Degree ya sasa imechuja kulinganisha na miaka ya nyuma

kevin strootman

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
1,069
1,716
Jamani hivi mnaionaje degeree ya miaka hii??

Mimi naona kama imechuja sana haina makali kama miaka ya nyuma, uzito wa degree ya sasa inavyochukuliwa mtaani ni sawa na uzito wa anaehitimu form six miaka ya nyuma

Nyie mnaonaje wadau??
 
sahihi maana zamani mtu anayejoin university anakua na uwezo usio tetereka ila kwa sasa chuo kumejawa na vilaza tu wa kuunga unga vikozi unadhan kutakua na kitu hapo
 
Zamani degree likuwa ni ajira, wasomi wachache, teknolojia duni. Ukisoma mkoa mzima unakujua chuo kikuu kimoja.

Leo watu ni wengi teknolojia ni pana, mwenye degree anajua theory zaidi na darasa la saba anafanya practical zaidi.

Wasomi wengi, vyuo vingi, ajira hakuna. Elimu imeimarika sana tatizo huwezi kusoma ukajulikana hata kijijini maana kila mtu ni knowledgeable.

Msomi pekee anayejulikana leo ni mwanasiasa au tajiri design ya Bhareksa.
 
sahihi maana zamani mtu anayejoin university anakua na uwezo usio tetereka ila kwa sasa chuo kumejawa na vilaza tu wa kuunga unga vikozi unadhan kutakua na kitu hapo

Hivyo vikozi ndio vinaungwaje mkuu!! ?
 
Zamani degree likuwa ni ajira, wasomi wachache, teknolojia duni. Ukisoma mkoa mzima unakujua chuo kikuu kimoja. Leo watu ni wengi teknolojia ni pana, mwenye degree anajua theory zaidi na darasa la saba anafanya practical zaidi. Wasomi wengi, vyuo vingi, ajira hakuna. Elimu imeimarika sana tatizo huwezi kusoma ukajulikana hata kijijini maana kila mtu ni knowledgeable.

Msomi pekee anayejulikana leo ni mwanasiasa au tajiri design ya Bhareksa.
Hahahahaah.. kweli kabisa kwasasa msomi ni mwenye pesa, huwezi ukajiita msomi halafu huna hata 100
 
Mimi huwa napenda kuwaambia vijana wajiangalie wao zaidi na sio jamii au mitaa inawachukulia vipi..

Umemaliza chuo umepata shahada yako, jiangalie wewe zaidi, hiyo shahada imepanua vipi fikra zako na uelewa wako katika jamii?

Mara nyingi wanaokuwa na hadithi hizi za shahada kupoteza mvuto ni wale ambao hata chuo walishindwa kufika!

Ili uwe mtu mkamilifu kuna wakati ni lazima uyape kisogo maoni ya wengine na ujiangalie wewe zaidi, walioshindwa wana maneno mengi!
 
Degree ipi ya zamani ina nguvu ya hawa wasomi wetu wa zamani vigeu geu : Lipumba, Msando, Prof Mkumbo and the likes
 
Mimi huwa napenda kuwaambia vijana wajiangalie wao zaidi na sio jamii au mitaa inawachukulia vipi..

Umemaliza chuo umepata shahada yako, jiangalie wewe zaidi, hiyo shahada imepanua vipi fikra zako na uelewa wako katika jamii?

Mara nyingi wanaokuwa na hadithi hizi za shahada kupoteza mvuto ni wale ambao hata chuo walishindwa kufika!

Ili uwe mtu mkamilifu kuna wakati ni lazima uyape kisogo maoni ya wengine na ujiangalie wewe zaidi, walioshindwa wana maneno mengi!
Mkuu umenena the truth
 
Ni kweli hizi hadithi wanazozileta wanakua wengiwao hawajaweza kupata degree, na wanakua na kiburi kuleta mada kama hizi maana unakuta kiuchumi wako vizuri zaidi ya wenye degree na kuendelea.
 
Back
Top Bottom