Nakubaliana na wewe kabisa, lakini kwanini tunafikia mahali kumchoma mtu moto kwa kukwapua? Adhabu kama hiyo inaendana kweli na kosa lenyewe? Na hawa wanaotoa tuhuma (wanaolia mwizi) na ambao ndio wanaotoa hukumu (achomwe moto) na ambao wanatekeleza hukumu hiyo (kuweka matairi na kuni shingoni) kwanini jamii inawavumilia? Sijasikia hata siku moja kuwa fulani ame/wamekamatwa kwa kumchoma mtu aliyedaiwa kuwa ni kibaka?