Unamaanisha nini unaposema Uchumi unazidi kudorola? Uchumi wetu unakuwa kwa 7% na sisi ni wa Pili wa ukuaji kasi wa uchumi Afrika baada ya Ivory Coast na hii kulingana na UN, WB,IMF sasa huko kudorola unamaanisha nini labda?
Wajua Deni la Taifa linaanzia wapi?.
Deni la Taifa (National Debt) inatokana na upungufu unaotokea ktk ulari wa malipo ya kimataifa (Balance of Payment). Ni matokeo ya kuwa na total variables za imports kuzidi Exports. Inapotokea nchi inaagiza na kuruhusu bidhaa toka nchi zingine kuliko kupeleka na kuuza zaidi ughaibuni ndipo inapoonekana kuwa taifa lina upungufu ktk Balance of Payment.
Sasa upungufu (deficit) hiyo lazima iondolewe. Sasa ili kuondoa huo upungufu Akaunti ya Taifa kule Word Bank (Foreign Reserves Account) inalazimika kuwa credited kwa kiasi cha tofauti iliyopo baina ya Exports na Imports ili kuondoa tofauti hiyo, kiuchumi huu mchakato waitwa Financing the deficit in the Balance of Payment.
Kiasi kilichotumika kudhamini tofauti hiyo kinaingizwa kwenye Deni la Taifa ndipo linapotokea ongezeko la deni letu.
Sasa financing deficit inaambatana na kitu tunaita Depreciation au Devaluation of domestic currency.
Umeandika WB, IMF na UN ndo walisema Tz ina growth ya uchumi kwa 7%, lakini lazima "ufahamu kuwa ili bepari akusifie lazima akuibie au akukopeshe zaidi"
.... juzi haohao World Bank walosema kuna kukua uchumi kwa kasi ndio wanasema deni la taifa limeongezeka.
Sasa vipo viashiria vya uchumi wa Taifa kukua. Kwanza uimara wa sarafu (Domestic currency) ukiilinganisha na Dola. Sarafu ya Tanzania imekuwa duni kwa muda mrefu $1=tshs 2180.
Sasa cha kujiuliza ni je sarafu yetu imepanda thamani?? jibu ni HAPANA
Pili ni kiasi cha bidhaa za viwanda vya Tanzania zinazouzwa ktk soko la nje (Exports) kuzidi bidhaa zinazonunuliwa toka nje ya nchi na kuingizwa Tazania. Hapo tunagundua kuwa nchi ina uzalishaji mkubwa hivyo uchumi wake unakua
(Ni kwa kuzingatia ziada ya tulichouza tofauti na tulichonunua).
Tatu BOT na Word Bank zikiprove Revaluation au Appreciation, pale thamani ya pesa yetu itakapoongezeka mathalani toka $1=2180tshs hadi $1=1500tshs au 1600 ndipo itaashiria kukua uchumi.
Ni vitu vigumu na vya kitaalam kama kidogo Elimu ipo chini lakini vinaeleweka.
Sasa ili kuwe na kukua kiuchumi tunahitaji kuanzisha viwanda, ambavyo vitazalisha bidhaa kubwa za kuingia kwenye ushindani wa soko la kimataifa. Tuone employments, tuone diversities za mapato chini ya TRA, wenyewe tutagundua.