DC Muro matatani kwa deni la miaka mitatu

nyamadoke75

Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
95
Reaction score
288
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameingia matatani na wamiliki wa duka la samani za majumbani la Future correct la jijini Arusha na wanatarajia kumshitaki kwa boss wake ama mahakamani Baada ya kugoma kulipa deni la sh, milioni 1,050,000 kwa muda wa miaka mitatu baada ya kukopa samani za ndani zenye thamani ya sh,milioni 4.4.

Kwa mujibu wa wamiliki wa duka hilo lililopo barabara ya Uhuru (Uhuru Road) jijini Arusha ,Muro ambaye ni mwakilishi wa Rais wilayani humo alikopa TV yenye ukubwa wa inchi 65 yenye thamani ya sh. Mil. 3.2.mnamo Tarehe 10/12/2018.

Pia anadaiwa kukopa radio aina ya (Home thieta) yenye thamani ya Tsh. milioni 1.2 vyote vikiwa na thamani ya Tsh. 4,400,000.

Inadaiwa kuwa siku hiyo baada ya kukabidhiwa mzigo huo Muro alilipa advance ya Tsh. 1,500,000 na deni kubaki Tsh. 2,900,000/.

Mnamo February 2,2020 Muro alilipa sh. Milioni 1 na kubaki sh. Million 1.9, pia tarehe 22/5/2020 alilipa sh. 350,000/ na tarehe 17/6/2020 alilipa sh. 500,000 na hivyo deni kubaki sh. 1,050,000/

Baada ya malipo hayo Muro aliendelea kusumbua deni hilo kwa miaka miwili mfururizo hadi Septemba 5 mwaka huu ambapo alidai lean a hawezi kulipa tena kiasi hicho cha fedha na kuwataka wakalalamike popote.

Lakini baadaye alibadilisha kauli na kudai kwamba atalipa januari mwakani jambo ambalo limesababisha usumbufu kwa mwenye Mali na ukizingatia kwamba wanapaswa kulipa kodi ya Serikali .

Wamiliki wa duka hilo wamempa Siku saba awe amelipa deni hilo kwani kwa kutofanya hivyo watamfikisha mahakàmani .

IMG_20191223_145144.jpg
 
Why wamelete kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi isiwe huko nyuma? Wanajua jery ni chuma muhimu linapokuja swala La ushindi wa ccm
 
Ufipa kila jambo wanalalamikia

Hii awamu haina mwenyewe, alikamatwa kubenea wakasema anaonewa haya ametuhumiwa Muro sijui watasemaje
 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameingia matatani na wamiliki wa duka la samani za majumbani la Future correct la jijini Arusha na wanatarajia kumshitaki kwa boss wake ama mahakamani Baada ya kugoma kulipa deni la sh, milioni 1,050,000 kwa muda wa miaka mitatu baada ya kukopa samani za ndani zenye thamani ya sh,milioni 4.4.

Kwa mujibu wa wamiliki wa duka hilo lililopo barabara ya Uhuru (Uhuru Road) jijini Arusha ,Muro ambaye ni mwakilishi wa Rais wilayani humo alikopa TV yenye ukubwa wa inchi 65 yenye thamani ya sh. Mil. 3.2.mnamo Tarehe 10/12/2018.

Pia anadaiwa kukopa radio aina ya (Home thieta) yenye thamani ya Tsh. milioni 1.2 vyote vikiwa na thamani ya Tsh. 4,400,000.

Inadaiwa kuwa siku hiyo baada ya kukabidhiwa mzigo huo Muro alilipa advance ya Tsh. 1,500,000 na deni kubaki Tsh. 2,900,000/.

Mnamo February 2,2020 Muro alilipa sh. Milioni 1 na kubaki sh. Million 1.9, pia tarehe 22/5/2020 alilipa sh. 350,000/ na tarehe 17/6/2020 alilipa sh. 500,000 na hivyo deni kubaki sh. 1,050,000/

Baada ya malipo hayo Muro aliendelea kusumbua deni hilo kwa miaka miwili mfururizo hadi Septemba 5 mwaka huu ambapo alidai lean a hawezi kulipa tena kiasi hicho cha fedha na kuwataka wakalalamike popote.

Lakini baadaye alibadilisha kauli na kudai kwamba atalipa januari mwakani jambo ambalo limesababisha usumbufu kwa mwenye Mali na ukizingatia kwamba wanapaswa kulipa kodi ya Serikali .

Wamiliki wa duka hilo wamempa Siku saba awe amelipa deni hilo kwani kwa kutofanya hivyo watamfikisha mahakàmani .

View attachment 1564018
Huo ni umbea kuleta Mambo binafsi ya mtu humu
 
Hawa washazoea mterezo
Alipe deni watu waendele kulipa kodi kwa taifa

Ova
 
Back
Top Bottom