Desmond Tutu aomba kusaidiwa kufa atakapougua

Desmond Tutu aomba kusaidiwa kufa atakapougua

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,348
Reaction score
15,109
Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu amesema katika ujumbe wake wa siku yake ya kuzaliwa katika gazeti la Washington Post kwamba angependelea kusaidiwa kufa.

Katika ujumbe huo Tutu alisema: Nimejiandaa kufa na nimesema wazi singependelea kuendelea kuishi kwa gharama yoyote.Ningependa kutibiwa na mapenzi na kuruhusiwa kufariki vile nipendevyo.Watu wanaokufa wanapaswa kuwa na haki ya kuchagua vile na lini watakavyokufa.Ninaamini kwamba,mbali na uuguzi uliopo ,chaguo lao linafaa kushirikisha kusaidiwa kufa kwa heshima.

Alitangaza hatua yake ya kuunga mkono wazo hilo baada ya kulipinga 2014.

Habari kwamba Desmond Tutu angependa asaidiwe kufa sio swala la kushangaza nchini Afrika Kusini.

Swala la kusaidiwa kufa limeigawanya nchi hiyo kwa kipindi cha muda sasa.

Mwaka uliopita mahakama kuu katika mji mkuu wa Pretoria iliamuru kwa kumpendelea mgonjwa mmoja aliyekuwa anaugua saratani kupitia kiasi, Robin Strasham-Ford ambaye alikuwa ametoa ombi la kusaidiwa kufa.

Alikuwa amesalia na wiki mbili pekee kufariki na alitaka sheria irekebishwe ili asaidiwe kufa bila ya kuwepo kwa kesi.

Sheria ilikuwa wazi,daktari yoyote ambaye angemsaidia mgonjwa kufariki angepewa hukumu ya miaka 14 jela.

Taifa hilo halina sheria ya kusaidiwa kufa,huku katiba ikilinda haki ya kila mmoja ya kuishi.

1476015319130.jpg
 
Desmond hatakufa bali atalala kwa amani siku yake ikifika
 
Sheria ya kusaidiwa kufa ni muhimu. Haina maana kutesekea kitandani.
 
Hii kitu iruhusiwe hata Tanzania, na kama mtu anataka kuchangia kiungo chake basi aruhusiwe
 
South Africa's Archbishop Desmond Tutu has revealed that he wants to have the option of an assisted death.

The Nobel Peace Prize laureate and anti-apartheid campaigner said that he did "not wish to be kept alive at all costs", writing in the Washington Post newspaper on his 85th birthday.

He was hospitalised last month for surgery to treat recurring infections.

My take
Hii ni dalili ya kukata tamaa au ni kilipunguzia taifa gharama za matibabu. Kwa sababu najaribu kijiuliza kama ni ujasiri mbona asichukue maamuzi mapema?
 
Ukiugua kwa muda mrefu, au ukiwa na ugonjwa MBAYA sana, Akili huwa zinaruka.
 
South Africa's Archbishop Desmond Tutu has revealed that he wants to have the option of an assisted death.

The Nobel Peace Prize laureate and anti-apartheid campaigner said that he did "not wish to be kept alive at all costs", writing in the Washington Post newspaper on his 85th birthday.

He was hospitalised last month for surgery to treat recurring infections.

My take
Hii ni dalili ya kukata tamaa au ni kilipunguzia taifa gharama za matibabu. Kwa sababu najaribu kijiuliza kama ni ujasiri mbona asichukue maamuzi mapema?
Umri unatosha kumfanya afikiri hivyo.
Kwa maana amekwisha itumikia dunia vya kutosha kiasi kwamba kuendelea kuwepo kwake hakubadilishi chochote tena.

Ni heri aondoke kwa amani huku akijua anaondoka (sio kwa dizain ya wahehe)
 
South Africa's Archbishop Desmond Tutu has revealed that he wants to have the option of an assisted death.

The Nobel Peace Prize laureate and anti-apartheid campaigner said that he did "not wish to be kept alive at all costs", writing in the Washington Post newspaper on his 85th birthday.

He was hospitalised last month for surgery to treat recurring infections.

My take
Hii ni dalili ya kukata tamaa au ni kilipunguzia taifa gharama za matibabu. Kwa sababu najaribu kijiuliza kama ni ujasiri mbona asichukue maamuzi mapema?
Mkifikia huo umri ndo mtaona kwann anasema hivyo
 
Hapo ndipo umuhimu wa kuhalalisha matumizi ya bangi unapohitajika, angepulizia pafu zake tatu kila siku na kuwa mtulivu, mwenye amani hadi roho yake itakapoacha mwili. maumivu ya mawazo ni mabaya kuliko hata haya ya mwili.
 
c398c21805bf139da7b41efb41ebe9e4.jpg

Tutamuenzi kwa hili "Earlier this year, he blessed his daughter Mpho's marriage with her female partner, despite South African Anglican law on marriage stating that "holy matrimony is the lifelong and exclusive union between one man and one woman".
 
ndo yule aliyesema Trump akishinda anarudi Africa ? Anarudi lini sasa
 
c398c21805bf139da7b41efb41ebe9e4.jpg

Tutamuenzi kwa hili "Earlier this year, he blessed his daughter Mpho's marriage with her female partner, despite South African Anglican law on marriage stating that "holy matrimony is the lifelong and exclusive union between one man and one woman".
Huyo kweli anahitaji kuuwawa - kusaidiwa kufa ni kuuwawa jamani. Askofu Mkuu mzima anabariki bintiye "kuolewa" na mwanamke mwenzie? Hivi haya majitu wana Biblia zao au? Nimeona hiyo habari mitandaoni nikashangaa sana.
 
Huyu mzee huwa simuelewagi kama kweli ni mtumishi wa Mungu... Huenda huyu naye ni 'mpiga deal'...
 
Halafu kuna mstari kwenye biblia unaosisitiza umuombe Mungu akushike mkono katika bonde la mauti ili usiogope, yeye hauamini huu mstari? Huu uoga wa kifo kautoa wapi?
 
Back
Top Bottom