Mkuu Nguruvi3, Walipofika wakakuta ugomvi umeisha wakauliza kama kuna tatizo, wewe ukasema hakuna tatizo, unadhani polisi watafanya nini?. Hawata fanya lolote kwako wala kwa mke wako, bali huyo jirani yako aliyeripoti tukio, watarudi nae kituoni kumchukua maelezo!.
Aliyewekewa sumu ni Mwakyembe hajaripoti polisi kuhusu kuwekewa sumu. Aliyepayuka hadharani kuhusu jinai ya sumu ni jirani (Sitta). Polisi wamechukua maelezo ya Sitta na kufanya uchunguzi, wakakuta hakuna jinai ya sumu!. Mwakyembe mwenyewe wala familia yake hawajalalamikia sumu!. Sasa kinachofuatia ni Jirani kushitakiwa kwa kuisumbua polisi na kwa case ya Mwakyembe sio tuu kuisumbua polisi bali uchochezi ili wananchi waichukie serikali yao kwa kuiona ni serikali ya wauaji!.
Mwakiyembe anaumwa, hajalalamikia kupewa sumu. Jirani ndio anae eneza uvumi wa simu ili kuwanyooshea kidole mahasimu wake wa kisiasa!. Sasa kwa vile issue ilikuwa ni kupewa sumu, imethibitika sio sumu!. Mwambieni jirani sasa na atoe uthibitisho, ila its high time Dr. akirudi toka matibabu ya India awaambie Watanzania ukweli wa anachoumwa!.
Mkuu Pasco, nikukumbushe kuwa kuna mtu aliwahi kueneza tuhuma kuhusu wewe nadhani unakumbuka. Yeye alisema pasco ..... kwa kutumia vigezo na hisia.
Wewe ulikuja hapa jamii forum na kutoa maelezo ya kujitosheleza kuwa huna hulka ilitosemwa, ukaenda mbali na kutoa ushahidi wa wewe kuanzia makutopora, chuo kikuu n.k. Hukusema tu 'Sina tabia hiyo' bali ulienda mbali ku-prove beyond doubt.
Serikali imesema 'hakuna sumu' , je inatosha kukanusha madai mazito kama hayo ya maisha ya raia kiongozi?
Pili, kumbu kumbu zinaonyesha kuwa Dr Mwakyembe ameshawahi kufikisha madai ya ajali, na yale mazito sana ya kuuawa kule Morogoro. Serikali haijashughulikia madai hayo. Hii inaondoa kabisa hoja ya kuwa 'hajaripoti polisi' kwasababu hata angeripoti bado hakuna utashi wa kushughulikia kwasababu madai yake yanawagusa watu wazito waliomo na waliostaafu na waliojiuzulu.
Kama madai ya Sitta ni uongo serikali inawajibu wa kumshataki. Haijafanya hivyo na haitafanya hivyo kwa kujua kuwa Sitta anaweza kutoa ushahidi utakaoleta utata. Ndiyo maana PM na kila mkubwa wa serikali anaogopa kuzungumzia tuhuma hizo.
Huwezi kujua mazingira yanayomlazimisha Mwakyembe kukaa kimya. Unakumbuka Said Kubenea alipotoka India alitaka kuitisha mkutano na wanahabari! unajua nini kilitokea hadi leo hajazungumzia suala hilo? Walikamatwa vibaka ili kumzuia 'technically' asizungumzie suala hilo.
Kama madai ni kuisumbua Polisi, iweje polisi hiyo hiyo isisumbuke wakati wa utata wa ajali na tuhuma za mauaji Morogoro?
Kwanini serikali ichague mambo ya kushughulikia yanayomsibu Mwakyembe na si maisha yake as whole!
Hadi tutakapopata ukweli wa jaribio la kumuua kule Morogoro hatutakuwa na imani na taarifa yoyote hasa kutoka Polisi kuhusiana na Mwakyembe! Nitty gritty
Na mwisho, endapo serikali imethibitisha kuwa sio sumu, ilitakiwa iende mbali zaidi. 'Sio sumu' ni kauli inayoweza kutolewa na mtu yoyote. Haya ni madai mazito sana na tayari yapo vichwani mwa watu, huwezi kuyafuta kwa neno moja bila kukata kiu kwa maelezo yanayoeleweka.
Wewe hukusema 'mimi siyo..' ulienda mbali zaidi. Hapo mkuu huoni kuna upungufu kwa serikali hasa tukizingatia unyeti wa suala lenyewe