JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
241
500
"NAMUUNGA MKONO MAMA 2025"

"Ni kweli kabisa 2025 ni mwaka wa kumuweka Rais Mwanamke Ikulu, ni wakati sasa wa Wanawake wote kuungana na kutumia fursa hii kufanikisha hili na kuendelea kuandika historia Tanzania, naamini Wanaume pia watatuunga mkono maana nia ya Mama kulitumikia Taifa letu wote tumeiona.

Lakini pia kwa kutambua wanawake tumefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa Nchi yetu, kujenga siasa za Nchi yetu. Na pia Kama Mhe Rais alivyosema tumekuwa chachu nyuma ya wanaume wengi kupata vyeo vya juu.

Ni wakati wetu sasa!

Namuunga mkono Mama, 2025 twende na Mama." - Ameandika Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Jokate Mwegelo kwenye ukurasa wake Rasmi wa twitter

IMG-20210915-WA0132.jpg

Jakate.PNG
 

Lutandagula

JF-Expert Member
Apr 8, 2018
1,472
2,000
Naona mwanamke kashaota mapembe sasa,rungu limeshamfikia kichaa,kaonja ladha ya urais kaona ni tamu mno!,CCM msitufanye sisi wajanga kujiapisha na kujipigia kura kwa sasa huo ni upumbavu na udikteta wa kijinga, nawambieni ipo siku Mungu atawapiga na kitu kizito kichwani hamtaamini shenzi nyie!
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,175
2,000
Labda Kiswahili ni kigumu au elimu ndogo ila Samia anavyosema kuwa kwa sasa yuko pale kwa sababu ya kudra za Mwenyezi Mungu na matakwa ya kikatiba, kwani akichaguliwa hatakaa pale kwa sababu ya matakwa ya kikatiba na kudra za Mwenyezi Mungu?
 

Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,159
2,000
Labda Kiswahili ni kigumu au elimu ndogo ila Samia anavyosema kuwa kwa sasa yuko pale kwa sababu ya kudra za Mwenyezi Mungu na matakwa ya kikatiba, kwani akichaguliwa hatakaa pale kwa sababu ya matakwa ya kikatiba na kudra za Mwenyezi Mungu?
Muelewe tu, anamaanisha kifo ni mapenzi ya Mungu, kwahiyo kwa kifo kile, yeye akawa raisi.

Anaenda mbali zaidi na kusema, 2025 mwendo ni ule ule, goli la mkono, "...hata usipotupigia kura, ccm ndio itakayounda serikali..", maneno kama hayo yaliwahi kutamkwa kipindi fulani nadhani.

Hitimisho ni kuwa, KUDRA za mwenyezi Mungu hazirihusu goli la mkono, hivyo hawajawahi kumuhitaji Mungu kwenye dhuluma wanazofanya.
 

Kitimoto

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
927
250
Mhe. awe anatanguliza kwa kusema Mungu akipenda namuunga mkono Rais Samia 2025.

Mhe. Rais akumbuke bado ana miaka takribani 4 ya kuongoza, itategemea nini amewafanyia Watanzania na pia akumbuke CCM ina wenyewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom