Denti auwawa kwa wizi wa Pera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Denti auwawa kwa wizi wa Pera

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Semilong, Apr 10, 2009.

 1. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wadosi 3...Samily Hassan,Nuzalt Hassan,Hassan Hassan na Faidh Abdulasuri..wakazi wa Kijiji cha Ihamila Ihanga, Tarafa ya Rujewa, wilayani Mbarali wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mwanafunzi wa kidato cha nne, Swaibu Moshi kwa madai ya kumkuta akiiba mapera.

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,alisema hao watuhumiwa wakiwa na mkoko wenye namba T 496 ALF Toyota Land Cruiser, waliwakuta katika shamba lao wanafunzi wawili, Salum Hamis na marehemu Moshi na kuwakamata kisha kuwaingiza katika gari hilo na kuondoka nao.

  Baada ya kuona hivyo, Hamis aliruka kutoka kwenye gari na kukimbia huku watuhumiwa hao wakiondoka na marehemu Moshi.

  Hamis baada ya kuona hivyo, aliomba msaada kwa raia wema ili kurudi kufuatilia alikopelekwa mwenzake. Wakati wakiwa njiani waliona gari hiyo ikisimama ghafla pembeni yao na kushuka watu wawili ambao walitaka wapande gari hiyo ili kumpeleka hospitali marehemu Moshi aliyonekana amelala nyuma ya gari, hata hiyo Hamis na raia mwema huyo walikataa.

  Alielezwa kuwa watuhumiwa hao baada ya kuona wamekataa waliamua kumpeleka marehemu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali na kumkabidhi kwa wauguzi ambao walimlaza.

  Baba mdogo wa marehemu, Bw. Hashim Omari ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Ibara alisema marehemu Moshi, Aprili 5 mwaka huu saa 11 jioni aliondoka kwenda kuangalia mechi ya mpira wa miguu hakuonekana tena mpaka saa 2 usiku alipofika mke marehemu Hassan Mulla aliyekuwa Diwani wa Kata ya Rujewa akiwa na Salum.

  Bw. Omari alisema mama huyo alimpa taarifa kuwa Hamis na mwenzake (marehemu) wamekamatwa wakiiba mapera na kwamba Hamis alikimbia na mwingine alianguka kwenye gari na kuumia na amelazwa hospitali kwa matibabu zaidi.

  Alisema baada ya kusikia hivyo alikwenda hospitali na kukuta wauguzi na kuambiwa mgonjwa wake alikuwa ameshafariki wakati akipelekwa hospitalini hapo. Alikwenda chumba cha maiti ili kuthibitisha na kugundua kuwa alikuwa na majeraha kichwani, utosini, kisogoni, ubavuni na jichoni.

  Alisema Aprili 6 mwaka huu alikwenda hospitali na kuomba mwili wa marehemu ufanyiwe uchunguzi ambapo aliomba madaktari wa Hosptali ya Mbarali wasitumike na kuamuliwa apeletwe daktari kutoka Hospitali ya Rufani ya Mbeya, Dkt. Mbaga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu ambapo iligundulika alikuwa amepasuka utosini na shingo yake kuvunjwa na damu kuvilia na kusema taarifa kamili za uchunguzi za kifo hicho zitatolewa na Jeshi la Polisi.

  Watuhumiwa hao waliachiwa kwa dhamana. Hata hivyo ndugu wa marehmu walikuja juu na kusababisha dhamana ya watuhumiwa hao kufutwa, hivyo kupelekwa Gereza la Ruanda wakisubiri upelelezi wa Polisi.

  wanatuibia, wanatuua, mikopo wanapendelewa wao benki, (polisi, mahakama, viongozi, rais wote wamewaweka mfukoni) hivi TZ itaendelea kuwa ivi mpaka lini???????????
   
 2. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Hii inatisha!! Ubinadamu umetutoka kabisa. Kisa ni pera tu?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Isiwe ni kwa sababu waliofanya kitendo hicho ni wahindi ndio mkaona kuna maonevu,mwizi ni mwizi tu akiwa mweupe au mweusi ,akiiba kuku au ng'ombe ,na kila siku wezi wanauliwa kwa kupora viselula ,kwa kuiba magengeni na huko kwenye mashamba ya watu ndio kabisa maana mtu anaingia gharama ya kusitawisha mimea ,sasa iweje mwengine anapanda na mwengine anavizia kuvuna , hawa wahindi ni wafanya biashara tena biashara zao huwa ni ndogo sana au huanzia na mambo ambayo sisi wengine tunayaona ya kipuuzi ,mhindi anaweza kuanza na biashara ya kuuza ubuyu,kuuza mifuko ya karatasi itokananyo na mifuko ya sementi kusema kweli biashara zao zinaanzia mbali na wanaweza kuziendeleza nakumbuka pale tanga barabara ya nane au kumi kama sikodei alikuwepo fupi ,huyu ni baniani akiuza genge la vitu mfano wa hivyo na hata maembe masala yalikuwa hayakosi kwake ,sasa jamaa amewakuta wezi tena shambani kwake aloo kule marekani wanakuekea na kibao wakikueleza No Trace Passing kwa maana akikukuta basi hata risasi anakulamba nayo ,kosa hapo kwa wahindi hao ni kuwa kijana amepoteza maisha akiwa mikononi mwao sheria lazima ifuate mkondo wake.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160

  Stori zako za nguruwe na vitunguu, sijui kikaruka kikatua ..blah blah , kawasimulie wakezo na wajukuu wako.

  Sisi wazalendo wa taifa hili tunashikwa na uchungu mkubwa kwa kupotewa na nguvukazi ambayo imekuwa mis-managed na watawala wetu dhalimu wakishirikiana na wageni.

  Hata hivyo inshallah mwafaka utapatikana.
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ....I Dont Believe This! Mwiba, Is That You?? Is This really your Contribution to this Saga??
   
 6. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hakuna nguvu kazi ya taifa kwa mwizi kama alivyosema ni bahati mbaya amekufa akiwa mikononi mwao sehemu nyingi tunaona watu wakiiba vitu vidogo wanapigwa na kuu liwa ok

  pamoja hiyo inasikitisha
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  matusi ya nini tena!?
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Dogo usiwashangae watu wanaovaa nguo za aina hiyo huwaga ni urithi kutoka kwa familia nzima ,hivyo usitegemee maneno ya au matamshi ya kiutu.
  Kinachotoka midomoni mwao ndicho kilichomlea hivyo katika siasa za vyama vingi ni lazima watu wa aina hiyo tuwavumilie na tuwaelewe na mapema maana kulifahamu suali ni nusu ya jawabu.Inatakiwa mtu wa aina hiyo umfahamu na mapema na kuendeleza nae mjadala hivyo hivyo.

  Nimesema kuwa trace passing kwa nchi nyengine unauliwa papo kwa papo, watoto wameonekana wakiiba ,wamekamatwa na wamepewa kibano ,sasa ikiwa kibano kimekuwa kikubwa na pengine inasemekana walikuwa wanapelekwa kituoni wakaruka kutoka kwenye gari ,hivyo ukiruka kwenye gari ni lazima utavurugika ikiwa hukuwahi kupitia mgambo na kujua style za kuruka kutoka kwenye gari inayokwenda mbio.

  Nguvu kazi ya Tanzania haitajengwa na wezi maana hawa wasiokuwa wezi tunawaona wanavyogawana mitaji na hazina ya Taifa je wakikulia na tabia za mkono mkono si watagawana mikoa.
   
 9. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hii hamaki mpya dhidi ya vifo vya sheria mkononi imeanza lini? Wezi si tunawakaanga na petroli, au?

  Tumeambiwa tuwaadhibu washutumiwa papo hapo. Ndivyo alivyoasa Waziri Mkuu wetu, ukimshuku muueni dakika hiyo hiyo. Sasa leo tunasumbuliwa na hilo? Au kwa vile safari hii wauaji ni wale wenye asili ya ugeni, Wahindi? Labda na wao wamelowea katika utamaduni wa wenyeji wao, wametopea, wamejifunza, wamekubali aina yetu ya haki. Jadi yetu inasema mshutumiwa wa wizi wa bangili, leso, pochi, kidani, simu, mkufuze, ukimkamata mpige mawe mpaka afariki dunia. Waziri wa fedha au ofisa aliyekabidhiwa kuchunga hela za Taifa benki kuu ukimshuku ametuibia mfukuze, halafu mpe siku yake mahakamani. Mwizi wa pera hana siku mahakamani. Hatutaki kutafuta ukweli kujua kama watoto walifahamu pera liko ndani ya shamba la Mhindi, au mapera wameyakuta yanadondoka ardhini wakajisaidia mawili matatu, au Mhindi huwa anaachia watoto wale mapera siku hiyo akacharuka watoto hawajui hili wala lile. Hapana, utamaduni wetu unasema ua. Ua hapo hapo.

  Utamaduni huo umejengwa kwenye tatizo linalokera wananchi, wanasema ukijaribu kumpeleka huyu mtoto kwa wahusika kutafuta ukweli kuhusu pera hilo basi ataachiwa kituo cha polisi hata kabla hajafika mbali kwenye kwenye mkondo wa sheria. Ndio falsafa ya uhalalishaji mauaji haya. Ni lini umesikia wananchi wamekasirika kuona kibaka kahukumiwa mawe mtaani? Huwezi sikia, tena tunafurahi, tunashiriki. Tunasema mwizi wa embe mpige matofali, akizirahi mchovye kwenye Diesel, ulia mbali. Mwizi wa migodi msikilize kwanza. Mpe ulinzi. Lete watetezi. Mashahidi. Njoo na makaratasi utuonyeshe hujaiba. Makaratasi hayo hayo uliyochonga kuibia. Unaweza kusema huzitaki, huzipendi hizi jadi lakini huwezi kukataa kwamba ni desturi, mazoea, utamaduni wetu.

  [​IMG]

  [​IMG]

   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Isiwe ni kwa sababu waliofanya kitendo hicho ni wahindi ndio mkaona kuna maonevu,mwizi ni mwizi tu............"

  *********************************

  Mwiba:
  Hawa sio Wahindi, ni Waburushi (Baluchis) wa maeneo ya Rujewa ambao wana historia ya kunyanyasa Waafrika tangu zama za zama. Ni kabila moja na kina Rostam, lakini kina Rostam wao wanatoka maeneo ya Nzega/Bukene. Asili yao ni Baluchistan, eneo katika mpaka baina ya Pakistan na Iran.

  Inasemekana hawa wa Rujewa wamehusika sana kutoa ushawishi mkubwa kwa serikali (wakati wa EL) katika kuwaondoa wachungaji Ihefu ili wao watwae maeneo kwa ajili ya kilimo cha mpunga, na kinara wao katika hili ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa mbeya.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hao si wahindi wala mabulushi hao ni WaTanzania maana ukianza kusema ni kutoka Pakistani na Irani utakuwa na wewe mwenyewe ni kutoka Congo ndipo historia inavyosema WaTanganyika wote ni wakuja hakuna mwenye asili ya dongo la hapa ,upo ,hili pande la ardhi tunalojivunia lote lilikuwa ni mbuga za wanyama na ushahidi upo kuwa wanyama walitapakaa hadi katika fukwe ushahidi ambao ungali bado upo ni sehemu ya njia ya ndani kwenda Tanga ukitokea Dar kuna mbuga flani ambayo hadi leo simba anafika hadi kwenye fukwe na wanyama wengine huonekana hapo wakiota jua katika mchanga wa pwani ,hivyo hao nawahisabu ni WaTanzania kama waTanzania wengine kuwagawa ni kosa ,na hata unavyosema kuwa ni wababe ndio wanalingana kabisa na baadhi yetu ,hata viongozi ni wababe au hukusikia yule aliewatia walimu bakora na kuwacharaza hadharani au hukusikia yule aliemzabua kofi Ali Hassan Mwinyi ,hivyo kama ni ubabe ndivyo tunavyoishi ,wasionewe kutokana na rangi yao na kuwashambulia eti ni wa kutoka PakistaniIrani ,wanatunyanyasa ndani ya nchi yetu itakuwa hatuwatendei haki makosa hayo ya kuwaona wengine ni wageni ndio yaliyoizamisha Zimbabwe au umeshasahau ?
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Hao si wahindi wala mabulushi hao ni WaTanzania maana ukianza kusema ni kutoka Pakistani na Irani utakuwa na wewe mwenyewe ni kutoka Congo ndipo historia inavyosema WaTanganyika wote ni wakuja hakuna mwenye asili ya dongo la hapa ,upo ,hili pande la ardhi tunalojivunia lote lilikuwa ni mbuga za wanyama na ushahidi upo kuwa wanyama walitapakaa hadi katika fukwe ushahidi ambao ungali bado upo ni sehemu ya njia ya ndani kwenda Tanga ukitokea Dar kuna mbuga flani ambayo hadi leo simba anafika hadi kwenye fukwe na wanyama wengine huonekana hapo wakiota jua katika mchanga wa pwani ,hivyo hao nawahisabu ni WaTanzania kama waTanzania wengine kuwagawa ni kosa ,na hata unavyosema kuwa ni wababe ndio wanalingana kabisa na baadhi yetu ,hata viongozi ni wababe au hukusikia yule aliewatia walimu bakora na kuwacharaza hadharani au hukusikia yule aliemzabua kofi Ali Hassan Mwinyi ,hivyo kama ni ubabe ndivyo tunavyoishi ,wasionewe kutokana na rangi yao na kuwashambulia eti ni wa kutoka PakistaniIrani ,wanatunyanyasa ndani ya nchi yetu itakuwa hatuwatendei haki makosa hayo ya kuwaona wengine ni wageni ndio yaliyoizamisha Zimbabwe au umeshasahau ?"

  ***********************

  MWIBA: Kama ni hivyo kwa nini Waarabu waliokuwa wanatawala Z'bar walipinduliwa? Si wangeachwa tu kwani walikuwa ni 'wakuja' tu kama vile wale watu weusi waliowapindua?
   
 13. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ulaya ukiiba dukani unaambiwa stop stop stop hamna mtu anayekupiga na kama ni mara yako ya kwanza unapewa caution mpaka urudie sana ndio unafungwa...
  bernard mardoff angekuwa TZ wala asingefungwa tena yeye ndie angekuwa tishio.

  utu ni neno kubwa sana......
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ni Kweli kwa Tanzania,USA na nchi za ulaya, lakini kuna nchi nyingi huko na Asia na Arabuni bado hujawa raia kama hufananii na ngozi yao hata ujikombe vipi.
  Na ukijifanya kijogoo kwa Binti zao mawe, wakati wao huku kwetu wanawapanga foleni binti zetu.
   
  Last edited: Apr 12, 2009
 15. p

  powermabula New Member

  #15
  Apr 12, 2009
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maneno mengi ni yani nini? Akiwa mburushi, mwarabu, msangu au mzungu. Mwizi ni mwizi. Na shangaa chuki ni yanini ardhi Tanzania iko tupu kila mahali. Watu wenyeji wa Rujewa wengi wao ni wavivu tuu wanapenda kunywa ulanzi na kukaa kwenye magenge na kuteta. Wanawalaumu maburushi . Maburushi ndio walichimba mfereji unaotoka mto mbarali mpaka kwenye mashamba yao. Ndio baadaye mwingereza na mchina akaona mfano huo ndio akafatilisha. Leo bila maburushi Rujewa ingekuwa ghost town. Mburushi ni mwihisani mkubwa kwa wazalendo wa Ibara.Mimi ni mmoja wapo sitasahau fadhila za maburushi. Wacheni ubaguzi wa rangi. Maburushi kama sisi wamekaa na sisi wakati wa dhiki na tukae nao wakati wa faraja. Acheni kuhukumu kabla kesi haijafika mbele ya sheria. Yeye marehemu angelingoja mpaka angefikishwa kwenye mikono ya sheria. Na yule aliyoruka akamatwe atiwe kizimbani. Yeye ndiye aliyetoa mfano mbaya. Basi wacheni chuki. Maburushi ni watanzania. Ile mambo ya Iran au Pakistan wacheni. Wako wengine watu wametoka nchi zingine za Afrika mbona hawatajwi wametoka Angola au Zimbabwe. Maendeleo yanakuja sio kwa kulaumiana. Imepitwa na wakati. Tuangalie nchi kama marekani haikujali Obama baba yake ni kutoka Kenya au wapi na wamemchagua. Tukitaka maendeleo tuache mambo ya rangi, asili, kabila, au dini. Tumuombee marehemu mungu amlaze mahali pema -Amen. Justice will prevail.
   
 16. p

  powermabula New Member

  #16
  Apr 12, 2009
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamekwibia nini? Kama wao wangekuja kwenye shamba lako kuiba ungeliwaachia wamalize kila kitu? .Mikopo kila mwananchi anapewa akiwa na uwezo wa kulipa.Usitoe malamiko yasio na busara. Wewe usilaumu ,chapa kazi. Utaona wapi utafika. Mtu anayetoa lawama hovyo anakuwa ameifunga akili yake kimaendeleo.
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sikuelewi
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160

  Matusi yepi hayo ndg?. Au kitu kischokufurahisha rohoni ndio unakiona ni matusi?
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sheria za nchi zinasema mwizi akikamatwa afanyweje..nataka ujibu hili swali ili kila mtu anayesoma hii thread ajue ulivyo mbumbumbu mzungu wa reli.

  Haya ukumbi ni wako.
   
 20. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Na bado Wameanza kurudisha hadi majina ya Mitaa... Mtaa uliokuwa waitwa Kisutu sasa waitwa Pramukh ... Street watarudisha kila kitu... Huo wa A.H.Mwinyi utaitwa Mahatma Gandhi siku si nyingi...
   
Loading...