Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 899
- 999
DC HAPI AENDELEA NA ZIARA YAKE KATA YA MWANANYAMALA-KINONDONI
Akiwa na siku 183 tangu kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni 18/April/2016, Ally Salum Hapi ameendelea kutekeleza kwa vitendo majukumu aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli.
Licha ya kusimamia vyema suala la watumishi hewa katika wilaya yake, akisimamia vyema na Kulimaliza suala la upatikanaji wa madawati katika wilaya yake ambapo ilikuwa changamoto kubwa tangu kutangazwa kwa Elimu bure.
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi kwa kutambua umuhimu wa majukumu yake na kutimimiza ule usemi wa HAPA KAZI TU hakuona ni vyema kukaa ofisini na kusubiri kuletewa mafaili mezani, sasa ameamua kuwafata wananchi popote walipo akipita kata hadi kata kutatua na kusikiliza kero za wananchi wake.
Ili kutimiza azma hiyo Mkuu wa Wilaya jana ameendelea na ziara yake katika kata ya mwananyamala ambapo pia alishiriki kikao cha Kamati ya Maendeleo ya kata (WADC na kufanya mkutano na wananchi eneo la Mwananyamala
Katika ziara yake, mheshimiwa Hapi
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni, amewataka wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuacha kutumia vibaya mihuri yao kwa kuuza viwanja vya wazi, kusababisha migogoro ya ardhi, kuwadidimiza wananchi maskini na kuwapa kipaumbele matajiri hata kama hawana haki.
Hapi amewataka wenyeviti hao licha ya kuwa wamechaguliwa na wananchi lakini, wazingatie sheria na kanuni za uongozi, kwani wengi wao wanatumia mihuri hiyo vibaya, ikiwa pamoja na kushiriki kuuza sehemu za wazi.
Akizungumza na watumishi wa Wilaya wakati wa ziara yake kwenye kata za Wilaya hiyo,kukagua utekelezaji wa ilani ya CHAMA CHA MAPINDUZI na Miradi ya maendeleo kwenye wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya ya kinondoni Ally hapi amesema Halmashali ya Manispaa Ya Kinondoni imetenga mil 140 kwajili ya maendeleo ya mtaa wa kambangwa fedha hizo zinatosha kukamilisha ujenzi wa soko la kabangwa pamoja na miundombinu inayohitajika katika soko Hilo.
Amesema ujenzi huo utafanikisha wafanyabiashara wote kwenye vibanda chakavu kupata Vizimba vipya na kuboresha biashara zao.
Mkuu huyo wa Wilaya Ally Hapi pia ametoa muda wa wiki mbili kwa Mtendaji na Afisa Afya wa Kata ya Kambagwa kuhakikisha Mitaro yote ya maji Machafu inasafishwa na kuwasimamia wafanyabiashara Kuweka vifaa vya kuwekea takataka katika Maeneo yao.
Aidha amepiga marufuku vibanda vyote vya kuonyesha video pamoja na michezo ya kamali muda wa kazi na kuwataka wazazi na walezi kuweka uangalizi kwa watoto wao.