DC Kihongosi: Wanaohoji mimi kuwachapa bakora Wafanyabiashara hawana hoja. Niliowachapa wamelipa sh 5,400,000.00 kama fidia

Kwani kunashida gani kuwachapa viboko hao wahujumu uchumi wa taifa?? Kweli wewe unaona ni haki kununua madawati yaliyogharimu Laki na zaidi kwa shs 500??!! Utakuwa unamatatizo ya akili siyo bure!
Muhujumu uchumi anatakiwa apelekwe mahakamani akashtakiwe kwa sheria ya uhujumu uchumi sheria si ipo?
Kisheria dc amepotoka
 
Ni
Mbona fedha waliyotozwa haitoshi? Dawati na kiti gharama ni shs. 100,000/=, fedha zilizolipwa zinatosha seti 54 tu wakati seti zilizoibwa ni zaidi ya 100.
Ni usanii hakuna fedha zilizolipwa.
 
Hoja sio kulipa fidia,

Wala swala la Uzalendo;

Hoja hapa ni kwa DC kuchapa viboko wananchi, jukumu ambalo hakutumwa alifanye.

Wakoloni wachape Babu zetu viboko ,

Viongozi wetu nao watuchape. Hapana.

DC aombe radhi. Huo ndio uungwana.
 
Mkuu wa wilaya ya Arusha mh Kihongosi leo amepokea fidia ya sh 5.4 milioni kutoka kwa wafanyabiashara wa chuma chakavu kama fidia ya vitu walivyouziwa na wanafunzi kinyume cha sheria.

Kihongosi amesema fedha hizo xitatumika kutengeneza madawati mapya.

Kadhalika DC Kihongosi amewaponda wanaomsakama mitandaoni kwa hatua yake ya kuwachapa bakora wafanyabiashara hao na kusema wanaolalamika hawana hoja ya msingi na siyo wazalendo kwa taifa letu.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Sina tatizo na kilichotokea ila wasiwasi wangu tu ni kwamba kwa jinsi Watanzania walivyo na Ugumu wa Pesa lakini huku imechangwa upesi sana.
 
Kwani kunashida gani kuwachapa viboko hao wahujumu uchumi wa taifa?? Kweli wewe unaona ni haki kununua madawati yaliyogharimu Laki na zaidi kwa shs 500??!! Utakuwa unamatatizo ya akili siyo bure!
Kwahiyo hatuna Mahakama tena bali sheria mkononi kwa wateuliwa!Kesho akiamua kuwapiga mateke,ngumi au hata kuwaingilia kinyume na maumbile kwa kile anachokiita uzalendo,tutamlaumu vipi wakati tumemsifu alivyojigeuza mahakama na kutoa adhabu?
 
Hoja sio kulipa fidia,

Wala swala la Uzalendo;

Hoja hapa ni kwa DC kuchapa viboko wananchi, jukumu ambalo hakutumwa alifanye.

Wakoloni wachape Babu zetu viboko ,

Viongozi wetu nao watuchape. Hapana.

DC aombe radhi. Huo ndio uungwana.
Makada wenzako wanaunga mkono humu jukwaani!
 
Ana hoja za kijinga sana huyo jamaa, kuwachapa na kulipa bila mahakama kudhibitisha makosa ya hao watu huo sio utawala wa sheria bali ni uhalifu. Ni sawa na wale majambazi wanaoteka magari na kupiga watu, kisha hizo pesa za wizi wanaenda kusaidia jamii zao. Kama kiongozi anaweza kupiga watu ili walipe, mahakama ziko kwa ajili gani?
Usisahau kwenye katiba wanasema kuna sheria ndogondogo pia ambazo hutajwa au kupendekezwa na wakubwa wa sehemu husika, ila sidhani kama alikosea na ndio lilikuwa wazo langu kwa matraffic wa barabarani kuwa sio lazima kila siku eti faini hapana muda mwingne mshushe mtu kwenye gari mwambie apige pushapu sidhani kama atarudia tena
 
Hoja sio kulipa fidia,

Wala swala la Uzalendo;

Hoja hapa ni kwa DC kuchapa viboko wananchi, jukumu ambalo hakutumwa alifanye.

Wakoloni wachape Babu zetu viboko ,

Viongozi wetu nao watuchape. Hapana.

DC aombe radhi. Huo ndio uungwana.
Sometimes you write sense
 
Wamelipa kwa hukumu ipi? Hiyo kesi imesikilizwa mahakama gani? Aseee Watanzania tumekuwa wapumbavu sana.
 
Daah nisije nikapigwa ban tena daaa .. mods msipige tu watu ban ujinga kama huu kama mnasapoti na nyie mjipige ban shenzi kabisa
 
Hivi huyo mpumbavu alishaona Magufuli anacharaza watu viboko?

Je bila kuwacharaza viboko wasingelipa hiyo hela? Huu ni upuuzi wa hali ya juu sema tu wengi hawajaelimika, huyu alikua ni wa kufungulia mashtaka kabisa, yeye anapiga mtu kama nani? Ni mahakama au?
Sheria inaruhusu mkuu wa wilaya kufanya hivo.
 
Si makalioni tu Mkuu popote pale. Hizi sheria za mwaka 47 zimeshapitwa na wakati na ndiyo sababu tuna mahakama ingawaje haziko huru tena kwani maamuzi yanafanywa na huyo anayejiita mwendawazimu, hivyo ni lazima zipigwe vita kwa nguvu zote.
Itakuwa anajua mahakama haziko huru ndo maana akaamua kujichulu;ia sheria na kuwalipisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom