Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Tulipokuwa tunapigania uhuru kutoka kwa wakoloni kulikuwa na mambo yetu ya msingi tuliyotaka sisi tuyapate.
Waasisi na wapigania uhuru wa Taifa letu walitaka uhuru (freedom) au self-determination(Yaani watu na taifa lao kwa ujumla wawe na haki ya kuunda serikali au utawala wao binafsi ) unaotokana na matakwa ya watu wake bila msukumo wowote wa nje au wa mtu yeyote.
Tulitaka tuwe huru kama kujiamulia masuala yetu binafsi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii hata kitamaduni bila kuingiliwa na mtu.
Tulitaka tuwe na utawala au serikali itakayoheshimu katiba ya nchi na kuweka wananchi katika dhima ya kila jambo,tulitaka serikali inayojali maendeleo ya watu (People centered development) na sio vitu kama mkoloni alivyokuwa anafanya.
Hatukuhitaji utawala ambao utafinya uhuru na matakwa ya wananchi.Hatukutaka utawala ambao maendeleo, haki na huduma za kijamii hutolewa kwa ubaguzi, rangi na itikadi na fikra tofauti.
Hatimaye tulitapata uhuru ,tukaweka siku ya tar 9/Dec kila mwaka kama ni siku ya kumbukizi ya uhuru wetu. Maana yake sio kukumbuka kuwa siku ya tar 9/Dec/1961 ni siku tuliyopata uhuru, haina maana hiyo.
Ina maana kuwa tunajikumbusha kila mwaka kuyaenzi na kuzidi kuyaimarisha yale yote tuliyokuwa tunayadai kutoka kwa mkoloni,ile misingi tuliyoiamini na kupigania sisi kupata uhuru ndio inapaswa izidi kuimarishwa, pia kuwakumbuka wote waliosaidia nchi yetu kupata uhuru na kuzidi kuenzi fikra na misingi yao.
Ukweli upo wazi kuwa misingi yote na uhuru binafsi wa watu na kimfumo umeyumba sana, ubaguzi umezidi kuwa mpinzani wewe sio mzalendo, kufanya siasa ni uasi,bendera za chama pinzani ni kuhimiza uwasi, uhuru wa vyombo vya habari mfukoni.
Hivyo kuna fikra za makundi mawili kuna watu wanaoamini kwamba.
Kushiriki katika siku ya uhuru haina maana yeyote na sio nguzo ya kuimarisha umoja wa Kitaifa.
Sababu siku hiyo ina kosa maana, kwani ile maana ya uhuru tunaoadhimisha haipo tena, na ukweli ndio huo kuwa uhuru umefinywa,demokrasia inachezewa.
Watu hawa kutohudhuria kwao ni njia ya kuendelea kuonesha hisia zao kwamba uhuru hakuna, demokrasia hakuna.
Mamlaka watakapojirekebisha wanaonekana kuwa wapo tayari kushiriki. Hii ni (Passive Resistance).
Hawa wanaweza kuutaja kama mfano, hiki kitendo cha Mkuu wa Wilaya wa Sumbawanga aliyeagiza Bendera za Chadema kushushwa, hii haina tofauti na wakati wa mkoloni dhidi ya vyama vya ukombozi.
Hawa wanamini kwamba umoja wa Kitaifa sio kufanya sherehe, umoja wa Kitaifa ni kuyasimamia na kuishi katika hizo kumbukizi za uhuru. Wao wanaamini umoja wa kitaifa tayari umeshavurugwa na hao wanaofanya hizi sherehe kwa kutoheshimu na kufuata misingi yote na malengo yaliyofanya tupiganie Uhuru.
Hawa wametafsiri uhuru kwa upana sana. Wakiona ni kupotezeana muda kusherekea uhuru ikiwa hakuna uhuru ni kuunga mkono kufinyangwa kwa uhuru.
Hawa wanaweza kutoa public statement siku ya uhuru ikawa ni statement au ujumbe wa maandishi kwenda kwa umma na watawala wakiwaambia watawala wanapaswa kuheshimu uhuru na demokrasia kwa vitendo kama waasisi wetu walivyofanya na sio kupitia sherehe tuu.Hiyo pia itasomwa na watawala pia ni njia moja wapo pia ya kusherekea.
2. Kuna kundi lina amini kwamba ,siku ya uhuru ni siku ambayo wanapaswa kuhudhuria sababu wanaamini ni siku muhimu ya Kitaifa na ina onganisha watu,n a ni siku ya maslahi ya Taifa Zima.
Njia hii ni (Collaboration), wakiamini kupitia siku hii labda wanaweza toa ujumbe kwa mamlaka juu ya umuhimu wa kuheshimu misingi ya uhuru na demokrasia.
Ila changamoto yake ni kwamba kupata hiyo nafasi ya kutoa ujumbe kwa watawala ni jambo ambalo lipo katika uwezo wao, wanaweza kuamua viongozi wa vyama pinzani wasimame wasalimie tu. Na nafasi inaweza kukosekana.
Ila kama wakipewa nafasi na kuongea hata dakika 5 kuongea kwa kutoa ujumbe wa kudai uhuru na demokrasia itakuwa na maana sana, mbele ya umati wa watu, je nafasi hiyo ipo? Maana unaweza kwenda kushiriki siku ya uhuru hata uhuru wa kuongea na kutoa ujumbe wanaweza nyima watu.
Wote wawili wanapigania uhuru na demokrasia kwa namna wanavyoona ni sahihi.
Abdul Nondo.