DC wa Songwe adaiwa kutishia kumuua Mbunge wa Songwe kwa kufuatilia fedha za Wawekezaji wa mazao

Safi kabisa endelezeni urithi mlioachiwa na marehemu Jiwe , muasisi wa ubabe , uvunjifu wa sheria , katiba , utekaji , kujimwa bafai , uuaji , ubambikiaji kesi , haya vijana wamerithi utapeli , ufisadi .
Ushuzi tupu.....
hv kila ukilala na kuamka unawaza Magu.....
na lazima ujamber jamber
 
MBUNGE wa Songwe (CCM), Philipo Mulugo, amemtuhumu Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samuel Jeremiah, kwamba ametishia kumuua.

Amedai kuwa chanzo cha kutishiwa na mkuu huyo wa wilaya ni kutokana na kumfuatilia kuhusu matumizi ya fedha za michango ya wawekezaji na anadai kwamba anamkwamisha kufanya maendeleo wilayani hapa.

Mulugo alimweleza hayo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia jenerali Nicodemus Mwangela, mbele ya kikao cha wadau wa zao la ufuta kilichojumuisha watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, madiwani, wanunuzi wa zao hilo, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakulima.

Hili ni tishio la pili la kutishia kuuawa kwa kiongozi baada lile la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mbozi, Hanji Godigodi ambaye alidai kutishiwa kuuawa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Henerico Mkola, na taarifa za tukio hilo kuripotiwa kituo cha polisi Vwawa na namba (RB) MBZ/IR/200/2021.

Akizungumza katika kikao hicho, Mulugo alisema vitisho dhidi yake kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya, vimekuja baada ya kuwa mstari wa mbele kuwatetea wakulima wa zao hilo ambao hawako tayari kwa sasa kupeleka mazao yao kuuza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani uliokuwa umetangazwa na serikali ya wilaya.

Mbunge huyo alisema mkuu huyo wa wilaya pia haelewani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, jambo ambalo amesema si jema kwenye uongozi na linakwamisha maendeleo.

Naye Katibu wa CCM wa Wilaya ya Songwe, Gerald Mwadalu, alipopewa dakika mbili kuzungumza, alimwambia mkuu wa mkoa kuwa kiongozi huyo wa wilaya hana uhusiano mzuri pia na madiwani na viongozi wa chama.

Mwadalu licha ya kukatishwa mara kwa mara na Mkuu wa Mkoa wakati akizungumza, alidai kuwa chama kimejitahidi mara kadhaa kumwita kwenye vikao ili wajadiliane lakini mara zote amekuwa akikaidi.

Katibu huyo alimkabidhi Mkuu wa Mkoa nyaraka kuhusu mwenendo wa mkuu huyo wa wilaya.

Wakati katibu huyo akiendelea kuzungumza huku akirekodiwa na waandishi wa habari, ghafla mkuu wa mkoa aliingilia kati na kuamuru waandishi wa habari kuacha kurekodi mambo anayoyasema.

Pia Mwengela aliagiza polisi kuzishikilia kamera za waandishi hao kabla ya kutoka katika ukumbi wa halmashauri hiyo ambako mkutano huo ulikuwa ukifanyika.

Akijibu tuhuma hizo, Jeremiah alisema kwa kifupi kuwa kama mbunge huyo anao ushahidi wa jambo hilo la kutishiwa maisha, anapaswa kwenda kutoa taarifa polisi.

Naye Mwengela aliingilia kati na baadaye akasema mbali na kuwapatanisha viongozi hao huko nyuma na kudhani yameisha, amejionea hali halisi ilivyo na kwamba kwa hekima alizojaliwa atazidi kuketi nao kwa ajili ya kuleta mshikamano.

Ippmedia
Heheheeeee. The "Original sin" continues tormenting.
 
Huyo Mhe. DC inadaiwa anaundugu na mwendazake, ndiyo maana licha ya malalamiko ya muda mrefu amekuwa akikingiwa kifua.
Nadhani wakati huu wa Mhe. SSH hatomaliza mwaka 2021 bila kutumbuliwa. I bet so
 
Bado hawajamwelewa mama kuhusu Uhuru wahabari na vyombo vyake na Uhuru wakujieleza...sijui kwann
 
Huyu dc japokuwa ni Dr wa phd, lakini hakupaswa kupata hiyo nafasi ni mtu mjanja mjanja sana wa mjini. Mzee wa lumumba huyu Samuel Jeremiah Opulukwa. Ana asili ya kutokea Geita wilaya ya Chato na amshukuru hayati kwa kumnyanyua. Ingekuwa mtu mwingine alitakiwa awe na adabu na bidii kwani hayati ameshaondoka hakuna wa kuwakingia kifua.
 
Mambo ya fweza tu hapo

Ova

Iko hivi issue pale ni zao la ufuta, kule hua kuna wahindi wanaweza kuingia sasa ili wanunueshambani na wasiguswe wanawahi kukata pesa kwa DC hapo mambo ya stakabadhi ghalani yanapigwa danadana na mkulima akienda kuiuzia serikali bei ni ndogo sasa wanakubaliana kwa hesabu fulani mkuu utachukua kiasi kadhaa, sasa mbunge anaona posho inampita juu kwa juu ndio ugomvi unaanzia hapo sasa
 
Alichofanya Mbunge ni kuwa upande wa wananchi walio mchagua, wakulima hawataki kuuza kwa mfumo wa stakabadhi gharani maana kuna hela walikopeshwa na wafanya biashara, sasa serikali ikisema inunue, wale wafanya biashara watalipwa nini?

DC amekaa pale kipigaji na hawasikilizi wananchi, alipoona wananchi wamekomalia kuikataa stakabadhi gharani akaja na upuuzi mwingine kwamba wafanya biashara waende wakanunulie ufuta hukohuko chunya tofauti na mwanzo ambapo ufuta ulikua unanunuliwa mbalizi, lakini hata hilo pia wafanya biashara hawataki maana hakuna miundo mbinu ya kueleweka, hakuna barabara ya kueleweka, hakuna maghara ya kuhifadhia mazao, hakuna huduma za kibenki, ina maana mtu ana uwezo wa kubeba million 50 anazurura nazo mtaani akitafuta mzigo, vipi kuhusu usalama wake?

In short huyo DC ni fucken kabisa
 
MBUNGE wa Songwe (CCM), Philipo Mulugo, amemtuhumu Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samuel Jeremiah, kwamba ametishia kumuua.

Amedai kuwa chanzo cha kutishiwa na mkuu huyo wa wilaya ni kutokana na kumfuatilia kuhusu matumizi ya fedha za michango ya wawekezaji na anadai kwamba anamkwamisha kufanya maendeleo wilayani hapa.

Mulugo alimweleza hayo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia jenerali Nicodemus Mwangela, mbele ya kikao cha wadau wa zao la ufuta kilichojumuisha watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, madiwani, wanunuzi wa zao hilo, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakulima.

Hili ni tishio la pili la kutishia kuuawa kwa kiongozi baada lile la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mbozi, Hanji Godigodi ambaye alidai kutishiwa kuuawa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Henerico Mkola, na taarifa za tukio hilo kuripotiwa kituo cha polisi Vwawa na namba (RB) MBZ/IR/200/2021.

Akizungumza katika kikao hicho, Mulugo alisema vitisho dhidi yake kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya, vimekuja baada ya kuwa mstari wa mbele kuwatetea wakulima wa zao hilo ambao hawako tayari kwa sasa kupeleka mazao yao kuuza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani uliokuwa umetangazwa na serikali ya wilaya.

Mbunge huyo alisema mkuu huyo wa wilaya pia haelewani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, jambo ambalo amesema si jema kwenye uongozi na linakwamisha maendeleo.

Naye Katibu wa CCM wa Wilaya ya Songwe, Gerald Mwadalu, alipopewa dakika mbili kuzungumza, alimwambia mkuu wa mkoa kuwa kiongozi huyo wa wilaya hana uhusiano mzuri pia na madiwani na viongozi wa chama.

Mwadalu licha ya kukatishwa mara kwa mara na Mkuu wa Mkoa wakati akizungumza, alidai kuwa chama kimejitahidi mara kadhaa kumwita kwenye vikao ili wajadiliane lakini mara zote amekuwa akikaidi.

Katibu huyo alimkabidhi Mkuu wa Mkoa nyaraka kuhusu mwenendo wa mkuu huyo wa wilaya.

Wakati katibu huyo akiendelea kuzungumza huku akirekodiwa na waandishi wa habari, ghafla mkuu wa mkoa aliingilia kati na kuamuru waandishi wa habari kuacha kurekodi mambo anayoyasema.

Pia Mwengela aliagiza polisi kuzishikilia kamera za waandishi hao kabla ya kutoka katika ukumbi wa halmashauri hiyo ambako mkutano huo ulikuwa ukifanyika.

Akijibu tuhuma hizo, Jeremiah alisema kwa kifupi kuwa kama mbunge huyo anao ushahidi wa jambo hilo la kutishiwa maisha, anapaswa kwenda kutoa taarifa polisi.

Naye Mwengela aliingilia kati na baadaye akasema mbali na kuwapatanisha viongozi hao huko nyuma na kudhani yameisha, amejionea hali halisi ilivyo na kwamba kwa hekima alizojaliwa atazidi kuketi nao kwa ajili ya kuleta mshikamano.

Ippmedia
Tunaruka masomo ya maadili ya uongozi
 
Fisi na tabia yao, washaanza.
Tuwaache wafu wazikane!
Wanachogombea ni mgao, kuna mmoja kishamlia timing mwenzake.

Upinzani wametuchelewesha ndugu zangu! Haya sasa!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Nyote hamjui hali ya Songwe, DC kajitahidi sana na hiyo wilaya mpya, kapiga kazi mno kwa maendeleo ya Songwe pale Mkwajuni katika sekta zote kuanzia afya, elimu n.k. Mulugo ana tabia za wivu na watu wake aliowapanga wanamfitini sana DC. Dc anasimamia maelekezo lengwa ya Serikali na yupo very strict na ujingaujinga unaoendelea. Watu wa Songwe ni wazito haswa jamaa anawaweza.
 
Nyote hamjui hali ya Songwe, DC kajitahidi sana na hiyo wilaya mpya, kapiga kazi mno kwa maendeleo ya Songwe pale Mkwajuni katika sekta zote kuanzia afya, elimu n.k. Mulugo ana tabia za wivu na watu wake aliowapanga wanamfitini sana DC. Dc anasimamia maelekezo lengwa ya Serikali na yupo very strict na ujingaujinga unaoendelea. Watu wa Songwe ni wazito haswa jamaa anawaweza.
Iko hivi issue pale ni zao la ufuta, kule hua kuna wahindi wanaweza kuingia sasa ili wanunueshambani na wasiguswe wanawahi kukata pesa kwa DC hapo mambo ya stakabadhi ghalani yanapigwa danadana na mkulima akienda kuiuzia serikali bei ni ndogo sasa wanakubaliana kwa hesabu fulani mkuu utachukua kiasi kadhaa, sasa mbunge anaona posho inampita juu kwa juu ndio ugomvi unaanzia hapo sasa

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom