu hauwezi kuwa sawa na jinsi nitakavyo mkosoa rafiki yangu wa hapa mtaani kwangu.
Hamna cha maana ulichoandika kwenye hili bandiko lako, zaidi umeonyesha tu udhaifu ulionao kwenye uelewa wa mambo.Kama hukutaka kuiga mngeendelea na tawala zenu za kitemi ...na si tawala za kidemokrasia..pumba kweli nyie .,eti kiti kitukufu......
Tatizo lenu nyie nzi wa Lumumba hamsikii wala hamuoni,wala chembe ya fikra pevu hamna.,rais asikosolewe .,kama sio upumbafu uliopitiliza ni nini? ?? Alikosea ktk teuzi kikatiba mkatetea mishipa ikawasimama,Leo eti mnampongeza kwa maamuzi aliyoyafanya kwa possi .,ningekuwa na uwezo nyie kila cku bakora tu mpaka akili zenu zikae sawa .,upumbafu wenu ndio unatugharimu ktk maendeleo ya taifa letu.,ujinga wenu unatufanya wote tuonekane mabogasi kimataifa..Hamna cha maana ulichoandika kwenye hili bandiko lako, zaidi umeonyesha tu udhaifu ulionao kwenye uelewa wa mambo.
Soma tena bandiko langu kwa makini, nimeeleza kwamba, sisi wa Tanzania hatupaswi kuiga kila linalofanywa na Marekani. Tutayachukua yale tunayoona yanafaa, na yale yasiotufaa tutawaachia wao.
Kama unaona tuliamua kuiga Democrasia, basi hilo tuliona linafaa, na kama wewe unadhani Democrasia ni kutumia lugha zisizo na staha katika kufikisha ujumbe wako basi bila shaka hata Democrasia yenyewe wala huielewi.
yuko sahihi ndg.kibamba. urais ni taasisi kubwa na tukufu kimsingi. inapaswa kuheshimiwa