Dell inspiron 1501 inawaka ila haidisplay kitu

Dell inspiron 1501 inawaka ila haidisplay kitu

Hakikwanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2010
Posts
4,055
Reaction score
1,024
Jamani naombeni msaada nina hiyo dell inawaka kwa maana ya kuonyesha mwanga kwenye LED ya power lakini haionyeshi kitu. Nimejaribu kubadili ram na kuunga kwenye monitor ya nje lakini wapi.
 
Jamani naombeni msaada nina hiyo dell inawaka kwa maana ya kuonyesha mwanga kwenye LED ya power lakini haionyeshi kitu. Nimejaribu kubadili ram na kuunga kwenye monitor ya nje lakini wapi.

Kama si mtaalamu usipende kujaribu utakuja haribu laptop au upoteze data.Kuna watu wamesomeas hiyo kitu nenda uchangie kipato chao.Huo ni ushauri.
Msaada wangu kwako:
Kuna vitu vingi vinachangia hiyo kitu ila kuna vitu nataka kujua kutoka kwako
1.Ukiwasha screen haionyeshi kitu chochote hata kwa mbali ?angalia kwa makini kama ni total black screen au kuna vitu vinaonekana kwa mbali.Mfano nembo ya microsoft wakati inaload.
2.Je operating system inaload completely,computer ikiwa inawaka uwa kuna kimlio cha kuonyesha imefanya test zote za hardware,je kuna mlio wowote unaosikia?
Kabla ya kunijibu hayo hapo juu jaribu
1.iwashe ukiwa umetoa battery iwe kwenye umeme tu
2.Toa RAM zote iwashe uone je itakupa mlio wa RAM kutokuwepo?Ikikupa fine isipokupa maana yake operating system haiload completely(POST haifanyiki).
Fanya one at a time,then leta mrejesho nyuma.
 
kuna port moja ya ram haipo sawa either imeshort circuit..toa ram zote kisha weka moja kwanza then washa ikigoma change port au ram mpaka utajua ni port au ram ipi ina shida....nishakumbana na ishu hii zaidi ya mara 5 kwa pc tofauti tofauti hasa dell na hp.
 
Hiyo ni NVIDIA mkuu, nenda kwa fund yeyote mambie aiheat nvidia au display, au vga. Haichukui hata dk 5.
 
Back
Top Bottom