johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 104,319
- 183,600
Nimeona mkuu wa mkoa Makonda ameshaleta kokoto, mchanga na matofari tayari kwa ujenzi wa ofisi za walimu. Sasa ningekuomba mkuu wa wilaya utujulishe yale mabanda ya biashara yaliyojazana pale shuleni ni mali ya nani? Ikumbukwe mabanda yale yamejengwa wakati serikali ya mtaa ikiongozwa na UKAWA yaani Mwenyekiti na wajumbe Cuf na diwani wa Chadema. Kabla ya hapo chini ya uongozi wa serikali ya mtaa wa CCM uwanja wa michezo shuleni hapo na ule wa makaburi uliuzwa hali iliyowafanya wananchi kukasirika na hatimaye kuichagua Cuf. Dc Salum Hapi najua unapita humu hivyo nasubiria majibu hapa hapa vinginevyo nitamwomba Lizaboni aniulizie mkoani. Nawasilisha!