comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Wanajamvi,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambae pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam Mh Ally Hapi amesema posho ambazo zimefutwa ni zile zisizo katika utaratibu amesema kuna posho zimebuniwa na madiwani ambazo hazikubaliki mfano wa posho zilizozuiliwa ni posho za kuwajengea uwezo madiwani, posho ya vitafunwa.
Aidha kuna posho zipo kisheria na zipo katika utaratibu hivyo zitaendelea kulipwa kwa mujibu wa sheria na taratibu ametaja hizo ni posho za sitting allowance (vikao vya kisheria na vilivyokatika utaratibu), Vikao vya kamati za tenda za Manunuzi, Posho za uhamisho zipo katika utaratibu kisheria hizo zitaendelea kulipwa
Mh Hapi amesema agizo la Waziri Mkuu lieleweke hivyo sio kuchanganya watu waelewe posho zote zisizo katika utaratibu zimefutwa na amewaasa Wakurugenzi kutowalipa madiwani posho zisizo kwenye utaratibu wa posho kisheria.
Chanzo: Clouds tv