DC kutumia Ofisi ya Umma kwa mambo ya chama ni sawa?

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
35
81
IMG-20240505-WA0003.jpg

IMG-20240505-WA0003.jpg

Habari za wakati huu Wana jukwaa hili.

Leo nimekuja hapa na hoja ya matumizi ya mali za Umma katika shughuli za Chama chochote cha siasa.

Wote tunajua kuwa siyo sahihi na ni kosa kisheria, mali za Umma, mali za serikali kutumika katika shughuli za Chama chochote cha kisiasa.

Zinaweza kutumika katika shughuli za kisiasa, lakini siyo katika shughuli za Chama chochote cha kisiasa.

Hata Ofisi yeyote ya serikali kutumika katika shughuli za Chama chochote cha siasa ni kosa kisheria.

Ngoja niende kwenye hoja ya msingi. Hapo juu niweka taarifa ya kipeperushi chenye taarifa ya Chama kimoja cha siasa hapa nchini CCM.

Tatizo siyo ujumbe uliopo kwenye kipeperushi hicho, hoja yangu wote tuangalie kwenye hicho kipeperushi upande wa kushoto kwa juu ambapo kumezungushiwa Duara.

Hapo kwenye Duara kuna nembo ya Serikali, Bibi na Bwana, lakini kinasema kimetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi ambayo ipo chini ya Simon Simalenga.

Kipeperushi chenyewe kinazungumzia Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, ambapo wanachama wa CCM wanaonekana wakiwa na Mwenyekiti huyo wakifurahi jambo.

Hoja hapa ni hiyo Nembo ya serikali kutumika katika kutangaza shughuli za Chama cha siasa na Ofisi ya serikali kutumika kutangaza shughuli za Chama cha siasa ambacho ni CCM.

Tukumbuke kuwa hii nembo ni mali ya serikali, na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya nayo ni mali ya serikali, inahudumia wananchi wenye itikadi mbalimbali za vyama vya siasa.

Tujiulize kama itakuwa sahihi kama Chama chochote cha upinzani, kazi zake zitatangazwa na Ofisi hiyo ya Mkuu wa Wilaya kama ambavyo imefanyika kwa CCM.

Katika jambo la hajabu, Mkuu wa Wilaya hii amekuwa akisambaza vipeperushi hivi katika mitandao ya kijaa bila ya woga kabisa, anafanya kama jambo halali kabisa huku wateule wake wakiangalia kabisa.

Tunachojua sisi wananchi wenye mlengo mwingine wa vyama tofauti na CCM, Huyu Mkuu wa Wilaya anakosea, anashindwa kutambua kuwa hiyo ni ofsi ya Umma ambayo inatoa huduma kwa wananchi wa vyama vyote.

Sasa Leo mwananchi mwenye itikadi na Chama kingine akiona Mkuu wa Wilaya anapost hicho kipeperushi nini kinakuja kichwani mwake? Anajua kuwa sasa hv Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ni Ofisi ya CCM.

Leo sisi wananchi wa Chama pinzani, tukifanyiwa jinai yeyote na CCM kwenye hii Wilaya hatuwezi kwenda kushitaki kwenye Ofisi ya Mkuu huyu wa Wilaya na tukasikilizwa na kupata haki.

Tunajua zipo mamlaka za huyu DC, ipo sekratalieti ya utumishi wa Umma, ipo mamlaka yake ya uteuzi, lakini yupo kiongozi wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa ambapo wote hao wanaona na wamekaa kimya bila ya kuchukua hatua.

Hili ni kosa kabisa kisheria, Mkuu wa Wilaya kutumia Mali za Umma ikiwemo Ofisi katika shughuli za Chama chochote cha siasa.

Simalenga anatakiwa kutambua kuwa Nembo na Ofisi yake vyote ni mali za Umma, ni mali za wananchi wote, hivyo Hana mamlaka ya kuvitumia kwa kazi za Chama chochote cha siasa.
 
Mkuu wa kaya aliyepita na wa sasa wamewahi fanyia kikao cha kijani nyumba nyeupe
 
Cha ajabu Nini anawakaribisha wanachama wa chama tawala kuwa wahidhirie huo mkutano na yeye atakuwepi kusikiliza kero zao na kuzipa ufumbuzi

Kionhozo wa chama tawala kutembelea eneo lako kuangalia utekelezaji wa Ilani yake lazima kiongozi wa Serikali utoke ukampokee
 
Back
Top Bottom