Deni la taifa lafikia trillion 40

Gmark

Senior Member
Nov 6, 2015
138
30
Hili ndilo deni linalotukabili, ni deni lilioongezeka mara nne (4) zaidi ukilinganisha na hali ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

Nadhani magufuli hana choice Bali kuendesha nchi kadri utashi wake wa kizalendo utakavyomwongoza. Kama hatafunga boot ataondoka na deni likiwa limeongezeka tena , hapo hatakuwa na distinction hata aweza kujiona kama hakukuwa na maana ya kuwa kiongozi.

Tunamuombea kwa Mungu ampe sura na moyo wa simba
 
Huyo aliyeiingiza nchi kwenye madeni hivo su aulizwe hezo hela zimefanya kazi gani?
 
Tusije kuwa kama Ugiriki kiuchumi ambao deni lao hali lipiki kiasi kwamba nchi nzima imebidi kubinafsishwa lakini bila mafanikio.Nina mashaka sana na future ya taifa letu halafu ikizingatiwa kwamba shilingi yetu ni dhaifu dhidi ya dola ya marekani.Shilingi ikishuka thamani na deni nalo lina ongezeka.
 
Mbona husemi huyo kibaka lowassa angepata wapi pesa kusomesha elimu bure kama si mikopo na kuuza mali za nchi
 
Nyerere aliwahi mshauri Marehemu Kabila rais wa DRC/Zaire kuwa asikubali kulipa madeni yaliyokopwa kipumbavu na kwa anasa za Mabutu. Nasi tz madeni yaliyosababishwa kipuuzi na mkwere bili yake ipelekwe msoga.

mimi nafikiri kuna haja ya kupeleka mswada bungeni kufuta pensheni zote za rais yeyote atakae itia hasara nchi hii itasaidia sana kuendelea kutotumia kodi zetu kumtunza mtu alieliletea hasara taifa
 
haya maposho ya wabunge yanazidisha matumizi mabaya ya pesa tu afu kuna wadau hawalipi kodi kabisa ndo wanaturudisha nyuma na tz yetu
 
kama vipi hii nchi iuzwe tu ili tulipe madeni
maana nasikia kuna mahali vipande vya nchi vishauzwa
 
mimi nafikiri kuna haja ya kupeleka mswada bungeni kufuta pensheni zote za rais yeyote atakae itia hasara nchi hii itasaidia sana kuendelea kutotumia kodi zetu kumtunza mtu alieliletea hasara taifa

Nadhani tuwakamue wabunge maana wanakiherehere cha kujifanya wako pamoja nasi tufute posho ya makalio,mashangingi na utumbo wa mil 250 kama mafao yao tuone kama deni halitaisha na wakatukopa sisi
 
Hii haikubaliki mtanzania mwenzetu anatunyonya harafu anaenda zake kupumzika Msoga. JPM tunamuomba asione haya kufirisi watu wa aina hii. Laana iko juu ya hili taifa.
 
Nadhani tuwakamue wabunge maana wanakiherehere cha kujifanya wako pamoja nasi tufute posho ya makalio,mashangingi na utumbo wa mil 250 kama mafao yao tuone kama deni halitaisha na wakatukopa sisi

ni kweli kabisa tukifanya hivyo hata bungeni wataenda wazalendo tu sio kama sasa bunge limejaa wapigaji tu
 
Back
Top Bottom