DC Shinyanga alazimika kunywa maji ya kisima kuwaondoa hofu wananchi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
jose.jpg

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amelazimika kula chakula na kunywa maji yaliyotoka kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu uliokataliwa na wananchi kwa hofu kuwa wakinywa maji hayo watakufa na wakipikia chakula kitabadilika rangi ya njano.

Mkuu huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho juzi alitaka kusikiliza kero za wananchi na kufahamu kwanini wanaendelea kutumia maji ambayo siyo safi na salama ikiwa mradi upo tangu mwaka 2014 hawajawahi kuyatumia.

Matiro aliyekuwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine na baada ya kusikiliza hoja hiyo walilazimika kuyaonja na kupika chakula kwa haraka na kubainika hayana chumvi wala chakula kilichopikwa kutokuwa cha njano ndipo ilipobainika kuwa walidanganywa kwa sababu za kisiasa.

Chanzo: Habari Leo
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,786
2,000
Aisee hiyo mamlaka ya maji na taka ya huko ni wajanja sana yaani wanamtumia mkuu wa wilaya kama chambo
 

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
2,887
2,000
Yaani hii serikali ya ccm mbovu sana, kisima na mgogoro upo tokea 2014, ndo wanaenda leo!, serikali ya ajabu kabisa hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom