TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,533
- 28,506
1. Rais Putin mbali na kuungwa mkono na chama chake, uchaguzi wa mwaka huu anagombea kama mgombea binafsi.
2. Mke na mshauri wa Mufti wa Russia(Dagestan) na mwanahabari aliyefanikiwa pia mkuu wa Kampuni ya Habari za Kiislamu, Dada Aina Gamzatova amekubaliwa kugombea urais wa Russia akikamilisha kupata saini laki tatu kutoka Russia nzima.
3. Wagombea urais wanaotokana na vyama vyenye uwakilishi bungeni hawalazimiki kutafuta saini.
4. Wale ambao (wagombea urais) wanaoungwa mkono na vyama visivyo na uwakilishi bungeni ndiyo wanalazimika kupata saini laki moja.
5.Mwanadada maarufu na mkuu wa bodi ya uhariri wa jarida la wanamitindo la L'Officiel na mjamaa(socialite), Ksenia Sobchak, amejiunga kwenye mbio za kupata urais wa Urusi.
6. Mwendesha mtambo wa kunyanyua vitu vizito (crane), mwana dada Natalya Lisitsina, anayewakilisha chama cha All-Russian United Labour Front ajaachwa nyuma kwenye mbio hizi za kupata urais wa Russia.
7. Mpaka sasa Mkuu wa tume ya uchaguzi , Urusi, ndugu Ella Pamfilova anasema vyama vya siasa 21 nchini humo na wagombea binafsi amabo ni wanasiasa na wanaharakati wapatao thelathini(30) wametangaza hadharani kuwa wana nia ya kugombea urais wa mwaka huu.
Uchaguzi wa urais nchini Russia utafanyika 18/03/2018.
Taarifa hizi Imechukuliwa kutoka>>>Prominent Muslim joins list of Putin's female rivals for 2018 election
====
Nimefurahishwa na kitendo cha Tume ya uchaguzi kuruhusu wagombea binafsi kuwa wengi. Ndiyo uhuru wa kutoa maoni huo.