Degree ya sasa imechuja kulinganisha na miaka ya nyuma

Mtoto mdogo unajua nini wewe ! Mimi nimesoma na watu wameoa darasa la kwanza. Mtu yuko 25 yrs. Na nimemaliza darasa la saba na watu wapo 30's !
Kwahiyo wewe hiyo unaona ni sawa??

Akili za kunguru hizi!
 
Hata siku hizi magari yamekuwa ya kawaida sana.. Zamani kumiliki gari ulionekana mtu fulani tajir sana..ila siku hizi watu wengi wana magari....!!
 
Degree haijachuja kwa upande wangu ila mazingira yamebadilika..
kwa upande wa idadi ya watu wanaosoma elimu ya juu wamekuwa ni wengi mfano leo hii zaidi ya wanafunzi elfu 40 wamejiunga na masomo kwa mwaka 2017/2018.. ukilinganisha na miaka ya nyuma walikua wanafunzi elfu mbili au tatu unakuta ndo wanamaliza degree so wasomi walikua wachache ndo mana ilikua ukisoma unaonekana ni msomi kweli kweli kutokana na uhaba wa wasomi..
pili kukua kwa teknolojia na kuongezeka kwa dhana za elimu hivyo kila mtu amepata nafasi ya kwenda shule.. ingawa kwa upande mwingine kuna baadhi ya wanafunzi wa sikuizi wamekosa ubunifu na hawapendi kujisomea vitabu na kujua vitu...
 
siku hizi hata wapumbavu wana degree, ninaishi na jamaa hapa kamaliza medical doctor degree nchini Russia lakini kutwa nzima kuongelea wanawake na pumba nyingine. ........hana lolote hana productive idea ya aina yoyote
 
Mimi huwa napenda kuwaambia vijana wajiangalie wao zaidi na sio jamii au mitaa inawachukulia vipi..

Umemaliza chuo umepata shahada yako, jiangalie wewe zaidi, hiyo shahada imepanua vipi fikra zako na uelewa wako katika jamii?

Mara nyingi wanaokuwa na hadithi hizi za shahada kupoteza mvuto ni wale ambao hata chuo walishindwa kufika!

Ili uwe mtu mkamilifu kuna wakati ni lazima uyape kisogo maoni ya wengine na ujiangalie wewe zaidi, walioshindwa wana maneno mengi!
Yaaaa wewe upo sahihi..
Maneno ya walioshindwa na wenye ghadhabu za kushindwa kwao huwa yanawaangukia wasio na hatia kwa kujifariji kwa yalioyopita.
Sioni umuhimu wa kupiga vujembe badala yake Wanatakiwa kutoa solutions au suggestions za nini kifanyike na kwa watu gani.?
Kwani mfano thamani ya gari ilivyokua zamani ni sawa na sasa. Dunia inabadilika hakuna umuhimu wa kurudi kwa wakoloni.
 
Naomba kujua miaka ya nyuma ina umbile gani? Na nyie mliosoma miaka hio mmegundua nini au mmeifikisha nchi wapi? kama hamna jibu basi give us chance we move our world alone!
 
Yaaaa wewe upo sahihi..
Maneno ya walioshindwa na wenye ghadhabu za kushindwa kwao huwa yanawaangukia wasio na hatia kwa kujifariji kwa yalioyopita.
Sioni umuhimu wa kupiga vijembe badala yake Wanatakiwa kutoa solutions au suggestions za nini kifanyike na kwa watu gani.?
Kwani mfano thamani ya gari ilivyokua zamani ni sawa na sasa.? Dunia inabadilika hakuna umuhimu wa kurudi kwa nyuma.
 
wadau "degree ya sasa" ni mtandao wa buzz umerudi kwa jina jingine au ufafanuzi please....mi sijaelewa
 
Nadhani kuna tatizo katika mfumo wa elimu. Licha ya kuwa kwa sasa techonlojia inawezesha kujifunza mambo mengi ila bado vijana tuna tatizo katika kufahamu vitu. Yaani kwa mfano rahisi ni kuwa kijana aliyemaliza chuo kikuu hawezi kusimama na wale wazee walioishia standard 8 wakati huo wakitumia mitaala ya Cambridge. Vyuo vilifunguliwa vingi na ili kuvijaza wakapokea mpaka wanafunzi ambao hawakuwa na uwezo mzuri katika hilo. Zamani waliopata nafasi za A-level na chuo walikuwa kweli wapo poa kichwani, sasa ni kufaulishwa tu ili nafasi zijae. Kuna vijana wa vyuo walikuwa wanashiriki mashindano ya Airtel Africa, Tz tulitia aibu sana, utafikiri tulikuwa tunapeleka watoto wa darasa la pili kumbe ni finalists.
 
sahihi maana zamani mtu anayejoin university anakua na uwezo usio tetereka ila kwa sasa chuo kumejawa na vilaza tu wa kuunga unga vikozi unadhan kutakua na kitu hapo
Hii si 7bu ya msingi ila kwakuwa ni mawazo yako ni sawa...
 
Degree inanisaidia kuyajua mazingira yangu kujijua mwenyewe kwenda sawa na teknolojia na mazingira yangu kujifanyia maumuzi ,kutatua shida zangu binafsi na wengine.
.Imenipa uwezo wa kujiamini na umiliki wa mazingira yangu.
 
Hahahahaah.. kweli kabisa kwasasa msomi ni mwenye pesa, huwezi ukajiita msomi halafu huna hata 100
Kusoma sana siyo ishu siku hizi na wala siyo kazi. Kazi ni kuigeuza elimu uliyoipata kuwa pesa.

Uwezo wa kugeuza elimu kuwa hela unatofautiana baina ya mtu na mtu.

Unaweza ukawa na elimu ya darasa ndogo tu (darasa la 7) lakini ukawa na uwezo mkubwa wa kuigeuza kuwa hela.

Pia unaweza ukawa na elimu kubwa sana (na vyeti lukuki hadi ukiitwa interview unabeba kwenye tolori) lakini ukawa na uwezo mdogo wa kuigeuza kuwa hela.

Kifupi ni kwamba, ukisoma sana unapishana na hela, ukitaka kujua hilo angalia mtaani kwenu walio na pesa wana elimu kiasi gani, fuatilia pia hata matajari wakubwa dunia kama akina Bill Gates hawana elimu kubwa kihivo.

Nafikiri nimesomeka...
 
Research Waulize wenye certifacte au dip walioko Kazini
Then na wenye degree waliopo mtaan then uje Na majib
 
Back
Top Bottom