Muelewe tu, anamaanisha kifo ni mapenzi ya Mungu, kwahiyo kwa kifo kile, yeye akawa raisi.Labda Kiswahili ni kigumu au elimu ndogo ila Samia anavyosema kuwa kwa sasa yuko pale kwa sababu ya kudra za Mwenyezi Mungu na matakwa ya kikatiba, kwani akichaguliwa hatakaa pale kwa sababu ya matakwa ya kikatiba na kudra za Mwenyezi Mungu?
Tanzania ipo kwenye kizungumkuti kikubwa sana....Samia aliwaambia CCM wenzake waache hizi vurugu mpaka 2025, leo ajabu yeye mwenyewe ndie amezianzisha, hana kumbukumbu kabisa.