DC MSTAAFU AFIA kwenye DALADALA !

DC MSTAAFU AFIA kwenye DALADALA !

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,551
Reaction score
272,295
anaitwa alhaji Musa Samizi , chanzo ni gazeti la nipashe la tarehe 13 nov 2013 , ukurasa wa 8 , Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali inapostahili , AMINA .
 
...Somebody Ongeza Nyama Habari Please. Nakumbuka kama Marehemu aliwahi ama Aligombea kuwa Mbunge wa Jimbo Fulani Kigoma kwenye miaka ya 80 kama Sikosei. Imetokea kwenye Dala2 hapa mjini ama Kigoma? Mwenye taarifa zaidi Ajazie hapa Tafadhali. RIP Mstaafu wetu Mussa Samizi.
 
Ukiona hivyo ujue hakua fisadi tena enzi za Nyerere,na ndiyo maana miaka ya nyuma Ma DC,Ma RPC,Ma Lecturer walikua wanakimbilia kwenye ubunge maana mafao ya kustaafu ubunge ni makubwa tena ndani ya miaka 5 tuu
 
anaitwa alhaji Musa Samizi , chanzo ni gazeti la nipashe la tarehe 13 nov 2013 , ukurasa wa 8 , Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali inapostahili , AMINA .

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuongoza maziko ya Mkuu wa zamani wa Wilaya mbalimbali nchini, Mussa Samizi aliyefariki Dar es Salaam, juzi.


Akizungumza kwa niaba ya familia ya Samizi nyumbani kwake, Tegeta Dar es Salaam, Katibu Mkuu msataafu wa CCM, Yusuf Makamba alisema maziko yatafanyika leo baada ya swala ya adhuhuri.



Makamba alisema, "Nilizungumza na Samizi muda mfupi, baadaye nilipata simu kuwa mtu huyu amefariki... Wale mabwana walipiga baada ya kuchukua simu yake na kuangalia mtu wa mwisho kuzungumza naye.



"Baadaye ya kunieleza kuwa amefariki kwenye daladala, nikawaambia wampeleke Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya taratibu nyingine... Kimsingi alikuwa anakwenda ofisi za TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania)."




Enzi ya uhai wake, Samizi aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Kasulu, Kigoma Mjini, Tabora, Handeni na Moshi mkoani Kilimanjaro ambako alistaafu.



Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Habari Tanzania (Shihata) na Shirika la Ujenzi wa Barabara (Mecco).


Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Camilus Wambura alisema taarifa za msiba huo alipewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana baada ya kutaka apewe ulinzi kwa ajili ya msiba huo.



"Mimi sina taarifa ya aliyekuwa mkuu wa wilaya kufariki akiwa kwenye daladala, ninachojua alikuja Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni leo (jana) asubuhi ili nimpatie walinzi kwa ajili ya kwenda nao kwenye msiba," alisema Wambura.




Ilielezwa kwamba alikuwa anasumbuliwa na kisukari. Samizi ameacha mjane na watoto watatu.

Cc: BabaDesi

 
Last edited by a moderator:
Makamba alisema, "Nilizungumza na Samizi muda mfupi, baadaye nilipata simu kuwa mtu huyu amefariki... Wale mabwana walipiga baada ya kuchukua simu yake na kuangalia mtu wa mwisho kuzungumza naye."Baadaye ya kunieleza kuwa amefariki kwenye daladala, nikawaambia wampeleke Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya taratibu nyingine... Kimsingi alikuwa anakwenda ofisi za TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania)."

Aisee.........:A S 39::A S 39::A S 39:
 
Alazwe mahali panapostahili,,,,,,amen.
 
Kheee huyu hakupewa gari alipostaafu
 
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi Amina!!
Vijana wetu wa siku hizi akifikia wadhifa huo wa kuwa Mkuu wa Wilaya humkuti hata siku moja amepanda daladala
 
Wazee wetu wazamani wengi hawakuwa mafisadi. Ila disadvantage yake wengi wanakufa maskini kwa sasa. Kuna mkuu wa wilaya mstaafu mmoja wa wilaya moja,tunapiga naye mambo mara nyingi. Lakini nikiangalia uwezo wake kwa sasa,namhurumia. Vijana tujitahidi tuwe tuna save na kuinvest kwamaisha yetu ya uzeeni.RIP DC!
 
Wazee wetu wazamani wengi hawakuwa mafisadi. Ila disadvantage yake wengi wanakufa maskini kwa sasa. Kuna mkuu wa wilaya mstaafu mmoja wa wilaya moja,tunapiga naye mambo mara nyingi. Lakini nikiangalia uwezo wake kwa sasa,namhurumia. Vijana tujitahidi tuwe tuna save na kuinvest kwamaisha yetu ya uzeeni.RIP DC!

Yap wengi walikuwa waadilifu lkn ndo hivyo wanaishia kwenye umaskini. Wengi wamewaona hawa na sasa hakuna anayekubali uadilifu, wanapiga tuuuu kwa kwenda mbele
 
Mzee wetu huyo! nimemmiss!


quote_icon.png
By Adrian Stepp
ha hahaha Safari_ni_Safari acha utani kwenye vitu sensitive kama kifo!



Kaka Mzee haonyeshi hata mshtuko wala majonzi......yaani akaamuru tu "mpelekeni

Poleni kwa wote; "InaLiLaah Waina iLLayhi Rajioun" kila kiumbe kitaonja mauti... Leo tupo hatujui kesho nani atatangulia .....Tunamuombea Rehema na alazwe peponi.AMIN
 
Back
Top Bottom