Dereva wa Mo Dewji afunguka, ‘alipokea meseji za vitisho’

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,795
Reaction score
48,057
Dereva wa bilionea Mohamed Dewji ambaye ametekwa na watu wasiojulikana, ameeleza jinsi ambavyo Bosi wake huyo alivyokuwa anaishi.

Akizungumza leo kupitia Clouds Fm, dereva huyo amesema kuwa ni jambo la kawaida kwa mfanyabiashara huyo tajiri kuendesha gari lake mwenyewe kwani alikuwa anaamini ana amani.

“Mo Dewji ni tajiri lakini anaishi maisha fulani hivi kama vile sio tajiri. Yaani alikuwa hana hofu na raia kwa sababu yeye kila mtu anayekutana naye ni kama vile anajuana naye miaka mingi,” alisema.

Dereva huyo ambaye amefanya kazi kwa Mo tangu mwaka 2001 ameeleza kuwa Mo alikuwa anajiamini na hakuwa na uoga dhidi ya raia, lakini aliwahi kumtahadharisha mwaka huu kuwa amekuwa akipokea jumbe za vitisho.

“Kuna kipindi aliniambia, ‘bwana kwa huku tunakoenda inabidi kuwa makini’. Nikamuuliza kwanini, akasema kuna kipindi alikuwa anapata meseji halafu kama za vitisho-vitisho. Ilikuwa kama miezi minne iliyopita,” aliongeza.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mo alitekwa na watu wasiojulikana mapema leo asubuhi katika hoteli ya Colleseum jijini Dar es Salaam.

Polisi wanaendelea na msako na tayari wameshawakamata watu kadhaa wakihusishwa na tukio hilo.

SOURCE: DAR24
 
Tundu Lissu alipokea kichapo cha kumiminiwa risasi za kivita akiwa na dereva wake katikati mwa eneo lenye utitiri wa walinzi wanaolinda masaa 24. Na kabla ya hapo alianza kupokea vitisho na kufuatiliwa kama chambo. Hapo vipi nako?
Lissu angekua na bunduki au mlinzi mwenye bunduki asingeumia vile mkuu
Wale walinzi unaoongelea wewe si ndio walitoa tape za cctv ? Wale sio wa kutegemea sababu huwalipi
Hata Mo unaambiwa gate liliachwa wazi makusudi ndio watekaji wakapitiapo
 
Jaribu kunisoma vizuri utanielewa hapo.
Nilikuwa nataka kukuonyesha tu kuwa, kuwa na ulinzi tu huenda kusingezuia kutekwa kwake ikiwa wahusika ni watu wale wale.... Na kujaribu kupambana nao kwa silaha za moto huenda kungeyamalizia maisha yake pale pale. Mpaka saa sote tunakubali kuwa wale sio majambazi, na huenda pia tutakuja kukubali pia wahusika sio watekaji, bali ni watu wale wale.....

Nini kimemkuta mfanyabiashara Zakaria wa kule Mara. Kama asingewazidi nguvu na ujanja wale watekaji, mpaka leo hadithi ingekuwa ni kuwa ametekwa na majambazi au kikundi cha watu wasiojulina.

Tukio la Lissu ni good case study, hakuna mtu anategemea mhalifu wa kawaida anaweza kufanya shambulio la namna ile katika mazingira yenye ulinzi wa kiwango kile na akatoja salama pasipo kukamatwa mpaka leo hii unless awe well protected na system fulani fulani.
 
Dereva wa bilionea Mohamed Dewji ambaye ametekwa na watu wasiojulikana, ameeleza jinsi ambavyo Bosi wake huyo alivyokuwa anaishi.

Akizungumza leo kupitia Clouds Fm, dereva huyo amesema kuwa ni jambo la kawaida kwa mfanyabiashara huyo tajiri kuendesha gari lake mwenyewe kwani alikuwa anaamini ana amani.

“Mo Dewji ni tajiri lakini anaishi maisha fulani hivi kama vile sio tajiri. Yaani alikuwa hana hofu na raia kwa sababu yeye kila mtu anayekutana naye ni kama vile anajuana naye miaka mingi,” alisema.

Dereva huyo ambaye amefanya kazi kwa Mo tangu mwaka 2001 ameeleza kuwa Mo alikuwa anajiamini na hakuwa na uoga dhidi ya raia, lakini aliwahi kumtahadharisha mwaka huu kuwa amekuwa akipokea jumbe za vitisho.

“Kuna kipindi aliniambia, ‘bwana kwa huku tunakoenda inabidi kuwa makini’. Nikamuuliza kwanini, akasema kuna kipindi alikuwa anapata meseji halafu kama za vitisho-vitisho. Ilikuwa kama miezi minne iliyopita,” aliongeza.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mo alitekwa na watu wasiojulikana mapema leo asubuhi katika hoteli ya Colleseum jijini Dar es Salaam.

Polisi wanaendelea na msako na tayari wameshawakamata watu kadhaa wakihusishwa na tukio hilo.

SOURCE: DAR24
Aiseee kumbe hapa kila mtu ni mpelelezi afu kila mtu anamjua sana MO
 
Tundu Lissu alipokea kichapo cha kumiminiwa risasi za kivita akiwa na dereva wake katikati mwa eneo lenye utitiri wa walinzi wanaolinda masaa 24. Na kabla ya hapo alianza kupokea vitisho na kufuatiliwa kama chambo. Hapo vipi nako?
Muroto alishindwa kabisa kuwakamata waliomjeruhi Lissu. juzi kati hapa alikamata malaya na dada poa ambao silaha walokua nazo ni kondom tu kwenye vipochi. Halafu anauza sura kwa tiivii
 
Blackmail ni kitu kibaya sana. Hizo njemba ziļizomteka kuna kitu zìnataka ķutoka kwa Mo na kama waņgekuwa wanaataka kumuua basi wangemshoot pale pale
Mambosasa huu ni wakati muafaka wakuonyesha kwamba wewe ni mambosasa. Piga kazi kaka tuletee hawa wajinga wanaotaka kuichefua Tanzania
 
Back
Top Bottom