Deo Kisandu: Hakuna chama kisafi Tanzania

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
887
0
Jamaa akiwa katika tuongee startv asubuhi anasema tatizo tanzania sio chama chamapinduzi kinacho leta umaskini tanzania ila tatizo ni viongozi wenyewe, pia amevilaumu vyama vya upinzani kuwa havina viongozi ila vina wanaharakati kwakua hawaja andaliwa kiuongozi, tatizo la watu ni kuwaonea wivu wenye madaraka

source tuongee asubuhi
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
1. Chama bila watu na viongozi hamna kitu!! Chama ni wanachama na viongozi so hapo kaongea ki utu uzima!!!!!
2. Ni kweli na tatizo la wanaoongozwa katika upinzani ni kuwa wanakosoa sana CCM wakati vyama vyao vina matatizo almost the same!!!!
3. Watu hawawaonei wivu ila wanawachukia
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,394
2,000
Huyu Jamaa Atatuharibia Chama Chetu(NCCR-MAGEUZI) UNATENGANISHAJE CCM NA WANACHAMA WAKE??AU KATIBA NA MFUMO WA UTAWALA??
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,771
2,000
Viongozi wa CCM ndiyo CCM yenyewe.Viongozi wa CCM wakishindwa CCM ndio iliyoshindwa.
 

Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,944
1,500
...nadhani hajui anachoongea,ccm maanayake nini kama si watu wake,afukuzwe hapo studio...
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,771
2,000
Jamaa akiwa katika tuongee startv asubuhi anasema tatizo tanzania sio chama chamapinduzi kinacho leta umaskini tanzania ila tatizo ni viongozi wenyewe,pia amevilaumu vyama vya upinzani kuwa havina viongozi ila vina wanaharakati kwakua hawaja andaliwa kiuongozi,tatizo la watu ni kuwaonea wivu wenye madaraka ;source tuongee asubuhi

CHADEMA alikuona hakufai na NCCR nako hakufai sasa hivi anaiona CCM haina tatizo.Si ni bora aende huko anako kuona kunamfaa.
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Kijana hawezi kuwa Mwenyekiti wa CCM taifa, HAKUNA DEMOKRASIA NDANI YA CCM ni rushwa na utemi. Miaka 53 wenyeviti 4, CDM miaka 22 wenyevti 3. Menyekiti wa CCM anagombea na kivuli, Makamu wake etc
 

Jamie Nsuri

Senior Member
Jan 16, 2014
156
0
Kuna half truth na half false. Yapo ambayo yangefanyika sawa uchumi wetu ungekua mbali zaidi. Waliokua madarakani ni CCM. Hata Kingunge anajua haya.
Wakufanya ilikua CCM
Upinzani kuna wakati hata mimi nawaona kama wanaharakati. Sijui tumekosea wapi ila yako mengi.
Jana bungeni walizungumzia mtu kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii Kama fao. Wakati. Wakati kujitoa ni kayakimbia mafao. Mfano wa mafao ni pension ya uzeeni, elimu kwa Watoto, survivors benefit, invalidity benefit, funeral grants etc. Anaejitoa anaishi kesho yake leo no longer eligible for the benefits. Ni fao au kutumia hifadhi vya jamii Kama SACCOS?

THEN. tukijiuliza sera za uchumi za vyama vyetu sioni wakijipambanua utofauti wao na CCM. Hata kijamii sielewi jamii tunayotaka kujenga.
Natambua kukemea ufujaji wa mali za ummah, kutetea haki za binadamu, mazingira, na democrasia.
Ni mambo muhimu lakini hata wanaharakati wangetosha.

Shida nyingine usafi tunao utaka hatuna na hatukuwahi kuwa nao. Maamuzi mengi yanaangalia faida za kisiasa kwanza hata kwa upinzani mwananchi anatumika tu.

False hapo ni jitihada nilizotaja japo hata wanaharakati wangeweza na wanafanya.
HAYA FAIR COMMENT MSIWEKE MISIASA YENU TENA.
 

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
887
0
Jamaa niliwahi kusema mwakani anahamia ccm maongezi yake yanajibainisha;tangu ahame chadema tanga amekua akitetea hoja za ccm
 

TzPride

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
2,601
2,000
Kama viongozi ni wabovu, sasa chama itakuwaje hakina shida?!

Ati upinzani hawana viongozi, ni wanaharakati!!! Hii kauli wanaitumia sana utadhania uanaharakati ni shughuli haramu. Iingie kwenye vichwa maji vya maCCM na ma-pro wao kwamba uanaharakati ni shughuli ya kijamii ambayo ndio hutoa huduma kwa wananchi...sio hayo ya uongozi wa chuo cha magogoni ambapo watu hufundishwa kuwa mafisadi.

Kama mwanaharakiti hawezi kuwa kiongozi mzuri, basi fisadi ataweza kuwa kiongozi bora. Obama alikuwa mwanaharakati na sasa ni kiongozi mzuri akiongoza taifa kubwa zaidi duniani.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,088
2,000
Jamaa akiwa katika tuongee startv asubuhi anasema tatizo tanzania sio chama chamapinduzi kinacho leta umaskini tanzania ila tatizo ni viongozi wenyewe,pia amevilaumu vyama vya upinzani kuwa havina viongozi ila vina wanaharakati kwakua hawaja andaliwa kiuongozi,tatizo la watu ni kuwaonea wivu wenye madaraka ;source tuongee asubuhi

Hayo ndiyo mawazo duni waliyo nayo watanzania wenye sauti, je wale wasiokuwa na sauti watakuwa na mawazo gani?
 

Jamie Nsuri

Senior Member
Jan 16, 2014
156
0
Naweza kusema pia bila upinzani CCM wangekua wamelala usingizi mzito. Wanachokosa upinzani ni kuwa na team imara za watafiti wa sera na kuwaheshimu. Waliopo hawaheshimiki na wanashindwa kabisa kujipambanua kwa sababu uwepo wao ndani ya vyama unategemea utii kwa viongozi wakuu na akiteleza akaonyesha hawafai anaenda na maji.
Pia nidhamu ndogo ya wana siasa upinzani kupenda kujijenga wao badala ya vyama.
 

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
887
0
Tatizo la vijana ni kupandikizana ujinga tukipewa fursa hatuzitumii.

Pia anasema haoni tatizo Ridhiwani,Januari na Godfrey Mgimwa wakiwa wabunge,sumu ya kubebwa ipo vyama vyote.

Pia jamaa amesisitiza kuwa yeye siyo mwanasiasa.

Je wanajamvi huyu kijana mwenzetu mna mwelewa?
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
kwani hata upinzani viti maalumu hali si ni kama hiyo!!!
Ni kweli hakuna kisafi,extent tu
 

Kuntakint

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,772
2,000
Msibaki kulaumu upinzani. Bila upinzani sidhani kama mngepata hata chumvi madukani. Kubali usikubali wapinzani wamesaidia sana hali kuwa ahueni Tanzania. Wapinzani wanapata tabu sana kwani chama tawala ccm hawataki upinzani iwepo, wanachotaka wapinzani wawepo jina kwa ajili ya kuwahadaa nchi za nje. Lakini wapinzani wako katika mazingira magumu sana, ni mtu -------- pekee atakae wabeza wapinzani. Chama ccm kina kila kitu toka jeshi, polisi ingawa hawatakiwi kuwa upande wowote lakini mwenye macho aambiwi tizama. Tizama wapinzani wanavyoonewa, wanapigwa, wanafunguliwa kesi za ajabu. Jiulize inakuwaje katibu mkuu wa ccm anaruhusiwa kuhutubia Tabora lakini wapinzani wanapoomba kuhutubia wanazuuliwa. Jiulize inakuwa Je ccm wanaruhusiwa kuhutubia Mtwara lakini wapinzani wanakatazwa. Nikirudi kwa huyo Kisandu kwanza kamvunjia heshima mwenyekiti wake wa chama na yote hayo ameyaongea ili afukuzwe na inaonekane vyama vya upinzani havina demokrasia. Ccm anayoisifia haina demokrasia hata kidogo ukikorofishana nao kwa mawazo watakuua, kama ni mfanyabiashara unafilisiwa mifano hai ipo. Kwa hiyo huyo Kisandu nccr hapamfai inabidi aondoke hapo amepita tu kwa kazi maalum.
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
KUNA UTOFAUTI MKUBWA KATI YA KIJANA WA CDM ANAPOONGEA NA KIJANA WA CCM,Ushahidi angalia TUONGEE ASUBUHI SAA hii, Mapuri anayokazi. CCM ni hopeless kabisaa. Pikipiki Mjini hongera CDM kwa kijana mwelevu na Poleni CCM kwa zuzuz lenu hilo. JE polisi imeshindwa wajibu wake inasingizia pkpk??? je kuna wezi mawaziri baraza la mawaziri limefutwa??, je kuna polisi majabazi je jeshi la polisi limefutwa???
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Naweza kusema pia bila upinzani CCM wangekua wamelala usingizi mzito. Wanachokosa upinzani ni kuwa na team imara za watafiti wa sera na kuwaheshimu. Waliopo hawaheshimiki na wanashindwa kabisa kujipambanua kwa sababu uwepo wao ndani ya vyama unategemea utii kwa viongozi wakuu na akiteleza akaonyesha hawafai anaenda na maji.
Pia nidhamu ndogo ya wana siasa upinzani kupenda kujijenga wao badala ya vyama.

Kwa nini unashindwa kusema wazi tu kuwa na viongozi ambao hawajasoma ni mzigo kwa pande zote? ????!!!!

Anzia bungeni tu hapo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom