Demographics | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demographics

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by X-PASTER, Jun 24, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=6-3X5hIFXYU"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
   
 2. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,536
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Bwana filamu hii ni kijinga mno. Namba zake hazilingani na takwimu halisi. Mfano: Filamu inasema "25% of the population are Muslim in Belgium". Wikipedia: "It is estimated that between 3 to 4% of the Belgian population is [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Islam_by_country"]Muslim[/ame] (98% [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Sunni"]Sunni[/ame]) (350 000 to 400 000 people)"; katika makala hii unapata pia chanzo cha takwimu kinyume cha filamu. Inaonekana filamu imetengenezwa na watu kutoka Marekani wasio na habari. Sijui kama wanataka kutisha watu au nini lakini namba si sawa. Pia wanatumia uwongo wa moja kwa moja.

  Nakaa Ujerumani najua majadiliano juu ya uhamiaji na watu kuja hapa si kweli ya kwamba kuna utabiri wa serikali ya Ujerumani ya kwamba nchi inaelekea kuwa nchi ya Kiislamu. Hii si kosa ni uwongo mtupu-.

  Bwana kwa nini unatupa takataka ya aina hii hapa? Intaneti inajaa ndoto, masimulizi, uwongo na kila aina ya maajabu. Kabla ya kuweka kitu hapa naomba ujitahidi kuhakikisha ukweli wake.

  Hasa naomba tusiweke filamu hapa badala ya kujitahidi kuandika kitu chenye maana. Yaani watu wengi hasa wenzetu huko Afrika hawana intaneti ya haraka. Ukifikiri filamu inasaidia basi weka kiungo chake lakini menginevyo eleza unachotaka kusema kwa maneno yako mwenyewe - au nyamaza.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pole sana kama limekugusa na kukuumiza kwa njia moja ama lingine.
   
 4. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu,
  Maelezo yako hayana maana yeyote kwani hujaleta hoja mbadala wa yale tuliyoyaona katika hiyo clip.
  Kila mtu ana uhuru wa kuweka jambo lolote ili mradi tu haliendani kinyume na rules za JF.
   
 5. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,536
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Nimetaja namba halisi ya nchi moja (Ubelgiji - kinyume cha madai ya filamu) na kutaja uwongo moja (kuhusu Ujerumani) nikauliza kwa nini tunapewa filamu bovu kama hii.
  Hapa mwekaji anaweza kuongeza maelezo yake. Je alimaanisha nini?

  Ni kweli ya kwamba hata filamu baya inaweza kutufundisha kitu. Pia habari za uhamiaji wa Waislamu katika bara la Ulaya ni kichwa kinachofaa kabisa kujadiliwa. Ila tu filamu hii ni bovu kabisa haina maana na hapa mwekaji anatakiwa kueleza anachomaanisha.

  Nimetoa pia hoja ya kwamba sipendezwi na filamu pekee kwa sababu watu wengi hasa Afrika hawawezi kuangalia filamu kutokana na hali duni ya mawasiliano.
   
 6. BabaBabuu

  BabaBabuu Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kwa kweli nakuunga mkono. tunaomba (wawili) majibu tafadhari maana hali kama hii ikiachwa kila mtu kuweka apendacho hata kama JF rules hazimkatazi lakini zinakuwa na upotofu, sio swala zuri. tutakuwa tunarudi kulekule kwenye magazeti ya shigongo ambayo ingawa hayavunji sheria za nchi (hayafungiwi) lakini yameachwa na yanaharibu watoto na wamama wa nyumbani (ofcourse na baadhi ya wanaume)
  pili huyu bwana aliyetoa mada anaonekana ni mfuata dini mzuri (nimemuona mara nyingi kule kwenye forum ya dini, mwingine ninayemjua ni maxshimba), si vizuri kutaja au kusema uwongo (refer hapo juu kwenye red highlight). asante
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Imewagusa wengi basi...!
   
Loading...