DC wa Songwe adaiwa kutishia kumuua Mbunge wa Songwe kwa kufuatilia fedha za Wawekezaji wa mazao

Alichofanya Mbunge ni kuwa upande wa wananchi walio mchagua, wakulima hawataki kuuza kwa mfumo wa stakabadhi gharani maana kuna hela walikopeshwa na wafanya biashara, sasa serikali ikisema inunue, wale wafanya biashara watalipwa nini?

DC amekaa pale kipigaji na hawasikilizi wananchi, alipoona wananchi wamekomalia kuikataa stakabadhi gharani akaja na upuuzi mwingine kwamba wafanya biashara waende wakanunulie ufuta hukohuko chunya tofauti na mwanzo ambapo ufuta ulikua unanunuliwa mbalizi, lakini hata hilo pia wafanya biashara hawataki maana hakuna miundo mbinu ya kueleweka, hakuna barabara ya kueleweka, hakuna maghara ya kuhifadhia mazao, hakuna huduma za kibenki, ina maana mtu ana uwezo wa kubeba million 50 anazurura nazo mtaani akitafuta mzigo, vipi kuhusu usalama wake?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Naona vita dhidi ya RC & DC imepamba moto. Kila kona wanasakamwa 😂😂😂. Mama toa listi watu wapone
 
Iko hivi issue pale ni zao la ufuta, kule hua kuna wahindi wanaweza kuingia sasa ili wanunueshambani na wasiguswe wanawahi kukata pesa kwa DC hapo mambo ya stakabadhi ghalani yanapigwa danadana na mkulima akienda kuiuzia serikali bei ni ndogo sasa wanakubaliana kwa hesabu fulani mkuu utachukua kiasi kadhaa, sasa mbunge anaona posho inampita juu kwa juu ndio ugomvi unaanzia hapo sasa

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Mbunge anajimwambafayi, ndiye mfitini na mtaka chokochoko, watoto wa baba mmoja hao. Ndugu wakigombana shika jembe ukalime.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
upinzani haupo....sasa wapambane na nani????? upinzani ndio ulikuwa unawapa kiki....tutokeje???ila wajipange wawatumikie wananchi....
 
Back
Top Bottom