Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,262
- 2,191
Kwanza kabisa niwapongeze "deep state" kwa kazi nzito na iliyotukuka mliyoifanya tangu Tanzania ipate uhuru hadi leo, mumekuwa muhimili muhimu kuhakikisha Tanzania inavuka salama katika nyakati zote ngumu, huku mukihakikisha kuwa amani ya nchi haichezewi wala kutiwa doa na mtu yeyote.
Kijani hii imetawala tangu tupate uhuru hadi leo ni miaka 60 sasa ,Ila ni dhahiri shahiri imeshindwa kutuvusha kama nchi kutoka kwenye lindi la umasikini, rushwa n.k, katika miaka 60 ya uhuru Tanzania bado afya, umeme, maji, elimu, miundombinu, yamekuwa matatizo yasiyo tibika kama cancer.
Ni wazi kwamba "elites" wa chama hichi cha kijani mawazo yao yamegota na sera zao zimekosa vision kabisa na zimepitwa na wakati, taifa halieleweki linaelekea wapi, hivyo hawawezi kutuvusha tena hapa, ni wamefika mwisho kisera, kifikra, kimkakati na kimbinu.
"Deep state" ni wakati wenu mwingine sasa kuandaa chama kingine kimkakati ili kushika dola, chama ambacho kitakuja na sera mpya, hali mpya na vision mpya ya kuliongoza taifa letu, chama ambacho kitatufanya kutoka hapa tulipo gota na kwenda kule watanzania wengi wanapokuota.
Najua mumejitahidi sana kuandaa na bado mnaendelea kuwaandaa baadhi ya viongozi kwenye chama cha kijani na nchi kwa ujumla kwa nia yenu nzuri tu ya kulivusha taifa ila wamewaangusha kutokana na sera mbovu za chama cha kijani, hivyo siyo vibaya sasa tujaribu na chama kingine tuone kitatufikisha wapi, kwani sera za chama cha kijani zimeshindwa kabisa kutuvusha.
Watanzania ni ngumu sana kujichukulia sheria mkononi kutokana na historia ya nchi hii, hivyo ni ngumu sana watanzania kuandamana au kufanya vurugu wakidai haki yao ya mageuzi kama nchi zingine, kwani nchi hii, haijawahi kuwa na migogoro ya ndani, kwahiyo hata wenzetu kupandikiza mamluku Tanzania kuchochea harakati za mabadiliko ni ngumu sana.
"Deep state" mumehepusha mengi na kufanya makubwa na mazuri zaidi, hivyo naamini nyinyi ndiyo watu wa kwanza ambao mnaweza kuleta "transformation" katika taifa hili na mkihamua kwanza, basi na watanzania watafuata.
Katiba mpya na iliyo bora ni muhimu sana na kupitia katiba mpya , mnaweza sasa kuandaa chama kingine kwa ajili ya kuliongoza taifa hili, kwani kwa sasa hamna chama chenye ubavu wa kuishinda kijani iliyo ota mizizi kila sehemu, lakini naamini mkiamua itawezekana kwani hakuna linaloshindikana mbele yenu.
Tambueni ya kwamba kwa "nature" ya taifa letu ni ngumu sana wananchi kudai mageuzi ya kiutawala kwa nyakati hizi hata wapitie katika kipindi kigumu kiasi gani, Ila nyinyi mkihamua kuanza kuleta hayo mageuzi hata wananchi watafuata pia, kwahiyo ni vyema mkaandaa chama kingine na kuwagroom viongozi wengine wapya kwa ajili ya kushika dola kwa wakati ujao, ili tuone kama tutavuka hapa ilipotufikisha kijani.
Kwa sasa si KIJANI wanaoweza kutufikisha pale tunapopakusudia kama taifa kwani wameishiwa na wamefika mwisho kifikra, bali ni nyinyi tu "deep state" wenye maamuzi ya juu zaidi yaliyobeba mustakabali na dira ya taifa letu.