DC TEMEKE AKUTANA NA BARAZA LA WAZEE
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa. Jokate Mwegelo amefanya kikao kifupi na Baraza la Wazee Wilayani hapo. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Temeke (DMDP) leo Julai,30,2021, majira ya saa nne asubuhi kufuatia ombi la Wazee hao.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wa baraza la Wazee, lengo likiwa ni kumkaribisha na kumpongeza Mhe. Mwegelo kwa kuaminiwa miongoni mwa wengi na kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke.
Aidha Mhe. Mwegelo amefurahishwa na uwepo wa Wazee hao, akisema umuhimu wao ni mkubwa katika kuleta maendeleo ya Temeke na hivyo kuwaomba wazee hao kusaidia katika kuwaombea viongozi wa nchi, hasa katika kipindi hiki cha janga la UVIKO 19 na pia ushirikiano juu ya maendeleo ya Temeke.
"..Ninawaomba sana ushirikiano wenu na ushiriki wenu, ili tuweze kuongoza vizuri zaidi".
Katika hatua nyingine Mhe. Mwegelo amewaomba Wazee hao kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Sita katika mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa kuwahamasisha watu wao kufuata mwongozo na taratibu zinazotolewa na Serikali kupitia waataalamu wa afya.
Pia ameeleza namna serikali chini ya Mhe. Rais, Samia Suluhu Hassan ilivyo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya COVID-19.
"... Mheshimiwa Rais amekuwa jemedari na ametuongoza vizuri sana katika haya mapambano .."